ACT Wazalendo waibwaga CCM Konde, Mohamed Said Issa ashindi kiti cha Ubunge

Kwa hiyo ikishinda CCM mnasema kura zimeibwa ila wakishinda upinzani basi mnasema uchaguzi ni wa haki

kwa hiyo ktk uchaguzi wa haki CCM haina haki ya kushinda???

Ebu tubadilike; yeyote anastahili kushinda
Hakuna kushinda hapo, ACT haijashinda, CCM wameamua YAISHE ili kulinda upuuzi unaoitwa serikali ya umoja wa kitaifa. Kama hakuna Tume huru ya uchaguzi hakuna ACT kushinda. CCM wamekubaliana wawaachie wenzao ACT ndiyo maana yule alijiuzuru
 
Uchaguzi wa Julai waliopiga Kura walikuwa 5020, ACT walipata 1373, CCM 1796. Leo CCM hata 800 hawajafikisha, nusu ya walizopata mwanzo. Tunaambiwa waliojiandikisha 6600 waliojitikeza kupiga Kura 3400.
Cost ya uhuni kwenye uchaguzi ziko kwenye gharama kwa mlipa kodi na tozo kuendesha chaguzi zenyewe, voter apathy kwa wananchi kupoteza imani na mfumo, vifungo, vipigo, pengine vifo vya wananchi vinavyoambatana na chaguzi Zanzibar. Sijui ushindi uko wapi ukitazama haya.
 
ACT wazalendo ndio chama kikuu cha upinzani!

Kiwe hata tawala, nini cha upinzani. Pitia nyuzi zote ndio utajua nguvu ya Cdm, haishiriki uchaguzi lakini ndio inatajwa zaidi. Na kukiwa na uchaguzi huru lazima kishinde kwa uhakika na sio kimagumashi.
 
Mabavicha mnaona sasa wenzenu wanashinda chini ya tume hii hii tena kwenye uchaguzi mdogo!
Unadhani hatuna uelewa wowote? Huo uchafu tunauelewa mwanzo mwisho, na hatuko tayari kushiriki chini ya tume hii. Na kwa bahati mbaya hatusikii hata wivu wala kutamani kushiriki huo ushenzi. Ukitaka kujua Cdm ina mvuto, fuatilia uchaguzi huko Ushetu jinsi ulivyokosa mvuto. Hao Wapemba huwa wanaishinda ccm toka enzi za Nyerere, hakuna jipya hapo.
 
Kwani ni lini CCM ilishinda Pemba,kule wakuu wanamsimamo sio wakawaida watu waliostand na polisi piga uwa au mmeshasau.CCM imeshaambiwa isahau kupata ushindi wa halali Pemba .
Nyie waTanganyika mnawadekeza sana polisi ndio maana wanawachezea masharub,polisi hahusiani kabisa na mambo makuu ya uchaguzi inakuwaje anakimbia na masanduku ya kura si anajitafutia kifo cha dharura..
 
Kwa hiyo ule wa kwanza ulikuwa ni uporaji au? Kura zote hizo? Yule aliyejiuzulu alishindaje?
Ndio maana mama yake mwenye hofu na Mungu hakutaka upuuzi huu.

Kwa mwislamu wa kweli Firdaus ndio kipaumbele chake.

Tunaposema yule shetani wa Chato yupo kuzimu na kamwe hawezi kumuona Mungu muwe mnatuelewa.

Yeye ndio Injinia wa upumbavu huu, wizi ww kura upo ila huyo mwendakuzimu alikuja kuuwa kabisa hata maana ya uchaguzi.

Mungu aendelee kumlaani huko aliko ikiwezekana afe mara ya pili.
 
Kwa taarifa yako Cdm haihitaji ushirikiano na chama chochote cha siasa kususia uchaguzi. Huko pemba ccm haijawahi kushinda uchaguzi. Cdm iko huku Bara zaidi ambako ndio kuna impact ya kweli ya tume ya uchaguzi. Tazama Cdm haijashiriki uchaguzi wowote na jinsi chaguzi hizi zinavyozidi kupoteza mvuto na kudharaulika.

Wananchi walio wengi wanajitambua, hata vyama vyote vishiriki kadiri cdm na kupewa viti vya ubunge, bado ukweli kuwa tume hii ya uchaguzi sio huru uko wazi. Na tunavyoendelea iwapo Cdm itaendelea kususia hadi madai yao yatimizwe, chaguzi zitakuwa na wapiga kura wachache hadi aibu. Unaona popote uchaguzi wa Ushetu unaongelewa? Hiyo ni impact ya Cdm kususia huo uhuni, na CCM wanalia sana baada ya kuachiwa goli wazi.
Nilishasema mara nyingi uko nyuma kwamba uhamuzi wa Chadema kususia uchaguzi mpaka pawe na tume huru. Utakuwa na impact kama vyama vyote vya upinzani vitakubali kususiha.

Nikawatahadhari, kuna vyama vitaendelea kushiriki chaguzi na vita shinda. Hii itadhoofisha madai ya kususia uchaguzi mpaka kuwe na tume huru!!
Tunasema yetu macho!!
 
Unadhani hatuna uelewa wowote? Huo uchafu tunauelewa mwanzo mwisho, na hatuko tayari kushiriki chini ya tume hii. Na kwa bahati mbaya hatusikii hata wivu wala kutamani kushiriki huo ushenzi. Ukitaka kujua Cdm ina mvuto, fuatilia uchaguzi huko Ushetu jinsi ulivyokosa mvuto. Hao Wapemba huwa wanaishinda ccm toka enzi za Nyerere, hakuna jipya hapo.
Wapemba walishasema wazi, kati ya kifo na ccm wanachaguwa kifo.

Hata hivyo tumpongeze yule mwanaccm aliyepewa ushindi wa dhulma akaukataa, hizo ndio njia sahihi za kumuogopa Mungu.

Ukifika peponi ukimkuta mtu kama huyo huwezi kushangaa, siyo yule kichaa wa Chato, kuzimu ndio makazi yake.
 
Wagombea wa Cdm wameshakimbia sana na hadi kupewa vyeo, lakini bado tuna akili zetu timamu. Yaani hata vyama vyote vya upinzani vishiriki na kupewa vyeo, ukweli kuwa tume hii ya uchaguzi sio huru, na CCM haistahili tena kukaa madarakani kwani haina ridhaa ya wananchi. Wangewapa TLP,NCCR, CUF nk kiti cha ubunge huko Ushetu ili hii dhana yako itimie, lakini tunasimama na ukweli na hatuyumbi kwenye hilo.
kuu,
Liangalie ili la kususia uchaguzi kwa upana zaidi.
Kama vyama vingine vya upinzani vitaendelea kushiriki uchaguzi na kishinda. Zaidi ya kudhoofisha madai ya Chadema ya kutaka tume huru kabla ya uchaguzi, unajua kitakachofuatia?

Kukusaidi, wagombea wa Chadema watakimbilia kwenye vyama vingine kama ACT, watapewa nafasi ya kugombea na watashinda!! The rest is history!
 
Ninmeangalia hii id ni ya mwezi uliopita,na inamwaga mashudu balaa.
mnadai nini Tena wakati hiyo time ambayo hamuitaki ndiyo inawapa ubunge au chagadema mpaka washinde wao ndiyo ionekane uvhaguzi ulikuwa huru?



Na nyie endeleeni kusikikiza akili matope za mbowe kususia wenzenu wanapeta chagadema siasa imewashinda
 
Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Konde, Abdallah Said Hamad amemtangaza Mgombea wa ACT-Wazalendo, Mohamed Said Issa kuwa mshindi wa Ubunge kwenye uchaguzi mdogo wa Jimbo hilo uliofanyika leo 09 Oktoba, 2021

View attachment 1969576

Mohamed Said Issa amepata kura 2,391 dhidi ya 794 za mgombea wa CCM, Mbarouk Amour Habib. Mgombea wa AAFP, Hamad Khamis Mbarouk amepata kura 55 na Salama Khamis wa CUF amepata kura 98
View attachment 1969577
Hii ni kitu inajulikana Pemba ndio ngao ya mrithi wa CUF ambayo baadae imerrithiwa na ACT.

Kwa hiyo huu sio ushindi wa kujitathmini hata kidogo.
 
Wapemba walishasema wazi, kati ya kifo na ccm wanachaguwa kifo.

Hata hivyo tumpongeze yule mwanaccm aliyepewa ushindi wa dhulma akaukataa, hizo ndio njia sahihi za kumuogopa Mungu.

Ukifika peponi ukimkuta mtu kama huyo huwezi kushangaa, siyo yule kichaa wa Chato, kuzimu ndio makazi yake.
Aliukataa?
 
CCM wajanja sana watatumia uchaguzi huu kama kigezo Tume ipo huru.

Zitto anatumika kama daraja la kuhalalisha dhulma siku za usoni.
Ingekuwa sehemu nyingine yoyote ile ningekubaliana na maelezo yako lakini sio Pemba!!
 
Kuweka kumbukumbu sawa hapa.

Jimbo la Konde lipo Pemba, mahali ambapo ndio ngome kuu ya chama cha ACT wazalendo (zamani CUF), toka kipindi cha mapinduzi mpaka kesho na keshokutwa, CCM haitaweza kushinda jimbo lolote Pemba, iwe mvua liwe jua. Na mara zote CCM ilipopewa ushindi kwenye jimbo lolote Pemba basi hakukuwa na uchaguzi bali kulikuwa na uchafuzi.

Huu uchaguzi mdogo ni marudio ya uchaguzi mwingine mdogo ambapo mara ya mwisho CCM walitangazwa washindi kihuni, na ACT wakachimba mkwara mzito wa kutaka kujitoa kwenye serikali ya umoja wa kitaifa hali iliyopelekea kwa mbunge mteule wa CCM kutangaza (kulazimishwa?) kujiuzuru na ndio huo uchaguzi kuitishwa upya jana.

HITIMISHO:
Huu ni mchezo wa kuchezea pesa za umma na kupotezea muda watu unaofanywa na CCM.
 
Back
Top Bottom