ACT Wazalendo wamlilia Fidel Castro

Jun 16, 2016
14
16
TAARIFA KWA UMMA.

Buriani Komredi Fidel Castro - Mshirika wa Tanzania katika Ukombozi wa Afrika

Chama cha ACT Wazalendo kimezipokea taarifa za kifo cha Komredi Fidel Castro, Mwanamapinduzi na aliyekuwa kiongozi (Waziri Mkuu na Rais) wa Cuba (1959-2008) na Kiongozi wa Chama cha Kikomunisti cha Cuba (1961-2011) kwa huzuni kubwa.

ACT Wazalendo tunatoa salamu zetu za rambirambi Kwa Rais wa Cuba, Komredi Raul Castro, Balozi wa Cuba nchini, familia ya Komredi Fidel Castro, Chama cha Kijamaa cha Cuba na Wananchi wa Cuba Kwa kuondokewa na Mwanamapinduzi huyu, ambaye ni mmoja wa miamba imara ya mapinduzi ya karne ya ishirini.

Maisha ya Komredi Fidel Castro hayakuwa yenye manufaa kwa nchi yake ya Cuba pekee bali kwa dunia nzima hasa nchi zinazoitwa za 'Dunia ya Tatu'. Mafanikio yake kwenye maeneo kadhaa ya uendeshaji wa nchi kupitia mapinduzi ya kijamaa ya Cuba yanaacha alama ya kudumu kwenye nyanja mbalimbali za maisha ya WaCuba na darasa maridhawa kwa nchi zinazoendelea, yakiweka msisitizo juu ya umuhimu wa Ujamaa kwa dunia.

Mathalani, licha ya utitiri wa vikwazo kutoka nchi za kimagharibi zikiongozwa na Marekani, Cuba imeweza, tangu miaka mingi iliyopita kufuta ujinga kwa asilimia 99 . Cuba pia ni moja ya nchi zenye mfumo bora wa afya na zinazozalisha madaktari Kwa wingi duniani. Msaada wa madaktari unaotolewa na Cuba kwa nchi za Amerika ya Kusini, Afrika na Asia unavuka kiwango kinachotolewa na nchi zote za G8 kwa pamoja!

Mengi yanaweza kusemwa juu ya hatua za kimaendeleo zilizopigwa na Cuba wakati wa Komredi Fidel Castro lakini ni dhahiri kuwa kwa kigezo cha ukuaji wa uchumi unaokwenda sambamba na maendeleo ya watu wengi badala ya uchumi unaokua kwa tarakimu huku ukinufaisha wachache, Cuba imepiga hatua kubwa.

Maisha ya Komredi Fidel Castro pia ni darasa maridhawa kwa vijana. Akiwa na umri mdogo wa miaka 27 Fidel Castro alianzisha 'vuguvugu la 26 Julai' (The 26 of July Movement) ambalo kwa kushirikiana na vijana wenzake (Makomredi Ernesto Che Guevara, Raul Castro, Camilo Cienfuegos na wengine wengi) liliweza kuuondosha utawala wa kidikteta wa Rais Batista mwaka 1959. Hili ni darasa muhimu kwa vijana wa Tanzania, Afrika na dunia kuwa mustakabali wa nchi zao na ulimwengu utajengwa kwa uthubutu na kujitoa kwao.

Komredi Fidel Castro ana mafungamano ya moja kwa moja ya kiutu na Afrika, akisaidia kwa kila nyanja katika harakati za ukombozi wa Afrika kutoka katika makucha ya Ukoloni na Ubeberu, harakati ambazo zilikuwa na makao makuu yake hapa nchini kwetu Tanzania.

Afrika itamkumbuka Komredi Fidel Castro kwa mchango mkubwa ambao Cuba imeutoa kufanikisha harakati za kudai uhuru kwenye nchi mbalimbali za bara hili, hasa Afrika ya Kusini, Namibia, Angola, Msumbiji na Kongo. Lakini Tanzania itamkumbuka zaidi kama mshirika wa muhimu wa harakati hizo za Ukombozi wa bara letu.

Cuba imepoteza Kiongozi wake
Afrika imepoteza Rafiki wa kweli
Tanzania imepoteza Mshirika katika Ukombozi wa Afrika
ACT Wazalendo tumepoteza Mjamaa mwenzetu

John Patrick Mbozu.
Katibu wa Kamati ya Nje, ACT Wazalendo
75f4595d5f9b2000b7bf1ec525e01d7b.jpg
 
Kalale salama komredi Castro.... Wazalendo tunaendelea kukuenzi.
 
Kuna fununu za mkono wa komredi fideli katika kifo cha komredi hugo chavez.
 
Back
Top Bottom