ACT-Wazalendo yabariki CCM kumsulubu Zitto

Alexander The Great

JF-Expert Member
Aug 28, 2018
4,502
23,582
WAKATI Wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wakipanga kumsulibu Zitto Kabwe, Chama cha ACT Wazalendo kimebariki mkakati huo.
images-3.jpeg


"ACT-Wazalendo kimeshauri Wabunge wa CCM kujipanga kwa hoja kwa kuwa, hoja za Zitto, Kiongozi Mkuu wa chama hicho na Mbunge wa Kigoma Mjini ni zenye kutafitiwa".

Ado shaibu, Katibu wa Itikadi, Mawasiliano na Uenezi wa ACT Wazalendo ametoa taarifa ya msimamo wa chama hicho na kusambazwa na Zitto mwenyewe.

Taarifa hiyo inatokana na dhamira ya wabunge CCM kutaka kumkabili Zitto kwa madai ya kumsumbua Job Ndugai, Spika wa Bunge la Jamhuri pia upotoshaji.

Baada ya kukutana kwenye Kamati ya Wabunge wa CCM (Caucus) wamemwona mbunge huyo ni adui namba moja.

Ado na ACT-Wazalendo wanaungana na dhamira ya CCM dhidi ya Zitto ila kwa kupambana kwa hoja.

Amesema, walichopanga kukifanya wabunge wa CCM, bila kujali wanatumia hoja yenye uzito gani kujibu, ndiyo maana hasa ya siasa.

“Kutarajia mashambulizi ya hoja za kisiasa kujibiwa kwa vitisho na mabavu ya vyombo vya dola kama ambavyo imeanza kujengeka katika miaka ya hivi karibuni ni utamaduni wa ovyo.” Amesema na kuongeza;

“Kumtisha, kumdhuru au kumuweka korokoroni mtoa hoja badala ya kuikabili hoja yake si siasa.”
 
Naona kichwa cha habari na mada iliyopo ndani vinatofautiana. ACT-Wazalendo wameshauri hoja za mbunge wao zijibiwe kwa hoja na si kwa vitisho! Sasa wapi wamebariki Zitto asulubiwe!!
 
Naona kichwa cha habari na mada iliyopo ndani vinatofautiana. ACT-Wazalendo wameshauri hoja za mbunge wao zijibiwe kwa hoja na si kwa vitisho! Sasa wapi wamebariki Zitto asulubiwe!!
Naona MWANA LUMUMBA una LIKES 47, mpaka sasa katika profile yako. Endelea kuzitafuta kwa kasi.

Tunawasubiri na kina ISIS
 
Back
Top Bottom