ACT-Wazalendo ngome ya vijana - Taarifa kwa vyombo vya habari

Dotto C. Rangimoto

JF-Expert Member
Nov 22, 2012
1,985
1,284
ACT NGOME YA VIJANA DAR ES SALAAM.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI.

Serikali ya awamu ya tano imeanza kutekeleza mpango wa elimu bure kuanzia darasa la kwanza mpaka kidato cha nne.

Katika kutekeleza mpango huo hutolewa ruzuku ya Tsh 25,000 kwa kila mwanafunzi wa sekondari na Tsh 10,000 kwa kila mwanafunzi wa shule ya msingi kwa mwaka

Fedha hizi za ruzuku ni sawa na wastani wa shilling 68 kwa mwanafunzi mmoja wa sekondari kwa siku na shilling 27 kwa mwanafunzi wa shule ya msingi kwa siku.

Sisi Ngome ya vijana ya ACT-Wazalendo Mkoa wa Dar-Es-salaam tumestushwa na kiasi hiki ambacho ni kidogo kisichoweza kukidhi mahitaji muhimu ya upatikanaji wa elimu bora nchini

Kwa maana hiyo basi kama serikali imedhamiria kutekeleza mpango wa elimu bure nchini kupitia utoaji wa ruzuku mashuleni tunaitaka iangalie upya kiasi hicho kama kinalingana na upatikanaji wa elimu iliyo bora na ifanye mambo yafuatayo

1.Serikali iongeze kiasi hiki cha ruzuku ili kiweze kukidhi dhana ya elimu bure na mahitaji ya mashule yetu kufikia kiwango cha shilling 40,000 kwa kila mwanafunzi wa sekondari kwa mwaka ambapo ni sawa na wastani wa shilingi 109 kwa siku, na shilingi 25,000 kwa mwanafunzi wa shule ya msingi kwa mwaka ambapo ni sawa na wastani wa shilingi 68 kwa siku.

2. Tunaitaka serikali iwekee uzio Fedha hizi ili zisijekutumika kwa ajili ya matumizi mengine yoyote ya serikali nje ya upatikanaji wa elimu katika eneo husika.

3. Fedha hizi zitumwe moja kwa moja kwenye akaunti za kila shule na halmashauri zihakikishe kuwa hakuna akaunti hewa

4. Pia tunaiomba serikali itoe mchanganuo wa matumizi ya Fedha hizi ili kuondoa mgogoro kati ya uongozi ya shule na wazazi.

Ngome ya vijana ACT-Wazalendo Mkoa wa Dar Es salaam tunaziomba kamati za shule na wazazi kufuatilia kwa karibu fedha hizi za ruzuku na matumizi yake kwenye shule zetu.

Kuhusu Bomoa Bomoa inayoendelea

Ngome ya vijana ya ACT-Wazalendo Mkoa wa Dar Es salaam inaitaka serikali kuzingatia UTU wakati wa utekelezaji wa sheria kwenye suala la bomoabomoa.

Kwa kuwa serikali ndiyo yenye jukumu la kuhakikisha watu wake wanakuwa katika mazingira salama tunaitaka iwasaidie wahanga wa bomoa bomoa hiyo hasa kipindi hiki cha mvua zinazoendelea kunyesha jijini Dar Es salaam kwa kuwapatia maeneo ya kujisitiri kwa wakati huu huku mpango endelevu wa kuhakikisha madhara kama hayo hayajirudii ukiwa unafanyiwa kazi.

Tunaitaka serikali katika kutekeleza sharia yake hiyo ya kuwaondoa waliojenga mabondeni ihakikishe inawawajibisha na wale wote waliozembea katika majukumu yao na kuwafanya wananchi kujenga katika maeneo yasiyo ruhusiwa

Mwisho Ngome ya vijana ACT-wazalendo Mkoa wa Dar Es Salaam inawapa pole watanzania wote walioathirika na uharibifu wowote uliojitokeza kipindi hiki cha mvua zilizonyesha na zinazoendelea kunyesha nchini,Kwa kuharibikiwa Mali zao kama nyumba na mashamba na miundombinu ya kwenye maeneo Yao.

Karama Kaila

Mwenyekiti WA Ngome ya Vijana Mkoa WA Dar-Es-Salaam.

Imetolewa ,leo januari 24/2016
 
Kiasi cha ruzuku ni kidogo sana. Elimu bure chini ya ccm ni mkakati maalum wa kuongeza idadi ya manyumbu.
 
Vizuri lakini mbona hamjengi chama?.

Au mmesharizika na mafanikio yenu mliyopata ya kumpeleka Zitto bungeni,hiyo ngome ya vijana mbona haifahamiki viongozi wao ni kina nani?.

Hata kama hamna rasilimali watu au fedha,chama chenu bado kidogo inabidi muingie vyuoni na sehemu mbalimbali kutafuta vijana ambao ni bright,ili baadae waje kuongoza chama.

Mwambieni pia Mwigamba nafasi aliyo nayo hana uwezo nayo,bora angeachia vijana wenye maono ya mbali zaidi.

Tambueni kujenga chama field sio sawa na kwenye makaratasi,Inabidi muwe na mpango kabambe wakuwajenga vijana hasa kisera na sio kishabiki.

Pia mwambie huyo Karama Kaila hio nafasi nae pia inampwaya,yampasa apunguze ushabiki na kujielimisha zaidi ili awe na ufahamu wa mambo mengi.Sio kukalia ushabiki muda wote.

Mwambieni pia Kiongozi wenu wa chama,ajenge chama kama taasisi na sio chama kiwekeze kwake.Pia atambue ndani ya ACT hatoweza fikia ndoto zake alizokuwa akiota,cha msingi ndoto zake zinaweza kukamilishwa na vijana atakao wajenga lakini sio lazima awe yeye.

Pia salamu ya chama chenu haivutii kabisa na wala haina uhamisgmhaji na haivuti antetion ya mtu pindi aisikiapo,mnaweza kubadili kama kikatiba inaruhusiwa.

Pia pongezi nyingi zimuendee Mama ana kwa kukitangaza chama kadri alivyyoweza,lakini nae inampasa agroom vijana wa kikr watakao kuja kuchukua nafasi yake.

KALINZI NYUMBANI.
 
Kalinzi Nyumbani,

Umetoa mchango mzuri saaana. Ila kuna moja umelisahau au pengine ni wewe. Mwalimu Kaijage ni jipu na janga kubwa saaana.
 
Kuhusu hili la elimu, mmekurupuka. Mngewauliza walimu. Mnayoshauri ndiyo yaliyofanywa kasoro kiwango. Pengine mnafikiri hizo pesa kwa mwanafunzi ni boom kama la chuo
 
Kalinzi Nyumbani,

Umetoa mchango mzuri saaana. Ila kuna moja umelisahau au pengine ni wewe. Mwalimu Kaijage ni jipu na janga kubwa saaana.
Mimi siwezi hata siku moja kuwa Mwal Kaijage ambae ushabiki wa vyama umemjaa.

Mimi ingawa namkubali Zitto lakini nimeamua kutofungamana tena na chama chochote ili niwe huru.Unapokuwa unaushabiki wa chama kuna baadhi ya mambo utayafumbia macho kisa ni ukweli ambao ni mchungu.

Lakini pia hivi Mwal Kaijage ana cheo gani ndani ya chama?,mimi siku zote namuona kama minor substance so siwezi kaa nikaandika juu yake.

KALINZI NYUMBANI.
 
Habib Mchange,Karama kaila,Mwl Kaijage,Janet Rite na baadhi ya masalia wengine wa usaliti ndiyo wanakiua chama kwa kuendekeza mipasho,matusi na majungu dhidi ya vyama vingine vya upinzani.
 
Zitto hawa watoto wanakutia aibu.
Hv hiyo hesabu wameipataje?
Wanaju siku za masomo ni ngapi kwa mwaka au wanagawanya tu kwa 365?
Hiyo hela ya ruzuku hapewi mwanafunzi hadi ionekane ndogo na kiwango hicho ndio kilichopitishwa, pesa ya ruzuku inatumika kiujumla kwa mgawanyo wa asilimia kugharamikia ujenzi, mitihani na vingine.
Hali halisi ni kwamba hiyo hela ilikua haifiki shule kwa miaka iliyopita japo ni ndogo lakini shule zilikua zinapata chini ya nusu ya hiyo.
Tunahitaji kuboresha lakini kwa kuanzia kilichofanyika sio cha kubeza.
 
ACT mliingizwa chaka na mheshimiwa mbunge na msha jichimbia kaburi. Hamuaminiki popote tz isipokuwa kigoma. Mlipigania maslahi ya zzk.

fighting without knowing your enemy is more than insaner
 
Siku zijazo msishauri jambo Kama lilivyofanyika, fanyeni utafiti lilivyofanyika kisha mje na mawazo mbadala. Mfano kwenye elimu akaunti zipo na miongozo fedha zitumikaje ipo tayari.
bomoabomoa pia waziri January alitolea ufafanuzi naninyi mnarudi aliyosema! Fatilieni mambo msiwe waziiito vijana
 
Vizuri lakini mbona hamjengi chama?.

Au mmesharizika na mafanikio yenu mliyopata ya kumpeleka Zitto bungeni,hiyo ngome ya vijana mbona haifahamiki viongozi wao ni kina nani?.

Hata kama hamna rasilimali watu au fedha,chama chenu bado kidogo inabidi muingie vyuoni na sehemu mbalimbali kutafuta vijana ambao ni bright,ili baadae waje kuongoza chama.

Mwambieni pia Mwigamba nafasi aliyo nayo hana uwezo nayo,bora angeachia vijana wenye maono ya mbali zaidi.

Tambueni kujenga chama field sio sawa na kwenye makaratasi,Inabidi muwe na mpango kabambe wakuwajenga vijana hasa kisera na sio kishabiki.

Pia mwambie huyo Karama Kaila hio nafasi nae pia inampwaya,yampasa apunguze ushabiki na kujielimisha zaidi ili awe na ufahamu wa mambo mengi.Sio kukalia ushabiki muda wote.

Mwambieni pia Kiongozi wenu wa chama,ajenge chama kama taasisi na sio chama kiwekeze kwake.Pia atambue ndani ya ACT hatoweza fikia ndoto zake alizokuwa akiota,cha msingi ndoto zake zinaweza kukamilishwa na vijana atakao wajenga lakini sio lazima awe yeye.

Pia salamu ya chama chenu haivutii kabisa na wala haina uhamisgmhaji na haivuti antetion ya mtu pindi aisikiapo,mnaweza kubadili kama kikatiba inaruhusiwa.

Pia pongezi nyingi zimuendee Mama ana kwa kukitangaza chama kadri alivyyoweza,lakini nae inampasa agroom vijana wa kikr watakao kuja kuchukua nafasi yake.

KALINZI NYUMBANI.

Nini kimekupata ndugu yangu,Wewe ni shabiki mkubwa wa Zitto na ulijipambanua kama mtetezi wa ACT hapa jukwaani,umechoka kutumika?

Anyway,haya ndiyo madhara ya kutarajia Chama kikutumikie,badala ya Wewe kukitumikia chama ,mambo yakienda kinyume na matarajio yako unaasi Chama.

Lakini kwako Wewe na watu wa aina yako mliyoipokea ACT kwa kigezo cha UKIGOMA,mnapoamua kuasi Chama,maamuzi yenu yanafika mbali zaidi kwani mnakuwa mmejiasi na kujisaliti wenyewe.Hayo ndiyo madhara ya kujenga Chama kwa kumzunguka mtu mmoja.Ndiyo maana wenye akili timamu tulipinga katiba inayomfanya mtu awe "nuru na taswira ya Chama.

Wanadamu wanabadilika,kumfanya mtu awe taswira na nuru ya Chama,wakati naye ni mwanadamu mwenye matamanio na mapungufu,ni jambo lisilokubalika.Aliyepewa " utukufu" na kuitwa nuru na taswira ya Chama,anaposhindwa kuishi kwa kadili ya maelekezo na misingi ya Chama,anachafua taswira ya Chama na kuizima nuru ya Chama,Chama kinapoteza uoni na mwonekano wake.

Leo hii nchi nzima Chama kimelala,kinasubiri runu itokayo kwa "kiongozi mkuu(umwami)"ili iweze kuangaza na watu waone Taswira yake.Jitahidini muweze angalau kubaki katika masikio yetu,vinginevyo mtasahaulika mapema mno.
 
ACT NGOME YA VIJANA DAR ES SALAAM.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI.

Serikali ya awamu ya tano imeanza kutekeleza mpango wa elimu bure kuanzia darasa la kwanza mpaka kidato cha nne.

Katika kutekeleza mpango huo hutolewa ruzuku ya Tsh 25,000 kwa kila mwanafunzi wa sekondari na Tsh 10,000 kwa kila mwanafunzi wa shule ya msingi kwa mwaka

Fedha hizi za ruzuku ni sawa na wastani wa shilling 68 kwa mwanafunzi mmoja wa sekondari kwa siku na shilling 27 kwa mwanafunzi wa shule ya msingi kwa siku.

Sisi Ngome ya vijana ya ACT-Wazalendo Mkoa wa Dar-Es-salaam tumestushwa na kiasi hiki ambacho ni kidogo kisichoweza kukidhi mahitaji muhimu ya upatikanaji wa elimu bora nchini

Kwa maana hiyo basi kama serikali imedhamiria kutekeleza mpango wa elimu bure nchini kupitia utoaji wa ruzuku mashuleni tunaitaka iangalie upya kiasi hicho kama kinalingana na upatikanaji wa elimu iliyo bora na ifanye mambo yafuatayo

1.Serikali iongeze kiasi hiki cha ruzuku ili kiweze kukidhi dhana ya elimu bure na mahitaji ya mashule yetu kufikia kiwango cha shilling 40,000 kwa kila mwanafunzi wa sekondari kwa mwaka ambapo ni sawa na wastani wa shilingi 109 kwa siku, na shilingi 25,000 kwa mwanafunzi wa shule ya msingi kwa mwaka ambapo ni sawa na wastani wa shilingi 68 kwa siku.

2. Tunaitaka serikali iwekee uzio Fedha hizi ili zisijekutumika kwa ajili ya matumizi mengine yoyote ya serikali nje ya upatikanaji wa elimu katika eneo husika.

3. Fedha hizi zitumwe moja kwa moja kwenye akaunti za kila shule na halmashauri zihakikishe kuwa hakuna akaunti hewa

4. Pia tunaiomba serikali itoe mchanganuo wa matumizi ya Fedha hizi ili kuondoa mgogoro kati ya uongozi ya shule na wazazi.

Ngome ya vijana ACT-Wazalendo Mkoa wa Dar Es salaam tunaziomba kamati za shule na wazazi kufuatilia kwa karibu fedha hizi za ruzuku na matumizi yake kwenye shule zetu.

Kuhusu Bomoa Bomoa inayoendelea

Ngome ya vijana ya ACT-Wazalendo Mkoa wa Dar Es salaam inaitaka serikali kuzingatia UTU wakati wa utekelezaji wa sheria kwenye suala la bomoabomoa.

Kwa kuwa serikali ndiyo yenye jukumu la kuhakikisha watu wake wanakuwa katika mazingira salama tunaitaka iwasaidie wahanga wa bomoa bomoa hiyo hasa kipindi hiki cha mvua zinazoendelea kunyesha jijini Dar Es salaam kwa kuwapatia maeneo ya kujisitiri kwa wakati huu huku mpango endelevu wa kuhakikisha madhara kama hayo hayajirudii ukiwa unafanyiwa kazi.

Tunaitaka serikali katika kutekeleza sharia yake hiyo ya kuwaondoa waliojenga mabondeni ihakikishe inawawajibisha na wale wote waliozembea katika majukumu yao na kuwafanya wananchi kujenga katika maeneo yasiyo ruhusiwa

Mwisho Ngome ya vijana ACT-wazalendo Mkoa wa Dar Es Salaam inawapa pole watanzania wote walioathirika na uharibifu wowote uliojitokeza kipindi hiki cha mvua zilizonyesha na zinazoendelea kunyesha nchini,Kwa kuharibikiwa Mali zao kama nyumba na mashamba na miundombinu ya kwenye maeneo Yao.

Karama Kaila

Mwenyekiti WA Ngome ya Vijana Mkoa WA Dar-Es-Salaam.

Imetolewa ,leo januari 24/2016
Hivi act ina madiwani wangapi tanzania mzima?
 
Mimi siwezi hata siku moja kuwa Mwal Kaijage ambae ushabiki wa vyama umemjaa.

Mimi ingawa namkubali Zitto lakini nimeamua kutofungamana tena na chama chochote ili niwe huru.Unapokuwa unaushabiki wa chama kuna baadhi ya mambo utayafumbia macho kisa ni ukweli ambao ni mchungu.

Lakini pia hivi Mwal Kaijage ana cheo gani ndani ya chama?,mimi siku zote namuona kama minor substance so siwezi kaa nikaandika juu yake.

KALINZI NYUMBANI.
Kweli wewe nyumbani ni kalinzi?
 
ACT na CCM si ndio wale wale? Kwanini msikae vikao vya ndani mkamalizana huko huko na "maelimu" yenu ya bure?
 
Back
Top Bottom