ACT Wazalendo: Matamshi ya IGP Simon Sirro baada ya kikao chake na Msajili wa Vyama vya Siasa hayaonyeshi nia njema

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
1,117
2,000
TAARIFA KWA UMMA.

Tumepata taarifa kupitia vyombo vya habari kuwa kikao cha Jeshi la Polisi na Vyama vya Siasa kilichoitishwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa kimepangwa kufanyika tarehe 21 Oktoba 2021.

Baada ya tafakuri ya kina, ACT Wazalendo tumeamua kuwa HATUTASHIRIKI kikao hicho kwa sababu zifuatazo;-

1. Tarehe 21 hadi 22 Oktoba 2021, viongozi wakuu wa ACT Wazalendo watakuwa kwenye Mkutano Mkuu wa Kitaifa wa Haki, Amani na Maridhiano ulioitishwa na Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD). Mkutano huo unatarajiwa kuhudhuriwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ndugu Samia Suluhu Hassan.

2. Baada ya Msajili wa Vyama vya Siasa kutangaza kikao cha Polisi na Vyama vya Siasa, Chama Cha ACT Wazalendo kupitia Kiongozi wa Chama Ndugu Zitto Kabwe, kilimwandikia Msajili kuwa kikao hicho kimjumuishe Waziri wa Mambo ya Ndani ambaye ndiye mwenye dhamana ya kisiasa ya Jeshi la Polisi. Hadi sasa hatujapata mrejesho wa suala hilo na mwelekeo ni kuwa kikao hicho kitakuwa Cha Polisi na Vyama vya Siasa pekee.

3. Matamshi ya IGP Simon Sirro baada ya kikao chake na Msajili wa Vyama vya Siasa hayaonyeshi nia njema ya kikao hicho. Kauli yake kuwa nchini Tanzania hakuna shida kuhusu mikutano ya nje na kwamba tatizo lipo kwenye mikutano ya ndani na inabidi sheria iwekwe sawa ni dalili ya wazi kuwa kikao hicho kinaweza kutumika kubinya zaidi shughuli za kisiasa nchini.

Imetolewa na:

Salim A. Bimani,
Katibu wa Habari, Uenezi na Mahusiano na Umma,
ACT Wazalendo.
26 Septemba, 2021.
IMG-20210926-WA0003.jpg
 

mshale21

JF-Expert Member
Apr 8, 2021
1,064
2,000
Kuna CCM, na Kuna vijiCCM vidogo vidogo lazima washiriki, kwa hyo hata wasipohudhuria lazim kile kilichokusudiwa kifanyike!

Kuna kitu kinatafutwa hapo, na lazima kipite taka msitake, msema kweli' Ni MUDA!
 

Retired

JF-Expert Member
Jul 22, 2016
30,039
2,000
Kuna CCM, na Kuna vijiCCM vidogo vidogo lazima washiriki, kwa hyo hata wasipohudhuria lazim kile kilichokusudiwa kifanyike!

Kuna kitu kinatafutwa hapo, na lazima kipite taka msitake, msema kweli' Ni MUDA!
Siro na Mutungi hawezi kuwa na nia njema na yeyote, ni kususia mavi yao eti ni mkutano
 

Lord OSAGYEFO

JF-Expert Member
Feb 19, 2021
1,724
2,000
Kuna CCM, na Kuna vijiCCM vidogo vidogo lazima washiriki, kwa hyo hata wasipohudhuria lazim kile kilichokusudiwa kifanyike!

Kuna kitu kinatafutwa hapo, na lazima kipite taka msitake, msema kweli' Ni MUDA!
Wapitishe Watakavyo ila MUNGU atapitisha zaidi kuna Mtu Alipitisha KINGA yupo wapi na kinga yake Wanadamu wanapanga Kuumiza Watu lakini MUNGU ni FUNDI
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom