King klax
JF-Expert Member
- Jul 10, 2015
- 4,242
- 2,677
Asante sanaIdadi ya wabunge sio uthibitisho wa kukubalika kwa chama ( Marekani kuna majimbo mengi tu ambako Democrats wanapata kura nyingi kuliko Republicans lakini wanapata viti vichache kuliko wenzao).
Hata katika uchaguzi uliopita ulioacha maswali mengi Chadema kilipata kura nyingi kuliko vyama vingine vyote vya upinzani. Wangekubaliana na matokeo ya uchaguzi Chadema ingekuwa na wabunge 20 bungeni. Aidha, ukiangalia nguvu ambazo chama tawala kinatumia kupambana na Chadema ni dhahiri kuwa wanakiona kuwa ni tishio kwao. Ni Chadema peke yake ambao hata uvaaji wa fulana zao unaweza kukusababisha ukae mahabusu. Ni hiki ndicho kinachofanya wengi tukione kuwa ni chama kikuu cha upinzani.
Ushirikiano wa vyama hauwezi kulazimishwa hasa kwa sababu kila chama kina sera zake. Na ushirikiano wa kulazimisha hapo mbeleni unaleta changamoto za kugawana viti na kama watashinda, madaraka.
Kama kweli watanzania watakuwa wameichoka CCM wataamua wenyewe nani awe mrithi wake. Anaweza kuwa Chadema, ACT-WAZALENDO, NCCR-MAGEUZI CUF, hata TLP.
Hizi sifa za kipi ni chama kikuu au chama kiongozi hakitabadilisha msimamo wao.
Mimi nawashangaa wale wanaosema kuwa hamna serious opposition wakati kila kukicha tunaona juhudi zinavyofanywa kuwakosesha pumzi. Kama hamna serious opposition pangekuwa hamna haja ya kuzuia mikutano ya hadhara, makongamano, maandamano, watu kuombewa, uvaaji wa t-shirt, ubebaji wa mabango n.k. Tusingeona utitiri wa watu kuswekwa mahabusu na kufunguliwa kesi ambazo hazina mbele wala nyuma. Tusingeona mitandao inabanwa maana chama tawala wangejua hamna chama ambacho kinaweza kuchukua nafasi yao kwa kuzingatia jinsi kinavyokubalika.
Hauwezi kuwafunga watu mikono na kuwaziba macho yao halafu ukatamba kuwa hauoni wa kukushinda kwenye mbio za steeple chase!
Amandla...