ACT WAZALENDO mbioni kufungua kesi Mahakama Kuu kupinga uteuzi wa Mahera kuwa Mkurugenzi wa NEC

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,618
218,040
Kauli hiyo ya Kizalendo imetolewa na Kiongozi wa ACT - WAZALENDO Mh Zitto Kabwe , ambapo chama hicho kimemuagiza Mwanasheria Jebra Kambore kuandaa makabrasha .

Chanzo : Mwananchi

Swali : Mbona Mh Magufuli kila akiteua mtu anapingwa sana na wananchi , tatizo liko wapi leo ambalo Mkapa na Kikwete hawakuwa nalo ?
 
ILI KULIPA NGUVU HILI SUALA,

YAITISHWE MAANDAMANO YA AMANI NCHI NZIMA KUPINGA HUO UTEUZI

NAOMBA JAJI MKUU, AYAPOKEE HAYO MAANDAMANO PALE VIWANJA VYA JANGWANI.

CHONDE CHONDE POLISI NAWAOMBA MUWALINDE WAANDAMANAJI HADI MWISHO WA MAPOKEZI YAO.
 
Kuna haja ya kutafuta namna bora ya kumpata Mkurugenzi mkuu wa NEC na wakurugenzi wengi na pia kuangalia upya sheria zinazosimamia uchaguzi na tume ya uchaguzi..

Kuna haja pia ya kuangalia upya namna ya kufanya teuzi za wakuu wa usalama na sheria zinazosimamia vyombo hivyo..

Kuna haja pia ya kuangalia upya namna bora ya uteuzi wa majaji wa mahakama kuu na mahakama nyinginezo na pia kuangalia upya sheria zinazosimamia utendaji wao..

Ni muhimu hayo yafanyike ili kuleta usawa kwenye jamii na sehemu ya kuonyesha demokrasia na ustaarabu uliokomaa. Sina uhakika kama vitu hivi vinaangaliwa kuendana na nyakati tulizopo..
 
kutoka haters hadi kuwa followers wa Zitto
Kuna kitu hukijui kuhusu mimi , ukikengeuka nakurarua bila huruma lakini ukirudi kwenye mstari nitakuunga mkono , hivi ndivyo tulivyomfanyia Dr Slaa , tulimuunga mkono lakini alipoamua kumkiri Shetani kuwa bwana na mwokozi wake tumemchanilia mbali na hatokaa atusahau .
 
Back
Top Bottom