Hismastersvoice
JF-Expert Member
- Jan 26, 2013
- 18,587
- 22,189
Serikali iliamua kuanzisha shirika la kuendeleza viwanda vidogo (SIDO) kwa lengo la kuwasaidia wananchi wajikwamue kiuchumi kwa kuzalisha bidhaa zao ndogondogo za matumizi ya kilasiku.
Kutokana na mpango huo wa Serikali, SIDO inatakiwa iwe mbele kuhakikisha inaisaidia Serikali katika kuwaelimisha Wananchi ujuzi wa kutengeneza bidhaa za viwanda vidogovidogo, lakini mambo ni tofauti kabisa! SIDO badala yake inawakomoa Wananchi wanaotafuta ujuzi wa kutengeneza bidhaa za mitaani mfano sabuni, mifuko ya karatasi ambavyo kwa sasa ni muhimu sana kimazingira.
Uasi wa SIDO dhidi ya serikali unaanzia pale inapoandaa kozi ya siku tano kutengeneza sabuni kwa shilingi lakini moja na nusu (150,000/=)! Ni kiwango cha ada cha juu sana kuliko ada inayotozwa kwenye vyuo vikuu vyetu! Kama SIDO inania ya dhati ya kuipeleka Tanzania kwenye viwanda haina budi kupunguza tozo hizo za ada zilingane na uwezo wa wananchi;
Pia ni jukumu la serikali kuingilia kati na kuiweka SIDO mikononi mwake kama nguzo ya kulipeleka taifa kwenye uchumi wa viwanda na kulirudisha taifa kwenye umaarufu wa SIDO ya miaka ya sabini.
Ninawasilisha.