ACT-Wazalendo Mkoani Lindi wazuiwa kumuombea Dua aliyekuwa Mwenyekiti wao Maalim Seif kisa Maombolezo ya Hayati Magufuli

Livejr

JF-Expert Member
Feb 6, 2014
2,068
2,792
Chama cha ACT-Wazalendo mkoani Lindi kimesitisha shughuli ya Maombi ya kumuombea alieykuwa mwenyekiti wao ambaye alifariki Februari 17, 2021.

Hali imetokea baada ya kuomba kibali kwa Jeshi la Polisi mkoani Lindi na kunyimwa, huku sababu kuu iliyoelezwa ni tupo kwenye kipindi cha siku 21 cha maombolezo ya kitaifa.

Je, kipindi hiki ina maana hata kufanya dua tu inakatazwa?

OMBI: Rais wa JMT, Mh. Samia Suluhu Hassan ikikupendeza fumua jeshi la Polisi kuanzia kule Juu mpaka wakuu wa Polisi Mikoa na Wilaya, hawa wanakutengenezea na wataendelea kukutengenezea chuki kubwa sana dhidi ya Wananchi.

FB_IMG_1617341274414.jpg
 
Watumie busara wafanye baada ya siku 21 za maombelezo. La sivyo watauona mziki wa Mama Samia.
 
Polisi wanataka kumchonganisha Mama na raia tu,hicho kisomo ni ibada sasa kama Serikali inafikia hatua ya kuingilia Imani za watu wake hiyo ni hatari nyingine mpyaaaaah!!
Hii serikali sijui kwanini wanashindwa kujizuia kuingilia uhuru wa watu wa kuabudu
 
Polisi wanataka kumchonganisha Mama na raia tu,hicho kisomo ni ibada sasa kama Serikali inafikia hatua ya kuingilia Imani za watu wake hiyo ni hatari nyingine mpyaaaaah!!
uhuru waa kuabudu una mipaka, ndio maana watu wanataka chadema ijitenganishe na kanisa la kilutheli.
 
Watumie busara wafanye baada ya siku 21 za maombelezo. La sivyo watauona mziki wa Mama Samia.
Maombolezo ya nani? Kama ni huyo dikteta uchwara ameshakufa tayari! Na ukishakufa ndiyo basi tena. Haisaidii chochote.

Na hapa usimsingizie mama watu! Wanao zuia shughuli mbalimbali za kijamii kuendelea ni hao policcm wasio jielewa! Na siyo mtu mwingine.
 
Tii sheria bila shurti, la sivyo utapigwa uchakae.
Atanipiga nani! Unadhani kila mtu unaweza ukampiga tu kirahisi? Yaani tuache kufurahia maisha kwa sababu kuna mtu mmoja huko wapi sijui, kafa!! Ujinga kabisa. Mimi naendelea na maisha kama kawaida!

Sina cha kuomboleza.
 
Mtoa tarifa hizo abadirishe tu ule muda wa kwenda kuomba hicho kibali ili wapewe, Maana huwenda kipindi anakwenda kituoni, kamkuta mkuu wa police ndo katoka kunyang'anyana bunduki na lijambazi, matokeo yake ndio hayo!

Katoa maamuzi akidhani Bado yupo kwenye Hali ya kunyang'anyana bunduki na jambazi
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom