ACT Wazalendo na CCM wavutana

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,492
54,890
Kutokana na mambo mbalimbali ambayo yanaendelea nchini ikiwepo mikataba mibovu ya madini viongozi mbalimbali wa vyama vya siasa wamekuwa wakisema njia pekee ya kuweza kusaidia nchi kulinda maliasili zake ni kuwa na Katiba mpya.
Wenezi.jpg

Jambo hili limewaibua Wenezi wawili wa vyama vya siasa akiwepo Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Humphrey Polepole kutoka Chama Cha Mapinduzi na Katibu mwenezi wa ACT Wazalendo Taifa, Bwana Ado Shaibu ambao walinyuka kwa hoja juu ya Katiba mpya huku Humphery Pole Pole yeye akisema kuwa waliofanya katiba ikwame ni viongozi wa upinzani pamoja na viongozi wa CCM ambao waliweka maslahi binafsi mbele kuliko maslahi ya wananchi.

Humphery Pole pole alidai kuwa wao kama Chama Cha Mapinduzi saizi wanajisafisha ili wawe wasafi ndiyo baadaye waje kuzungumzia suala la Katiba Mpya wakiwa ni wasafi na kusema anaamini pia vyama vya upinzani ndiyo vitachelewesha tena kwani wao mikono yao ni michafu lakini haoni dalili za wapinzani hao kujisafisha.

"Katiba hatukufanikiwa kwa sababu wengi wa sisi viongozi tena kutoka upinzani na Chama Cha Mapinduzi tuliweka maslahi yetu mbele tukaweka mbali maslahi ya wananchi kwa sababu za ubinafsi lakini serikali ya CCM saizi tunarekebisha hayo. Mimi nilitegemea na vyama vingine vikianza kuosha mikono yao michafu mno halafu ndiyo tuzungumze katiba, ukizungumza katiba na una mikono michafu haina tofauti na chakula kipo mezani una mikono michafu na bado unataka kula haiwezekani" alisema Pole Pole

Kwa upande wa pili Katibu mwenezi wa ACT Wazalendo Taifa, Bwana Ado Shaibu alipingana na hoja ya Pole pole na kusema kuwa analeta hoja nyepesi kwenye jambo la msingi na kusema kuwa katiba ya nchi ni mali ya wananchi na si mali ya chama fulani cha siasa, hivyo kusema CCM saizi inajisafisha ikimaliza kujisafisha ndiyo izungumzie katiba si sawa.

"Ndugo Pole Pole anasema mchakato wa katiba ni sharti tusubiri CCM inawe mikono, kanuni ya wapi hii? Taratibu za wapi hizi za kidunia za kutengeneza katiba zinazosema tunasubiri chama tawala kijisafishe, kinawe mikono kiwe safi ndipo turejee mchakato wetu, taratibu za wapi hizo zinazosema mpaka vyama vya siasa vinawe mikono ndipo virejee mchakato wa katiba. Katiba ni mali ya wananchi na wanasiasa wakizungumza wanazungumza kama sehemu katika jamii, wanasiasa watasema lakini haiondoi ukweli kwamba katiba ni zao la wananchi, kwa hiyo kusema mpaka CCM iwe safi ni kurejea katika propaganda" alisema Ado Shaibu

Mbali na hilo Ado Shaibu alimtaka Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi kutoka CCM ndugu, Humphery Pole Pole kuwa wazi kwamba kwa CCM ya sasa katiba siyo kipaumbele chao hivyo wananchi wajue kuliko kufanya propaganda ili hali anatambua wazi kuwa hata Rais John Pombe Magufuli katiba si ajenda yake kwa sasa.

"Rais Magufuli yeye alishaweka wazi kuwa katiba siyo ajenda yake, sasa kuna dhambi gani wapishi wa propaganda wa CCM kusema kwamba hatutaki katiba siyo vipaumbele vyetu, wanyooshe tu maelezo na si kupindisha pindisha ili watu wajue namna ya kupigania katiba yao" alisisitiza Ado Shaibu

Humphery Pole Pole alikuwa mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba iliyoongozwa na Jaji Joseph Warioba ambayo iliwasilisha kwenye Bunge rasmi la Katiba.
 
Wanajua fika kwamba katiba mpya ikiwa bora hakuna wa kupona ndani ya ccm
 
Hivi ni lazima binadamu uanvyozidi kuzama kwenye CCM ndiyo unavyozidi kuwa mpumbavue na mnafiki?

Huyu pole pole aseme ni mpinzani nani alikwamisha upatikanaji wa katiba mpya kwa ajli ly aubinafis?

Ameamua kura nguruwe, achague aliyenona. Hawezi tena kuzungumzia sulala la katiba mpya ikiwa hatakuwa na ujasiri wa kusema kweli kwamba KATIBA MPYA ILIKWAMISHWA NA CCM!... BILA KUMUNG'UNYA.

Ati CCM wanajifasisha ndipo katiba ianze!. Upumbavue!!!!. Kwani katiba ni ya ccm? Bila ccm Tanzani ahaipo? WAkati wanajisafisha Taifa lisimame bila kufanya maendeleo wakisubiri ccm kwanza itengemae?? Upumbavue mkubwa. Hata siwezi kusoma yote kwa ajili ya upumbavue wa haka ka bwana mdogo!

Kutokana na mambo mbalimbali ambayo yanaendelea nchini ikiwepo mikataba mibovu ya madini viongozi mbalimbali wa vyama vya siasa wamekuwa wakisema njia pekee ya kuweza kusaidia nchi kulinda maliasili zake ni kuwa na Katiba mpya.
Wenezi.jpg

Jambo hili limewaibua Wenezi wawili wa vyama vya siasa akiwepo Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Humphrey Polepole kutoka Chama Cha Mapinduzi na Katibu mwenezi wa ACT Wazalendo Taifa, Bwana Ado Shaibu ambao walinyuka kwa hoja juu ya Katiba mpya huku Humphery Pole Pole yeye akisema kuwa waliofanya katiba ikwame ni viongozi wa upinzani pamoja na viongozi wa CCM ambao waliweka maslahi binafsi mbele kuliko maslahi ya wananchi.

Humphery Pole pole alidai kuwa wao kama Chama Cha Mapinduzi saizi wanajisafisha ili wawe wasafi ndiyo baadaye waje kuzungumzia suala la Katiba Mpya wakiwa ni wasafi na kusema anaamini pia vyama vya upinzani ndiyo vitachelewesha tena kwani wao mikono yao ni michafu lakini haoni dalili za wapinzani hao kujisafisha.

"Katiba hatukufanikiwa kwa sababu wengi wa sisi viongozi tena kutoka upinzani na Chama Cha Mapinduzi tuliweka maslahi yetu mbele tukaweka mbali maslahi ya wananchi kwa sababu za ubinafsi lakini serikali ya CCM saizi tunarekebisha hayo. Mimi nilitegemea na vyama vingine vikianza kuosha mikono yao michafu mno halafu ndiyo tuzungumze katiba, ukizungumza katiba na una mikono michafu haina tofauti na chakula kipo mezani una mikono michafu na bado unataka kula haiwezekani" alisema Pole Pole

Kwa upande wa pili Katibu mwenezi wa ACT Wazalendo Taifa, Bwana Ado Shaibu alipingana na hoja ya Pole pole na kusema kuwa analeta hoja nyepesi kwenye jambo la msingi na kusema kuwa katiba ya nchi ni mali ya wananchi na si mali ya chama fulani cha siasa, hivyo kusema CCM saizi inajisafisha ikimaliza kujisafisha ndiyo izungumzie katiba si sawa.

"Ndugo Pole Pole anasema mchakato wa katiba ni sharti tusubiri CCM inawe mikono, kanuni ya wapi hii? Taratibu za wapi hizi za kidunia za kutengeneza katiba zinazosema tunasubiri chama tawala kijisafishe, kinawe mikono kiwe safi ndipo turejee mchakato wetu, taratibu za wapi hizo zinazosema mpaka vyama vya siasa vinawe mikono ndipo virejee mchakato wa katiba. Katiba ni mali ya wananchi na wanasiasa wakizungumza wanazungumza kama sehemu katika jamii, wanasiasa watasema lakini haiondoi ukweli kwamba katiba ni zao la wananchi, kwa hiyo kusema mpaka CCM iwe safi ni kurejea katika propaganda" alisema Ado Shaibu

Mbali na hilo Ado Shaibu alimtaka Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi kutoka CCM ndugu, Humphery Pole Pole kuwa wazi kwamba kwa CCM ya sasa katiba siyo kipaumbele chao hivyo wananchi wajue kuliko kufanya propaganda ili hali anatambua wazi kuwa hata Rais John Pombe Magufuli katiba si ajenda yake kwa sasa.

"Rais Magufuli yeye alishaweka wazi kuwa katiba siyo ajenda yake, sasa kuna dhambi gani wapishi wa propaganda wa CCM kusema kwamba hatutaki katiba siyo vipaumbele vyetu, wanyooshe tu maelezo na si kupindisha pindisha ili watu wajue namna ya kupigania katiba yao" alisisitiza Ado Shaibu

Humphery Pole Pole alikuwa mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba iliyoongozwa na Jaji Joseph Warioba ambayo iliwasilisha kwenye Bunge rasmi la Katiba.
 
Mimi nimeipenda hii confession ya huyo kijana kwamba wao ni wachafu ndo maana hatukupata katiba ya wananchi. Kwa maana hata yule alokuwa mwenyekiti na makamu wake kwenye lile bunge pia walikuwa wachafu ndo maana wakahesabu hata kura za marehemu lkn bado Mr God akasema no way. This also tells us kwamba mikataba ile mibovu ni matokeo ya uchafu wao. Sasa swali wananawa kwa sabuni ipi ili watakasike? This is good news congrats Mr slowslow
 
Kwanini usimshauri mzalendo aanzishe mchakato wa katiba mpya ili iwe fimbo kwa wahujumu uchumi wote?
 
Hoja ya Polepole inaspin kututoa kwenye hoja ya msingi.Bila katiba bora juhudi zao siyo endelevu!
 
Back
Top Bottom