Adabu za sadaka za kujitolea


N

njia ya saada

Senior Member
Joined
Sep 3, 2018
Messages
110
Likes
84
Points
45
N

njia ya saada

Senior Member
Joined Sep 3, 2018
110 84 45
1. Adabu za lazima
1. Kufanya kwa ajili ya Mwenyezi Mungu U (Ikhlaas) – Anatoa Zaka kwa lengo la kutaka radhi ya Mwenyezi Mungu, sio kwamba aonekane au atajwe vizuri na watu.

2. Kujiepusha na kujisifu (kwamba ni mtoaji) na kuudhi watu (kwa kutoa kwake) kwa kauli ya Mwenyezi Mungu U: { Enyi mlioamini! Msiharibu sadaka zenu kwa masumbulizi na udhia}(Al-Baqarah: 264).

2. Adabu zinazopendekezwa.
1. Inapendekezwa kwa muislamu kutoa sadaka kwa wanaohitajia miongoni mwa jamaa zake ambao sio jukumu lake kuwalisha, kama vile ami zake, na wajomba zakle, na mke kumpa mumewe aliyefakiri, na wengineo, na hivi ni bora kuliko kuwapa sadaka watu wasiokuwa hawa, Anasema Mwenyezi Mungu (s.w): “Yatima aliye jamaa (na asiyekuwa jamaa)” (Al-Balad: 15).

Na katika Hadith: (Hakika ya sadaka kwa masikini ni sadaka, na kwa jamaa yako ni mambo mawili: sadaka na kuunganisha kizazi) [Imepokewa na Nasaai.].

2. Kuchagua katika mali yake mali iliyohalali, nzuri, yanayompendeza nafsiyake. Anasema Mwenyezi Mungu U: {Hamtoweza kuufikia wema (khasa) mpaka mtoe katika vile mnavyovipenda} (Aali Imran: 92)

3. Kufanya siri katika kuitoa; kwa kuwa hivi ndio karibu zaidi na Ikhlas, na ni mbali sana na kuonesha watu na kutaka kusifiwa, na ni karibu zaidi katika kumkirimu fakiri, Anasema Mwenyezi Mungu U: {Mkizidhihirisha sadaka ni vizuri, na mkizificha mkawapa mafakiri kwa siri basi hivyo ni kheri } (Al-Baqarah: 271).

Na ikiwa katika kuitoa kwa kuonekana kuna maslahi, kama vile watu kuiga kutoa, na kuwatia moyo waliohudhuria, basi inapendekezwa kuitoa wazi, pamoja na kuchunga muislamu niya yake nakuilazimsha juu ya ikhlas

Kutoa sadaka anayoweza hata kama ni kidogo sana, amesema Mtume ﷺ: (Uogopeni moto japo kwa ubali wa tende) [Imepokewa na Bukhari.]
https://www.al-feqh.com/sw/sadaka-ya-kujitolea
 
Madam Mwajuma

Madam Mwajuma

Verified Member
Joined
Sep 13, 2014
Messages
6,862
Likes
5,163
Points
280
Madam Mwajuma

Madam Mwajuma

Verified Member
Joined Sep 13, 2014
6,862 5,163 280
Takbir
 

Forum statistics

Threads 1,237,558
Members 475,562
Posts 29,293,415