ACT Wazalendo: Tumepokea kwa masikitiko makubwa kauli ya Rais Samia kuhusu katazo la mikutano ya kisiasa ya hadhara

Nyie ni vigeugeu hakuna wa kuwasikiliza
Ni kiongozi gani au chama gani cha siasa kisichokuwa kigeu geu? Chadema kupitia viongozi wake wa juu kabisa walituaminisha kuwa Lowasa ni fisadi papa kwa zaidi ya miaka 7 afu wakajaribu kutumia mwezi mmoja tu wa kupiga kampeni ya kubadilisha maneno yao wenyewe (kumeza matapishi yao) kwa kusema kuwa Lowasa sio na wala hakuwahi kuwa fisadi toka kuumbwa kwa ulimwengu, kwa bahati nzuri watanzania wa miaka hii sio nyumbu tena, tunajitambua vizur tukawapuuza kwa kuwanyima kura na mgombea wao akaangukia pua.. ACT Wazalendo walikataa kukubali matokeo ya uchaguzi kwa madai kuwa uchaguzi haukuwa huru na wa haki lk punde kidogo wakakubali na kuingizwa ndan ya serikali ya kitaifa ya Zanzibar.. Alichofanya Lipumba kabla na baada ya uchaguzi mkuu ni aibu kwa elimu yake.. hapo sijawataja kina Mrema, Cheyo, Mbatia nk. Swali langu ni kiongozi gani au chama gani cha upinzani ambacho sio kigeu geu?
 
Back
Top Bottom