Uchaguzi 2020 ACT Wazalendo mnafanya Kosa walilofanya CHADEMA mwaka 2015. Mgombea anaeuzika kwa sasa ni Tundu Lissu

Sir John Roberts

JF-Expert Member
Mar 1, 2017
9,565
15,920
Nimesikitishwa sana na kitendo cha ACT kumteua Benard Membe kuwania urais JMT.
Huu naweza kuuita ubinafsi japo bado sijafahamu kama kutakua na makubaliano ya kumsimamisha mgombea mmoja kwa vyama vyote vya upinzani kwaniaba.

Ni kweli Membe ni mgombea potential kwa ACT wazalendo (japo mie siungi mkono hoja hii). Hili ni kosa ambalo lilifanywa na chadema mwaka 2015 ambao walimteua Edward lowassa lakini akaja kuwageuka mbeleni baada ya kuukosa urais. We learn through experience. Kama ACT wazalendo hamkujifunza hili kwa chadema basi ni either wabinafsi ama mna shinikizo kutoka upande wa pili.

Ushauri wangu.kwa sasa Tanzania nzima na dunia inajua Tundu Tundu lisu ndio kiongozi pekee wa upinzani ambae anaweza kupambana na ccm na akaiishinda.hili hata magufuli analijua ( refers hotuba zake za hivi karibuni).

Tafadhali Zitto angalieni namna ya kumsimamisha mgombea mmoja kwa urais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania nae awe ni Tundu Lissu. Nawahakikishia mtafanikiwa lakini mkiuvunja umoja wenu hamtafanikiwa.

Kila la kheri!
 
Hakuna ujanja ujanja Safari hii kila mmoja ashinde mechi zake. Kila Chama kina haki ya kusimamisha wagombea sio CDM pekee yake. Huyo TL unaesema atashinda sijui atashindaje ambapo hataweza hata kupata wabunge 20?.
Acha ujinga subirini uchaguzi msianze kupanga matokeo, janja janja hamna safari hii lazima kieleweke.

Sent from my Nokia 5.1 Plus using JamiiForums mobile app
 
Sasa kama Lissu ndiye aneyeuzika, Je kama Lissu akashinda urais, ACT nayo itakuwa chama tawala au itaendelea kuwa chama cha upinzani?

Lissu atatekeleza Ilani ya ACT au ya CHADEMA?

Na je ACT ikimuunga mkono Lissu, wamekubalianaje kwenye suala la kuachiana majimbo ya wabunge?
Nafikiri bado mchakato unaendelea
 
Hakuna ujanja ujanja Safari hii kila mmoja ashinde mechi zake. Kila Chama kina haki ya kusimamisha wagombea sio CDM pekee yake. Huyo TL unaesema atashinda sijui atashindaje ambapo hataweza hata kupata wabunge 20?.
Nawashangaa sana hawa mijamaa hao 20 ni wengi sana wakipata 5 washukuru mungu

Sent from my SM-A015F using JamiiForums mobile app
 
Vyama sio lazima viungane ili kushinda, kuna vyama havina mchango wowote, hao nccr hawana wanacholeta mezani, wao wanakubalika wapi ili waachiwe jimbo?!
Kuna vyama vinajimwambafy tu havina athari wala mchango.

Hao ACT zaidi ya Zanzibar huku bara waachiwe nini au wapi?!
Kila mmoja akapambane.

Mbona ccm haitafuti washirika?! Hata cuf na nccr walivitumia kuua UKAWA sasa hawawataki unaona wanavyotapa tapa.
 
Sasa kama Lissu ndiye aneyeuzika, Je kama Lissu akashinda urais, ACT nayo itakuwa chama tawala au itaendelea kuwa chama cha upinzani?

Lissu atatekeleza Ilani ya ACT au ya CHADEMA?

Na je ACT ikimuunga mkono Lissu, wamekubalianaje kwenye suala la kuachiana majimbo ya wabunge?
Bila kusahau Ruzuku, 2015 UKAWA ilowapa Ruzuku CDM lakini sijui Kama waligawana na akina Mbatia na Kina Makaudi. Wasisahau pia kuwa Zitto ana Political ambutions zake na akicheza karata zake vizuri anaweza kwenda kuwa kiongozi wa Kambi upinzani na hatimae kuwa Main Opposition Part hali itakayomfanya 2025 awe Potential Candidate wa Opposition. Lakini pia CDM msisahau kuwa mlishawahi kufanya an attempt kumumaliza kisiasa Zitto na bado hiyo kumbukumbu anazo
 
Hivi nyie viumbe mnaamini mtashinda mbele ya hii tume na katiba iliyopo??

Daaah Huo muda wa kupiga kura bora nipige ulabu tuu huku na ruka debe la rege za luck Dube
Duh.. watu Kama ww ndo mnashindisha Hawa wakoloni weusi
 
Kila mtu apambane na maamuzi ya chama chake, bila shaka mtoa mada umeona mtakwenda kugawana kura pamoja na ACT wazalendo ndio maana umekuja hapa kujitetea, hata nyie chadema mnachofanya ndio yaleyale ya 2015 na mwaka huu hakuna kura mtakayo ambulia.

Kila mtu afe na anachokiamini.

2020 twende na John Magufuli
 
Back
Top Bottom