ACT Wazalendo: Uchukuaji fomu kwa wagombea wa uchaguzi wa serikali za mitaa umejaa hujuma

Influenza

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2018
Messages
926
Points
1,000

Influenza

JF-Expert Member
Joined Jul 1, 2018
926 1,000
Siku tatu kabla ya kumalizika kwa muda wa uchukuaji fomu katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, chama cha ACT-Wazalendo kimesema zoezi hilo limetawaliwa na hujuma.

Kimesema wanachama wake wanaokwenda kuchukua fomu wanakumbana na vikwazo mbalimbali vinavyokatisha tamaa ikiwa ni pamoja kunyimwa fomu, kukuta ofisi zimefungwa, kutishwa na kupewa fomu zisizo kamili.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Ijumaa Novemba Mosi, 2019 Mratibu wa Mawasiliano Uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa chama hicho, Mbarala Maharagande amesema hujuma hizo zinafanywa makusudi na baadhi ya watendaji wa serikali wanaohusika na usimamizi wa uchaguzi.

Amesema katika jimbo la Liwale, wagombea wa vyama vya upinzani kikiwemo chama hicho wameshindwa kuchukua fomu kutokana na wahusika kutokuwepo ofisini.

“Katika jimbo la Liwale lenye Kata 20 kwa kiasi kikubwa wagombea wa upinzani wamekosa fomu, baada ya kusukumana ndiyo jana zimetolewa katika kata tatu, hii ni hatari,” amesema.

Chama hicho kimemuomba Waziri wa TAMISEMI, Selemani Jafo kuchukua hatua kwa kuwakumbusha watendaji wake wanaofanya hujuma hizo alizodai kuwa zinaweza kuleta vurugu.

Jana CHADEMA kilimuandikia barua Jafo kumueleza kasoro mbalimbali zinazojitokeza katika uchukuaji fomu, ikiwa ni siku moja baada ya kuiandikia barua ofisi ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kikieleza kasoro tisa zinazojitokea katika uchukuaji fomu.
 

mbenge

JF-Expert Member
Joined
May 15, 2019
Messages
557
Points
1,000

mbenge

JF-Expert Member
Joined May 15, 2019
557 1,000
Katika mazingira yenye hujuma kama haya inahitajika kuwa na "Plan B" nayo si nyingine bali kutengeneza mgogoro wa kimkakati. Ni kumdili mtu "personally" tu na ndiyo itakuwa suluhisho la muda, "select few cases and then severely and fiercely deal with them accordingly" wachache wakionjeshwa maumivu ya uovu wao, "actions will speak more louder than mere words".
 

Forum statistics

Threads 1,381,426
Members 526,090
Posts 33,799,869
Top