ACT-Wazalendo Zanzibar siyo chama kipya bali ni chama kilichojiengua kutoka CUF na kwenda ACT-Wazalendo

rose mzalendo

Member
Mar 5, 2019
71
114
Chama cha ACT-wazalendo ambacho ni CUF iliyojiengua ni Chama ambacho kwa muda mrefu sasa kimekuwa kikitumiwa na Mataifa ya nje (mabeberu) kuratibu na kuanzisha Vurugu na migogoro ya kisiasa ikiwa na lengo la kuhakikisha mikakati ya kufanikisha muungano wa Tanzania Bara na Tanzania Visiwani unavunjika.

ACT-Wazalendo pasipo kuzingatia Sheria na kanuni za Uchaguzi imeituhumu NEC na ZEC kuwa zinashirikiana na vyombo vya Dola kuhakikishisha wana kihujumu chama hicho kwa kuwaondoa kwa kuwaundia mizengwe Wagombea wao ili wagombea wa CCM wapite bila kupingwa.

ACT-wazalendo (CUF iliyojiengeua) ni Chama ambacho kinaogozwa bila kuzingatia sheria na kanuni jambo ambalo linadhihirisha kuwa na uwezo mdogo hasa kufuatia Sakata la mgogoro uliowahi kutokea kati CUF ya MAALIM SELF SHAARIF HAMMAD dhidi ya CUF ya PROF. IBRAHIM JUMA LIPUMBA hivyo ACT-Wazalendo (CUF ILIYOJIENGUA) ni chama ambacho hakina weledi kwenye mambo ya kisheria na kikanuni hasa za Nchi na hata za Chama ambazo wamezitunga na kujiwekea wenyewe.

Chama cha ACT-Wazalendo kinapigania kushinda Urais ili Mataifa ya nje yaisaidie Serikali ya Zanzibar kuuvunja muungano, watahakikisha Zanzibar inakuwa Dola ya kiislam, na kuratibu makundi ya kigaidi kuidhofisha Tanzania Bara, pia yatahakikisha Zanzibar inaongozwa Kisultan.

Nakiasa Chama cha ACT-Wazalendo Zanzibar kijikite zaidi kutangaza sera na kuacha propaganda, kwa kuwa ACT- Wazalendo Zanzibar wameshindwa kunadi sera za Chama hicho na kuendelea kunadi sera za chama cha CUF, haya ndiyo madhara ya kuhama chama na kuhamia chama kipya bila kujitathimini na kuzifahamu vyema sera za chama kipya.
 
Chama cha ACT-Wazalendo kinapigania kushinda Urais ili Mataifa ya nje yaisaidie Serikali ya Zanzibar kuuvunja muungano, watahakikisha Zanzibar inakuwa Dola ya kiislam, na kuratibu makundi ya kigaidi kuidhofisha Tanzania Bara, pia yatahakikisha Zanzibar inaongozwa Kisultan.
Hii ndiyo sababu itakayofanya tuichague upinzani zanzibar!
Maadam dikteta la bara limeendelea kusigina katiba na sheria hakuna budi kuwa na "strategic area" iliyo karibu na bara kwa ajili ya kuleta uhuru wa kweli
 
2499918_IMG_20200828_140607.jpg



2499917_IMG_20200828_140614.jpg
 
Back
Top Bottom