Boramaisha
JF-Expert Member
- Apr 29, 2009
- 820
- 18
Mnashangaa nini na ndio ubepari wenyewe huo! Mmeyavulia nguo yakogeni tu.
Sasa mkuu mwenye habari anakwambia bei mashuleni au mahotelini yameandikwa interms of dola na siyo TZs. Sasa kwa mtanzania unapesa zako mfukoni za TZS umefika hotelini usiku hizo dola unazipata wapi au ndo kugongwa bei yoyote. Mambo mengine serikali yetu inaexpose tu their inferiolity. Na hapo wanakwambia tanzania ni soveiregnity lakini ni kwenye mipaka tu na madaraka mambo mengine wanaamuliwa tu na ngozi nyeupe. It sucks!.Nyambala,
Hiyo sheria bado ipo (legal tender is still a Tanzanian Shilling - TZS!). Cha msingi watu kujua ni kwamba, wafanyabiashara wanaweza kuweka bei in any currency provided the TZS equivalent is also provided/declared. Zaidi ya hapo wafanyabiashara kisheria hawatakiwi 'kumlazimisha' mteja kufanya malipo kwa currency tofauti na TZS (i.e. ukitoa/lipa TZS na muuzaji akikataa kupokea anavunja sheria). Hayo yote ni kwa biashara au mauzo yanayofanyika ndani ya Tanzania.
Hapa Tanzania hilo jambo limepigiwa kelele wee mpaka kuna wakati lilifikishwa bungeni lakini wapi,hapa jirani yetu Kenya huwezi ukaenda dukani eti kitu kinauzwa kwa dola ,hakuna hata nchi masikini kama Malawi hakuna eti kulipa kwa dola ,lakini tusilaumu tu serikali huu ndio mfumo ambao sisi wananchi tumeulea angalia hata humu JF kwenye matangazo members wanauza vi laptop vyao eti kwa dola,hata magari wanauza kwa dola.Ndugu zangu wana JF nisaidieni, nilalamike wapi?
Narudisha watoto wangu shule na mwingine mmoja anaanza shule, kufika tu shuleni naambiwa ada ni dola za kimarekani kadhaaa, nashangaa, anayenihudumia ananiambia lakini unaweza kulipa kwa shilingi ila utabadilisha kwa kiwango cha 1,400/= kwa dola moja, naendelea kushangaaaa.
Naenda hotelini bagamoyo, nimeamua kupunguza uchovu wa pilika za Dar, nafika naambiwa bia dola mbili, chumba dola kadhaa, nashangaa, nauliza kwani hapa ni marekani? naambiwa shilingi haina msimamo. Nashangaaaaa
Napewa safari ya kikazi kwenda Afrika Kusini, najua niko kwa watu na pesa inayoweza kunisaidia ni Dola au Randi. Nikiwa hotelini nataka kulipa nilichotumia kwa dola, mhudumu ananiambia hapana nenda pale badilisha halafu nipe randi. nashangaaaaaaa.
Who is suppose to manage this in our country? Mr Ndulu? Mr Mkullo? au Mh Raisi? Naamini mtanisaidia. Hili jambo linanikera sana na sielewi ni nani sahihi wa kumlalamikia.
Respct.