ACT-Wazalendo yatoa masharti Uchaguzi Mdogo Konde

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,992
2,000
CHAMA cha ACT-Wazalendo kimesema hakitashiriki uchaguzi mdogo wa Jimbo la Konde hadi watumishi wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), waliohusika katika uchaguzi uliopita watakapowajibishwa.

kabwe.jpg

Akisoma maazimio ya chama katika eneo la Konde Pemba wakati wa ziara maalum ya viongozi wa ACT-Wazalendo, Kiongozi Mkuu wa chama hicho, Zitto Kabwe alisema chama hicho hakitashiriki uchaguzi huo hadi watumishi wa ZEC wawajibishwe.

Zitto alisema kuwa wananchi ambao waliumizwa na kuteswa kwenye uchaguzi walipwe fidia, ili wapate haki yao.

Alisema azimio lingine ni pamoja wa kuundwa kwa kamati ya kisheria ya kuratibu maridhiano ya kijamiii, ili ZEC ionyeshe mwelekeo nini kifanyike yazidi kukua.

Aidha, azimio la tatu ni kuitaka Serikali ya Zanzibar na ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuzifanyia marekebisho sheria zote za uchaguzi kabla ya mwaka 2025, ili uchaguzi mkuu ujao uwe sawa katika kushindania nafasi za uongozi.

Alisema halitakuwa jambo la busara kila baada ya uchaguzi kuirudisha Zanzibar nyuma kimaendeleo, ni vyema umoja na maridhiano ya kisiasa kudumu muda wote.

Mjumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho ambaye ni Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar, Othman Masoud Othman, alisema kilichomfanya mbunge mteule wa Konde kutoka CCM kuachia ngazi ni mazungumzo.

Alisema vilelezo na ushahidi waliowasilisha ni matunda na matokeo chanya yaliyopatikana ya kujiuzulu kwa mbuge mteule wa jimbo hilo.

Makamu Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo, Juma Duni Haji, alisema hawako tayari kuingia kwenye uchaguzi wakati walioharibu uchaguzi huo hawajachukuliwa hatua zozote.

Chanzo: Nipashe

Muuza viatu

JF-Expert Member
May 14, 2020
3,288
2,000
Kiuhalisia ei si ti hawapo tayar kwa uchaguz na ndio maana wametoa masharti ambayo hayawezekani
 
Mr Dudumizi

JF-Expert Member
Sep 9, 2020
2,310
2,000
Ukisusa wenzio wala... nashauri mzee wa ubwabwa aje aweke mgombea. Na wapemba wanavyopenda ubwabwa hapo lazima chama chake kitashinda kwa kishindo.
 
PSPA Pure'12 udsm

JF-Expert Member
Jan 11, 2013
824
500
Mwanzo niliwabeza CHADEMA kwa kujiweka pembeni kushiriki hizi chaguzi ndogo. Lakini hata ACT wameelewa kwa vitendo kwamba Upya wa Serikali sio upya wa CCM na madhambi yake.
 
BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,992
2,000
Kwa hii Serikali haramu sidhani kama watafanya lolote. Kwa ufinyu wa akili yao wanadhani wana hati miliki ya Tanzania.
Nawapongeza ACT kwa kunarrow their demands ili nchi iendelee kusonga mbele katika mwelekeo sahihi
 
denooJ

JF-Expert Member
Mar 31, 2020
10,412
2,000
CCM wanavyopenda kulindana sidhani kama hao ACT madai yao yatafanyiwa kazi, na kama watarudi kwenye uchaguzi bila madai yao kufanyiwa kazi halafu "wakipigwa" tena nawashauri wafunge midomo yao tu.
 
Muuza viatu

JF-Expert Member
May 14, 2020
3,288
2,000
CCM wanavyopenda kulindana sidhani kama hao ACT madai yao yatafanyiwa kazi, na kama watarudi kwenye uchaguzi bila madai yao kufanyiwa kazi halafu "wakipigwa" tena nawashauri wafunge midomo yao tu.
Na hata yakifanyiwa kazi patahitajika muda wa kutosha hii itapelekea uchaguz mdogo kusubir sana na baadh ya sheria kubadilishwa husuusan sheria za uchaguz
 
PTER

JF-Expert Member
Dec 28, 2014
17,521
2,000
Kwa hii Serikali haramu sidhani kama watafanya lolote. Kwa ufinyu wa akili yao wanadhani wana hati miliki ya Tanzania.
Kuna eneo ambalo vyama vya upinzani vimefeli kwa kampeni zake za mabadiliko makubwa ya electoral laws.
1. Hawana taarifa za uchaguzi za madhira yote kuwa documented na kusambaza kwa wananchi ikiwemo vyombo vya habari na Tume ya uchaguzi yenyewe.
ACT walijitahidi kwenye uchaguzi wa 2020.

2. Kufanya lobbying kwenye mashirika ya haki binadamu ya ndani pamoja na taasisi za kiraia kufanya mijadala na mihadhala juu ya mabadiliko ya electoral laws ikiwemo mabadiliko ya katiba.

3. Kushindwa kufanya lobbying kwenye vyuo vikuu kwenye kufanya mihadhara na makongamano kwa sababu vina nafasi ya kufanya hivyo itakuwa karata nzuri kwa mfano Kigoda cha Mwalimu ingefanyika Lobbying kuhakikisha main theme ya kongamano lile iwe Katiba au uchaguzi na maendeleo. Au Nyerere day makongamano yatawaliwe na theme ya chaguzi zetu na mtazamo wa Nyerere juu ya chaguzi na demokrasia.

4. Main stream media zimeufyata sana lakini vingetakiwa kufanyika lobbying ya kuuma na kupuliza ingeleta tija kidogo.

Bado hawjachelewa they can do it.
 
BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,992
2,000
Nakubaliana nawe lakini yote haya KAMWE hayatafanikiwa bila ya kuwepo Katiba mpya na Tume huru ya uchaguzi.
Kuna eneo ambalo vyama vya upinzani vimefeli kwa kampeni zake za mabadiliko makubwa ya electoral laws.
1. Hawana taarifa za uchaguzi za madhira yote kuwa documented na kusambaza kwa wananchi ikiwemo vyombo vya habari na Tume ya uchaguzi yenyewe...
 
Muuza viatu

JF-Expert Member
May 14, 2020
3,288
2,000
Nakubaliana nawe lakini yote haya KAMWE hayatafanikiwa bila ya kuwepo Katiba mpya na Tume huru ya uchaguzi.
Nadhan jamaa alimaanisha kufanya lobbying maeneo hayo aliyoyagusia km kushawish mada ktk kigoda cha mwalimu au mihadhara ya ktk mavyuo labda ingeweza leta yote mabadiliko ktk sheria za uchaguz hata hiyo katiba mpya
 
PTER

JF-Expert Member
Dec 28, 2014
17,521
2,000
Nakubaliana nawe lakini yote haya KAMWE hayatafanikiwa bila ya kuwepo Katiba mpya na Tume huru ya uchaguzi.
Niliyoyasema mimi ni yale yatakayotuwezesha kupanua hii kampeni ya katiba mpya badala ya sasa ambako inachukuliwa kama a political agenda ya chama cha siasa tu.

Lazima lobbying ifanyike kwenye taasisi mbalimbali za umma ikiwemo viongozi wa dini Baraza la viongozi wa dini chini ya Askofu Paul Ruzoka linaweza a good starting point ya kumshawishi rais aanzishe mazungumzo na vyama vya siasa.

Tusitake kuwa kwenye misigano ya kisiasa tutashinda tupate kila kitu no let's go to the table with least expectation lakini tujue ipi itakuwa last position yetu.

Hii hatua ya kufanya siasa kwa kuwindana na mabomu ya machozi inazalisha extremism at the same time haina afya kabisa hasa kwa taifa.

Hebu tuanze kutafuta lobbyists wazuri mambo yataanza kwenda.
 
Kati ya niliyotaja hapo lipi linahitaji katiba mpya ?
 
BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,992
2,000
Mwamakula Kiongozi wa dini katiwa ndani, Sheikh Ponda alitiwa ndani pamoja ná Watanzania kulishinikiza Baraza la Kikatoliki nchini liikemee hii Serikali haramu na maovu yake dhidi ya Chadema na Watanzania bado Baraza hilo limekaa pembeni. Sasa Watanzania wanaanza kujadili kususia kwenda makanisani ili kuwaonyesha hawa Viongozi wa dini hawaridhishwi na ukimya wao.
Kwa Watanzania wanaojitambua wanajua fika kwamba katiba mpya si ya Chadema bali ni ya Watanzania wote bali wenye ufinyu wa akili ndiyo wanadhani hivyo.

Ninachokiona hapa hawa wanaopigia chapuo katiba mpya kipind hiki lengo lao haswa si katiba isipokua wana malengo mengineyo ila hili LA katiba wanalitumia km nyenzo ya kufanikisha hayo wanayoyataka na ndio maana mipango yao sio thabit wala endelevu.
 
wababayangu

JF-Expert Member
Jul 17, 2021
580
1,000
CHAMA cha ACT-Wazalendo kimesema hakitashiriki uchaguzi mdogo wa Jimbo la Konde hadi watumishi wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), waliohusika katika uchaguzi uliopita watakapowajibishwa.

kabwe.jpg

Akisoma maazimio ya chama katika eneo la Konde Pemba wakati wa ziara maalum ya viongozi wa ACT-Wazalendo, Kiongozi Mkuu wa chama hicho, Zitto Kabwe alisema chama hicho hakitashiriki uchaguzi huo hadi watumishi wa ZEC wawajibishwe.

Zitto alisema kuwa wananchi ambao waliumizwa na kuteswa kwenye uchaguzi walipwe fidia, ili wapate haki yao.

Alisema azimio lingine ni pamoja wa kuundwa kwa kamati ya kisheria ya kuratibu maridhiano ya kijamiii, ili ZEC ionyeshe mwelekeo nini kifanyike yazidi kukua.

Aidha, azimio la tatu ni kuitaka Serikali ya Zanzibar na ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuzifanyia marekebisho sheria zote za uchaguzi kabla ya mwaka 2025, ili uchaguzi mkuu ujao uwe sawa katika kushindania nafasi za uongozi.

Alisema halitakuwa jambo la busara kila baada ya uchaguzi kuirudisha Zanzibar nyuma kimaendeleo, ni vyema umoja na maridhiano ya kisiasa kudumu muda wote.

Mjumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho ambaye ni Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar, Othman Masoud Othman, alisema kilichomfanya mbunge mteule wa Konde kutoka CCM kuachia ngazi ni mazungumzo.

Alisema vilelezo na ushahidi waliowasilisha ni matunda na matokeo chanya yaliyopatikana ya kujiuzulu kwa mbuge mteule wa jimbo hilo.

Makamu Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo, Juma Duni Haji, alisema hawako tayari kuingia kwenye uchaguzi wakati walioharibu uchaguzi huo hawajachukuliwa hatua zozote.

Chanzo: Nipashe

Zitoooooo
Tayari kakisaliti chama.
Kweli fweza mwana halam.
 
PTER

JF-Expert Member
Dec 28, 2014
17,521
2,000
Ninachokiona hapa hawa wanaopigia chapuo katiba mpya kipind hiki lengo lao haswa si katiba isipokua wana malengo mengineyo ila hili LA katiba wanalitumia km nyenzo ya kufanikisha hayo wanayoyataka na ndio maana mipango yao sio thabit wala endelevu.
Lengo lao ni lipi ?
 
PTER

JF-Expert Member
Dec 28, 2014
17,521
2,000
Mwamakula Kiongozi wa dini katiwa ndani, Sheikh Ponda alitiwa ndani pamoja ná Watanzania kulishinikiza Baraza la Kikatoliki nchini liikemee hii Serikali haramu na maovu yake dhidi ya Chadema na Watanzania bado Baraza hilo limekaa pembeni. Sasa Watanzania wanaanza kujadili kususia kwenda makanisani ili kuwaonyesha hawa Viongozi wa dini hawaridhishwi na ukimya wao.
Kwa Watanzania wanaojitambua wanajua fika kwamba katiba mpya si ya Chadema bali ni ya Watanzania wote bali wenye ufinyu wa akili ndiyo wanadhani hivyo.
Tusijiegemeze kwenye hoja "watanzania wanaojitambua" kwani tunajua ni wangapi wanaojitambua? na kwa kiasi gani kutambua kwao kutafanikisha agenda ya katiba mpya ?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom