Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 46,986
- 144,313
Siku chache zilizopita, niliongelea swala la kuwataka CHADEMA kujiepusha na matumizi ya neno "chama kikuu" cha upinzani nchini kwasababu mbalimbali mojawapo ni katika kuimarisha upinzani nchini na kuondoa inferiority complex miongoni mwa vyama vingine vya upinzani.
Katika dhana hiyo hiyo ya kutafuta ukubwa/ ukuu miongoni mwa vyama vya upinzani nchini, leo hii ACT-Wazalendo wameamua kujiita "chama kiongozi wa upinzani nchini". Hii inadhihirisha kile nilichokisema kuwa maneno haya ya "ukuu" yanaathiri umoja na mshikamano miongoni mwa vyama vya upinzani.
Teyari baadhi ya makamanda wameanza kuhoji uhalali wa ACT kujiita ni chama kiongozi wa upinzani nchini jambo ambalo si jema sana.
Najua si vyama vyote vinavyoitwa vyama vya upinzani ni kweli vyama hivyo ni vya upinzani, bali baaidhi ni vyama mapandikizi kwa lengo la kuvuruga upinzani ila bado ukweli huu hauondoi athari ya vyama vingine kuwa na ukuu dhidi ya vyama vingine.
Wasomeni hapa ACT katika taarifa yao hii ndio mjue huu ukuu sio jambo jema miongoni mwa vyama vya upinzani.