ACT Wazalendo washinda Uchaguzi wa Marudio Mbeya

MAAJABU YA CV YA AGNESS MARWA.

Hii ndio CV ya mbunge Agness Marwa aliyesema kuwa anasikia uchungu sana bunge kuoneshwa Live. Akiwasilisha mchango wake bungeni alisema anasikia uchungu mno bunge kuoneshwa Live kiasi kwamba anatamani kulia. Hataki kabisa wananchi watizame bunge Live.

CV yake ina maajabu yafuatayo;

#AjabuNoMoja
Agness amesoma shule mbili za sekondari kwa wakati mmoja. Nyaibara Secondary na Kenton High school. Mwaka 2009 alifanya mtihani kama QT Nyaibara uliomuwezesha kufanya mtihani mwaka 2010 kama school candidate ambapo alifanikiwa kupata alama 32. Kipindi hichohicho kati ya 2008 hadi 2014 alikua Kenton high school ambapo alihitimu na kufanikiwa kupata alama za juu zaidi yani div.4 ya point 33.

#AjabuNoMbili
Agness amezaliwa mwaka 1977 lakini ameanza form one mwaka 2008 akiwa na miaka 31. Tena sio elimu ya watu wazima. Hasha.! Elimu ya kawaida ya kuvaa sketi na blauzi nyeupe na kuchapwa viboko. Kidumu chama cha mapinduzi.

#AjabuNoTatu
Agness akiwa form two mwaka 2009 alidahiliwa Chuo kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kampasi ya Mlimani ambapo alipata fursa ya kusomea taaluma ya Teknolojia ya habari na mawasiliano kabla ya kurudi tena shuleni Kenton kuendelea kidato cha pili.

#AjabuNoNne
Agness amesoma Elimu ya sekondari miaka 6 akishindwa kufaulu licha ya kutokua na mchujo. Mwaka 2009 akiwa kidato cha pili mtihani wa mchujo wa form two ulifutwa kwa hiyo wanafunzi wote waliendelea na kidato cha 3 hata "waliofanya vibaya". Lakini Agness alishindwa hata "kufanya vibaya" ili aendelee kidato cha 3. Hivyo akarudia form two miaka mitatu mfululizo kabla ya kuruhusiwa kuendelea na form three mwaka 2013 baada ya walimu kuona anapoteza muda.

#AjabuNoTano
Akiwa kidato cha pili mwaka 2010 alikua Mkurugenzi Mtendaji (Managing Director) wa Kampuni ya Aggy Classic Interteimnent, na alikua akipewa tender kubwa za kuandaa matamasha ya Mwenge na sherehe mbalimbali za CCM.

#AjabuNoSita
Akiwa form one mwaka 2008 alikuwa Mwenyekiti wa chama cha watumiaji wa mazao ya ziwa Victoria Musoma (Seafood Union). Kwahiyo alikua anaregulate mazao yote ya ziwani. Yani ili Professor wa pale Buhare aweze kula samaki ilikua lazima Agness (mwanafunzi wa form one by then) atoe idhini. Yeye ndiye alikua na ithibati ya mazao yote ya ziwani kupitia Musoma SeaFood Union.

#AjabuNoSaba
Akiwa Form 2 mwaka 2007 tayari alikua Mkufunzi aliyebobea (Experienced Facilitator) wa masuala ya ujasiriamali kupitia Shirika la Nyang'oto. Hii inaonesha huyu dada ni 'genius' maana watu wanasomea degree za Enterprenuership vyuo vikuu miaka mitatu au zaidi, lakini yeye amekua mkufunzi mbobevu akiwa form one. CCM ni ileile.. oooh ni ileile.!

#AjabuNoNane
Kwa miaka 14 kutoka mwaka 1994 hadi 2008 Agness alikua nje ya mfumo rasmi wa Elimu akikijenga chama chake. Hakika CCM ina mikakati hodari..

#AjabuNoTisa
Akiwa kidato cha tatu mwaka 2013 Agness alichaguliwa kwa kishindo kuwa mjumbe wa Mkutano Mkuu taifa wa umoja wa wanawake wa CCM (UWT) na kuwabwaga maelfu ya wanawake wenzie walioomba nafasi hizo.

#AjabuNoKumi
Pamoja na yoooote hayo Agness ni Mbunge ktk Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Chombo cha juu kabisa cha maamuzi katika nchi. Na anategemewa kutoa mawazo yake yalete maendeleo kwa wananchi. Duuh bado tuna safari ndefu sana. CCM Hoyeee.!!
Nahisi kizunguzungu ghafla!
 
Agnes Marwa ana Elimu sawa na Mbowe na Mnyika na amemzidi mbali Kubenea.Jikite kwenye mada.Jifunze kupokea habari tofauti.
Hongera mkuu Umenena kweli tupu. Manake kuna wengine humu huwa hawaelewi hata maana ya Unazi. Wao kila kitu kikiwa na utofauti japo kidogo tu na matarajio yao basi huwa ni balaa
 
Nitashangaa sana kama ACT-WAZALENDO watakuwa tayari kutumika kama toilet paper au condoms. Let them fight their own battle because they have been called names and sidelined a great deal. Their future is brighter. Haina tija kwao kushirikiana na watesi wao.
Hapo penye ku sideline a great deal ndio penyewe, hivi CCM waliwalambisha elfu ngapi ili mpunguze kura za upinzani!? It was a great deal, indeed!
 
Hapo penye ku sideline a great deal ndio penyewe, hivi CCM waliwalambisha elfu ngapi ili mpunguze kura za upinzani!? It was a great deal, indeed!
Nakusikitikia sana kuona wewe kila anaetofautiana na fikra zako kuwa amenunuliwa sio kila mtu ana price tag. Usione kuwa wewe unanunulika basi ukadhani kila mtu ni hivyo. Ningekuwa nanunulika leo ningekuwa zaidi ya Makonda
 
Nakusikitikia sana kuona wewe kila anaetofautiana na fikra zako kuwa amenunuliwa sio kila mtu ana price tag. Usione kuwa wewe unanunulika basi ukadhani kila mtu ni hivyo. Ningekuwa nanunulika leo ningekuwa zaidi ya Makonda
CCM hawana muda wa kununua wewe, Zitto does it on their behalf!
 
Kwa mujibu wa Kongozi mkuu wa ACT Zitto Kabwe.Chama cha ACT Wazalendo kimeshinda kwa kishindo katika uchaguzi wa Marudio Mtaa wa Sasa Mbeya.

Maoni yangu:
CCM na Chadema jipangeni ACT wanajenga himaya kisiasa.Chadema Uchaguzi ufuatao kwa mkoa wa Mbeya utakuwa mgumu sana kwenu Mbeya...na huenda mkapoteza Mbeya Mjini,Kyela msahau kabisa.Mgawanyiko Mbeya na dharau za Sugu zitawatafuna.
MIMI NI KATIBU MWENEZI ACT MBEYA MJINI NINACHOFURAHI NI KWAMBA NIMEWASHINDA CCM ....CHADEMA NYIE NDUGU ZETU NA MARAFIKI WETU NA WENGI WENU TUNAISHI VIZURI ADUI YANGU NI CCM.... HATA HIVYO HIVYO KUNA SIKU TUTAFANYA KAZI PAMOJA CHA MSINGI TUITOE CCM
 
nasikiliza bunge hapa,bwana msigwa kajitutumua kuuliza pesa za mcc kajibiwa kiustadi na mh.muhungo naona hata kuja kurudia tena kuuliza kuhusu pesa za mcc
 
Kuna kanuni ya NCHI iliyovunjwa hapo? Hayo mengine ni porojo zako tu! Vyama vya siasa viko kwa mujibu wa katiba, na kila mtanzania ana haki ya kujiunga na chama chochote kile cha siasa!
Wewe haki imeshikwa na Lowassa, alipo upo, akienda utaenda, huna tafauti na bendera jinsi unavyofuata upepo, au wale wanyama wanapofanya maajabu ya kuvuka ule mto kwa wingi....bila kujali hatari ya mamba.
 
Ben, do you want to tell us ACT-WAZALENDO na CHADEMA (UKAWA) sail in the same boat? Tafadhali.......!!!! Naamini ACT-WAZALENDO wameshinda on their own maana they had been called names for quite sometime now. Ni wapinzani in their own way.

Ni kweli, ACT ni wapinzani wa wapinzani. Very funny
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom