ACT-Wazalendo: Tishio la kufutwa, hatutarudi nyuma

Kwa ulaji huu wa Ruzuku ACt itajifuta mapema kabla haijaanza
Mkuu huyu msajili anakuwa kama wale ambao Mh.Magufuli aliwakemea kwa kufanya mambo ya ajabu na kusingizia maagizo kutoka juu.

Kwa taswira tuliyo nayo nje ya Tanzania itakuwa mbaya zaidi msahili akikifuta ACT kwa sababu zinazo takiwa kutoa onyo tu.
 
Zamania miaka ya 1990s kulikuwa na msemo kwamba ukimuondoa Saadam Husein mmoja kwa hila, watatokea kina saadam husein 100. Ukimuua Osama Mmoja watatokea kina Osama 100. Wakati huo tuliona kama mzaha msaha tu. Baada ya kuwaondoa kina Osama na Saadamu na Kina Gadaf dunia imekuwa na shida kuliko pale hao watu walipokuwa hai.


Somo kwetu kumfitini Maalimu Seif na Lupumba kwa nia ya kuiua CUF kumeibua chama dhaifu kuwa chama Imara Kuliko CUF ya Lipumba. Ni kweli Wafitini wanahangaika na kuchanganyikiwa kwa maana kulikuwa na chama kimoja pinzani chenye nguvu, Na sasa kuna vyama Viwili vyenye nguvu kubwa Bara na Visiwani.


Ole Ole Ole kwa CCM kama ACT na Chadema wakakubaliana kushirikiana Uchanguzi 2020 kwa kuachiana majimbo, CCM wanaweza kupata taaabu sana.

Kwa maana nionavyo mimi ni kama CCM inaihujumu zanzibar, Wazanzibar "INASEMEKANA" Wamejiunga na kuwa kitu kimoja. Wazanzibar wamekuwa wamoja zaidi Maalimu alipohamia ACT.

Huenda Wazanzibar kwa mara ya kwanza wakawa na Rais Zanzibar mpya kutoka upinzani 2020.


Kwa nini?

Mbinyo walionao CCM kwa kupora kura za CUF 2015 wa wahisani na wafadhiri ni mkubwa sana na kusababisha kuyumba kwa uchumi na kuleta maisha magumu.

Wazanzibar wamekuwa wamoja zaidi kuliko 2015, kwa sababu ya kuibuka kwa mafuta na kudhurumiwa kwa Masuala na haki zao za kimuunga km, Michezo na misaada kiuchumi.

Kuporomoka kwa uchumi kwa makosa ya Serkali kuu ambayo yameadhili pia upande wa pili wa Muungano bila ya sababu za kimsingi.

Kuchoshwa kwa siasa za uhasama huko zanzibar.


NB: CCM msimchululie Poa Zitto Kabwe . Mtakuja kushangaaaaa!.

Maalimu Seif angehamia Chadema isipokuwa ni suala la Udini.
 
Zitto anayechambua ripoti ya CAG yenye makumi kwa makumi ya kurasa na kuandikia maelezo, kuichambua karatasi yenye maelezo ya kiumbe anayefahamika kama Msajili wa Vyama vya Siasa si ilikuwa ni kama kumtaka amwandikie barua demu anayempenda?! Yaani unatiririka tu!!!


😂😂😂😂nimeipenda hii aisee
 
Zamania miaka ya 1990s kulikuwa na msemo kwamba ukimuondoa Saadam Husein mmoja kwa hila, watatokea kina saadam husein 100. Ukimuua Osama Mmoja watatokea kina Osama 100. Wakati huo tuliona kama mzaha msaha tu. Baada ya kuwaondoa kina Osama na Saadamu na Kina Gadaf dunia imekuwa na shida kuliko pale hao watu walipokuwa hai.


Somo kwetu kumfitini Maalimu Seif na Lupumba kwa nia ya kuiua CUF kumeibua chama dhaifu kuwa chama Imara Kuliko CUF ya Lipumba. Ni kweli Wafitini wanahangaika na kuchanganyikiwa kwa maana kulikuwa na chama kimoja pinzani chenye nguvu, Na sasa kuna vyama Viwili vyenye nguvu kubwa Bara na Visiwani.


Ole Ole Ole kwa CCM kama ACT na Chadema wakakubaliana kushirikiana Uchanguzi 2020 kwa kuachiana majimbo, CCM wanaweza kupata taaabu sana.

Kwa maana nionavyo mimi ni kama CCM inaihujumu zanzibar, Wazanzibar "INASEMEKANA" Wamejiunga na kuwa kitu kimoja. Wazanzibar wamekuwa wamoja zaidi Maalimu alipohamia ACT.

Huenda Wazanzibar kwa mara ya kwanza wakawa na Rais Zanzibar mpya kutoka upinzani 2020.


Kwa nini?

Mbinyo walionao CCM kwa kupora kura za CUF 2015 wa wahisani na wafadhiri ni mkubwa sana na kusababisha kuyumba kwa uchumi na kuleta maisha magumu.

Wazanzibar wamekuwa wamoja zaidi kuliko 2015, kwa sababu ya kuibuka kwa mafuta na kudhurumiwa kwa Masuala na haki zao za kimuunga km, Michezo na misaada kiuchumi.

Kuporomoka kwa uchumi kwa makosa ya Serkali kuu ambayo yameadhili pia upande wa pili wa Muunga bila ya sabbau za kimsingi.

Kuchoshwa kwa siasa za uhasama huko zanzibar.


NB: CCM msimchululie Poa Zitto Kabwe . Mtakuja kushangaaaaa!.

Maalimu Seif angehamia Chadema isipokuwa ni suala la Udini.
Hapo mwisho ungefafanua ingekuwa poa sana( Maalim Seif angehamia Chadema isipokuwa suala la Udini).
 
Sawa mkuu,Mimi nilitegemea utetezi ujae vifungu vya sheria na kuonesha hayo madai sio ya kweli. Huo utetezi wa kupigania wanyonge mara viongoz wa serikali huwa wanasema bwana asifiwe mara tumsifu Yesu Kristo au asalam aleko ni utetezi wa kipuuz dhidi ya wafuas wake kusema takbir. Alichojaza huyo jamaa ni Appeal to emotions FALLACY.

We think too small, like the frog at the bottom of the well. He thinks the sky is only as big as the top of the well. If he surfaced, he would have an entirely different view.

Hapa ndio msomi kamaliza kujenga hoja!! Alaaniwe aliyeleta mwenge wa uhuru nchi hii.
 
Zitto Kabwe Ruyagwa ANAJIBU MASUALA YA MSINGI KAMA ANAMJIBU NAIBU WAKE HAJI DUNI.

Suala la Udini, ukiacha Takbir kutumika ACT imekuwa ni Chama kinachoamini katika uislam na kuwapa nafasi waislam kuliko dini yoyote ile.

Acha kina Maganja na Dorothy waliokaa kama mapazia. 2015 wagombea udiwani wasiokuwa waislam ndani ya ACT mfano wa Wiston Andrew Mogha walifanyiwa figisu hadi wakafikia kuichukia siasa.

Suala la Kuchoma Bendera, Zitto Kabwe anajibu kama vile watanzania ni washamba wasioelewa. Haihitaji kujua namba ya kadi za wachoma bendera kujua kama ni watu wa ACT au la.

Kwenye ukaguzi siwezi kugusa sana ingawa wenyewe kwa wenyewe hutupiana madongo kwa kusema Mwambuja alikikwamisha chama kuwasilisha hesabu sababu ya ufisadi uliofanyika kipindi chake.

Msajili akikiacha hichi chama tutarajie na wa upande mwingine wakija na chama kina Bendera ya msalaba na slogan ya Yesu anaweza.

Picha inasanifu yaliyoandikwa
IMG-20190326-WA0032.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tunazifahamu Hila na Njama Dhidi ya ACT Wazalendo, Haturudi Nyuma!

(Taarifa ya Kiongozi wa Chama Ndugu Kabwe Z. Ruyagwa Zitto Kuhusu Tishio la Msajili wa Vyama vya Siasa Kukifutia Usajili Chama cha ACT Wazalendo)

1. Utangulizi

Jana tarehe 25 Machi 2019, tulipokea barua kutoka Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa yenye kumbukumbu Na. HA. 322/362/20/98 ambayo; pamoja na mambo mengine, ilieleza juu ya kusudio la serikali kutaka kukifuta Chama cha ACT Wazalendo.

Barua hiyo ilieleza kuhusu mambo matatu yaliyosababisha Ofisi ya Msajili itangaze kusudio hilo ovu juu yetu. Kwanza ilizungumza kuhusu hoja zinazohusiana na ukaguzi wa hesabu za chama uliofanywa na Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), pili kuhusu vitendo vya kuchomwa hadharani kwa bendera na kadi za chama cha CUF na tatu matumizi ya neno takbira kama yalivyoonekana katika baadhi ya video zilizosambaa katika mitandao ya kijamii.

Naomba niwaeleze kwa kina kuhusu hoja moja baada ya nyingine kabla ya kutoa maoni yetu na mwelekeo wa chama baada ya kupata barua hii.

1. Kuhusu Ukaguzi wa CAG

Barua ya Msajili wa Vyama vya Siasa inadai kwamba ACT imekiuka Sheria ya Vyama vya Siasa kwa kutopeleka kwake hesabu zilizokaguliwa kwa mwaka wa fedha 2013/2014 kama sheria inavyotaka.

Tuhuma hizi hazina ukweli wowote. ACT Wazalendo ilianzishwa na kupewa Usajili wa Kudumu tarehe 5 Mei, 2014 na kwa hivyo, kwa mwaka huo wa fedha (2013/14) Chama chetu kilikuwa na miezi miwili tu ya kukaguliwa. Kazi yetu ACT Wazalendo kama chama cha siasa ni kuwasilisha ripoti kwa ajili ya kukaguliwa na CAG. Ripoti ya hesabu za 2013/14 imewasilishwa kwa CAG kwa barua.

Kwa kutumia Kanuni za Kimataifa za Kihasibu na kwa ushauri wa CAG, chama chetu kilielezwa kinaweza kuunganisha hesabu za mwaka 2013/2014 na 2014/2015 katika ripoti moja, wakieleza kuwa hilo jambo la kawaida kabisa katika kanuni za uhasibu kwani inaruhusiwa kuunganisha hadi miezi 18. Kwa kuunganisha huku hesabu, ACT ilikuwa na miezi 14 tu.

Kabla ya kuchukua uamuzi wa kukubali ushauri huu wa kuunganisha hesabu kutoka Ofisi ya CAG, Chama chetu kilimwandikia Msajili wa Vyama vya Siasa (Kwa barua mbili zenye kumbukumbu namba AC/HQ/MSJ/2015/006 na AC/HQ/MSJ/2015/008 za tarehe za tarehe 22 na 29 Januari 2015) naye akajibu na kuridhia hesabu za miezi miwili ya mwaka 2013/2014 kuunganishwa kwenye mwaka wa fedha 2014/2015 (kwa barua yenye kumbukumbu Na. KA/ 322/20/60 ya tarehe 16 Februari 2015).

Taarifa zote hizi ziko wazi kwa kwake mwenyewe Msajili na kwenye Ofisi ya CAG, kuanzia barua za kutaarifiwa Juu ya kukusanywa kwa pamoja kwa taarifa ya Ukaguzi wa Mahesabu ya ACT Wazalendo kwa miezi 14 ya mwanzoni (miezi miwili ya mwaka 2013/14 na miezi 12 ya mwaka 2014/15), mpaka ripoti husika ya Ukaguzi kutoka kwa CAG. Tumeshangaa sana anaposema ana nia ya kutufuta kwa kutokupeleka ripoti ambayo tayari anayo Ofisini kwake.

ACT Wazalendo tunajua kuwa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa haina utaalam wa Masuala ya Ukaguzi wa Fedha na Matumizi ya Vyama. Hivyo tunajua kuwa upo uwezekano kuwa wameshindwa kuisoma, kuichambua na kuielewa ripoti hiyo ya Ukaguzi wa Hesabu za ACT Wazalendo kwa mwaka wa Fedha wa 2014/15, hatuwalaumu kwa jambo hilo. Ndio maana kisheria kazi hiyo ya ukaguzi amepewa CAG.

Lakini Msajili wa Vyama vya Siasa nchini angekuwa na nia njema, angeweza tu kuomba ufafanuzi au uchambuzi wa taarifa husika kutoka kwa CAG au hata kwetu ACT Wazalendo, Chama chenye uzoefu wa kuchambua hizo ripoti za CAG, na angepewa taarifa husika. Taharuki hii aliyoisababisha haikuwa na sababu yeyote, ni suala la uelewa tu.

Tunawaahidi wanachama wa ACT Wazalendo kuwa sisi Viongozi wao tutajibu barua hii ya msajili kwa kumuelewesha. Zaidi tunaishauri Ofisi ya Msajili kuwa ni vyema basi wakishindwa kuzielewa taarifa tunazowapelekea warudi kwanza kwa CAG ama kwetu kuomba ufafanuzi na uchambuzi kabla ya kuandika hizi barua za kutishia kutufuta.

2. Kuhusu Kuchoma bendera na kadi

Barua yenyewe ya Msajili iliyotufikia inasema kwamba imeona picha zinazoonyesha “wanaodaiwa” kuwa wanachama wa ACT Wazalendo wakichoma bendera na kadi za chama cha CUF. Katika hili, Msajili mwenyewe anaonyesha kwamba hana uhakika kama kweli wahusika ni wanachama wa ACT.

Si ilibidi Msajili ajiridhishe kwanza kuwa wale ni Wanachama wa ACT Wazalendo? Kama hajaridhisha anawezaje kutangaza NIA ya kutaka kufuta Usajili wa Chama chetu kwa jambo hilo? Watanzania waone Ofisi ya Msajili ilivyo na NIA Mbaya na Chama chetu, Watanzania waone namna Ofisi ya Msajili, inayoongozwa na Jaji inavyotoa tuhuma pamoja na kutoa hukumu bila hata ya kuwa na Ushahidi.

Chama chetu HAKIHUSIKI kabisa na uchomaji wa bendera wala kadi za Chama chochote. Kihistoria sisi ni Chama cha Masuala, tunaojikita juu ya Utetezi wa Wakulima wa Korosho, Mahindi, Giligilani, Karafuu, Mkonge na Mbaazi wanaokosa masoko ya bidhaa zao. Sisi tumezoeleka kuwa ni wapaza Sauti za Wafuagaji wanaotaifishiwa Mifugo yao na Wavuvi wanaonyang’anywa nyavu zao.

ACT Wazalendo tunatambulika kwa Uchambuzi wa Bajeti na kupinga Sera za mbaya za kuongoza Uchumi zinazowafanya wananchi waishi maisha magumu. Matumaini ya wananchi kwetu ni kwa sababu wamezoea kutuona tukichambua ripoti za CAG na kuhoji kutokuonekana kwa TZS 1.5 Trilioni na kusimamia uwajibikaji wa Serikali. Chama chetu utambulisho wake ni utetezi wa wanyonge wanaoonewa popote pale duniani, iwe ni Sahara Magharibi, Palestine au MKIRU (Mkuranga, Kibiti na Rufiji). Rekodi zetu zinatutambulisha hivyo.

Tumesikitika sana Ofisi ya Msajili hata kuwaza tu kuwa Chama cha Masuala cha namna hiyo kinaweza kuhusika na mambo ya Uchomaji wa bendera na kadi za vyama vingine. Tumesikitika sana.

3. Kuhusu "Takbir"

Barua hiyo ya Msajili inaeleza pia kwamba chama chetu kimevunja sheria ya vyama vya siasa kwa sababu “wanaodaiwa kuwa wanachama wetu” wametumia maneno takbira kwenye shughuli za kichama na kwamba maneno hayo yana udini. Majibu ya hili ni kama kwenye suala la kudaiwa kuchoma kadi na bendera. Msajili hajaainisha hao wanaodaiwa kuwa ni wanachama wetu wana kadi namba ngapi za uanachama na ni kutoka tawi gani la chama chetu.

ACT Wazalendo ni chama cha siasa cha watu wa matabaka na dini zote na hata wale wasio na dini. Katika Katiba yetu ya chama tumeonyesha wazi kwamba hatufungamani na dini yoyote na ndiyo sababu tumeruhusiwa kufanya shughuli za kisiasa.

Tuna ushauri tu kwa Ofisi ya Msajili, katika nchi ambayo Viongozi karibu wote wa Serikali wanaanza hotuba zao kwa salamu za kidini za “Bwana Yesu Asifiwe, Tumsifu Yesu Kristo na Assalaam Aleykum” ni rahisi kwa “wanaodaiwa kuwa wanachama wa ACT Wazalendo” kutumia kaulimbiu za Dini zao kama wanavyofanya Viongozi wa Serikali.


4. Mtazamo Wetu

Barua ya Msajili haina nia njema kwa ACT Wazalendo na wapenda demokrasia wote hapa nchini. Kukosekana kwa nia njema kulionekana mapema kabisa baada ya barua iliyotakiwa kutumwa kwetu kusambazwa kwanza katika mitandao ya kijamii kabla hata haijatufikia ofisini. Taswira tunayopata ni kwamba ilivujishwa makusudi na ofisi ya msajili kutimiza dhamira ovu waliyonayo dhidi yetu.

Serikali na Chama cha CCM vimepata mchecheto na ufuasi mkubwa wa chama chetu, hasa baada ya Maalim Seif Sharif Hamad na waliokuwa Viongozi wenzake kutoka chama cha CUF kuhamia ACT Wazalendo. Wameogopa zaidi kuwa sasa ACT Wazalendo ndio kimbilio la Wazanzibari wote waliomchagua Maalim Seif kuwa Rais wao kwenye uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, 2015.

Ushauri tu kwa CCM na Serikali yake, hata wasiwaze tu kuifuta ACT Wazalendo, hatua mbaya ya namna hiyo ya kionevu itawanyima fursa karibu theluthi moja ya Watanzania ya kufanya siasa kwa njia halali za kisheria. Watu hawa wakinyimwa fursa hii kionevu kupitia ACT Wazalendo watatumia njia nyengine zinazoweza hata kuleta mpasuko kwa Taifa letu. Ikifika hatua hiyo, sisi Viongozi wa ACT Wazalendo hatutakuwa na sauti ya kuwakataza watu hawa watakaodhulumiwa fursa ya kufanya siasa kwa njia halali za kisheria.

Tunachukua nafasi hii pia kuzitaka Taasisi za Dini, Asasi za Kiraia, Nchi marafiki na wahisani kupaza sauti juu ya jambo hili. Wasikae kimya wanapoona uonevu unataka kufanyika.

5. HATURUDI NYUMA

Kwa wanachama wa ACT Wazalendo, wafuasi na watanzania kwa ujumla, barua hii ya Msajili haijatutisha wala kututikisa. Na tutaazima busara za mwanachama wetu mwandamizi, Maalim Seif, kuwa TUSICHOKOZEKE. Na hatutachokozeka.!

Tamko langu hili kwenu liwe ni ishara kwenu kuwa Chama kiko salama na imara, na kwamba barua hii ya Msajili itajibiwa kwa hoja, na ushahidi wa hoja kabla ya hizo siku 14 alizozitoa. Ulinzi wa chama hichi ni wajibu wenu, sisi Viongozi wenu tuko hapa kutoa dira na mwongozo.

Endeleeni kugawa kadi na shughuli nyengine za uenezi wa Chama chetu, ziara zetu sisi Viongozi kuja kukagua shughuli zenu ziko kama ilivyo ratiba yetu. Huko mliko mtembee kwa fahari mkijua kuwa wapinzani wetu sasa wanatuogopa, hawataki tena kusubiri uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020, wanataka kutufuta kwa hila. Tunajua hawataweza.

Mungu yupamoja nasi.

Nawashukuru sana.

Kabwe Z. Ruyagwa Zitto
Kiongozi wa Chama
ACT Wazalendo
Machi 26, 2019
Dar es salaam

Sent using Jamii Forums mobile app



Msisahau kumtumia hii
 
Back
Top Bottom