gigabyte
JF-Expert Member
- May 27, 2015
- 5,196
- 5,764
Uko kwingine ndo kamwe huwezi kufanikiwa kwa lolote.kama tu vyama vya siasa vinakutana na madhila yote hayo na viko kisheria na katiba iliyopo inatamka wazi uwepo wake usitegemee hayo makundi mengine yatafanikiwa hicho unachokitaka kabla hawajakutana na rungu kubwa la serikali ya chama kinachoogopa hoja.Njia pekee na rahisi ni hii hii ya siasa na hiyo misuguano ipo tu na kamwe haiwezi kuacha kuwepo kwasababu ya upuuzi wetu kama binadamu wakiafrika.watu watakua wanakuja nakupita hadi mambo yatakapokaa sawa kwasababu watu wanaelimika na kujua haki zao.Kuna muda utafika wengine wataamua kutumia njia ambazo wamewai kuzitumia wengine lakini hiyo huwa ni hatua ya mbali sana kwenye madai kama hayo.Tatizo hapa sio vyama vya siasa au siasa tatizo hapa ni ukondoo miongoni wa wananchi wengi ndo maana wanasiasa wenye madaraka wanatumia hiyo nafasi kuamua vile wanataka wao.Niliyoyasema mimi ni yale yatakayotuwezesha kupanua hii kampeni ya katiba mpya badala ya sasa ambako inachukuliwa kama a political agenda ya chama cha siasa tu.
Lazima lobbying ifanyike kwenye taasisi mbalimbali za umma ikiwemo viongozi wa dini Baraza la viongozi wa dini chini ya Askofu Paul Ruzoka linaweza a good starting point ya kumshawishi rais aanzishe mazungumzo na vyama vya siasa.
Tusitake kuwa kwenye misigano ya kisiasa tutashinda tupate kila kitu no let's go to the table with least expectation lakini tujue ipi itakuwa last position yetu.
Hii hatua ya kufanya siasa kwa kuwindana na mabomu ya machozi inazalisha extremism at the same time haina afya kabisa hasa kwa taifa.
Hebu tuanze kutafuta lobbyists wazuri mambo yataanza kwenda.