ACT wazalendo kuzindua kampeni leo

mcubic

JF-Expert Member
Mar 3, 2011
10,307
6,514
TAARIFA KWA UMMA



KESHO (leo)Disemba 31/2016 Chama cha ACT Wazalendo, tutazindua rasmi kampeni za kuwania Ubunge na nafasi za udiwani katika kata ambazo tumesimamisha wagombea

Kutokana na uzinduzi huo awamu ya kwanza ya viongozi wa kitaifa watagawanyika katika timu mbili tofauti kwa ajili ya kushiriki kampeni hizo.

Timu ya kwanza itaongozwa na mwenyekiti wa Chama Mama Anna Mghwira na makamu Mwenyekiti wa Chama Tanzania Bara, Mzee Shaban Mambo ambapo ziara yao itaanzia mkoani Geita katika kata ya Nkome(Disemba 31) Kahama katika kata ya Isagenhe(Januari Mosi),Dodoma katika kata ya Ihumwa(Januari 2),Morogoro, katika kata ya kiwanja cha ndege(Januari 3),Dar esSalaam katika kata ya Kijichi(Januari 4) na Zanzibar katika jimbo la Dimani (Januari 5)

Timu ya pili itaongozwa na kiongozi wa Chama Zitto Kabwe na Naibu katibu mkuu Bara Msafiri Mtemelwa, ambapo ziara yao itaanzia katika kata ya Kijichi jijini Dar esSalaam(Januari Mosi),Morogoro katika kata ya Kiwanja cha Ndege( Januari 2/2016) Ruvuma katika kata ya Tanga(Januari 3) Dodoma katika kata ya Ihumwa (Januari 4),Kahama katika kata ya Isagenhe(Januari 5) na Geita katika kata ya Nkome(Januari 6)

Chama cha ACT wazalendo kina matumaini makubwa ya kufanya vizuri katika maeneo tuliyosimamisha wagombea wetu na kuleta mabadiliko ya kiutendaji na kiuawajibikaji katika maeneo hayo huku tukitanguliza uzalendo kwa Taifa letu.

Chama cha ACT Wazalendo kinaendelea kusisitiza kuwa pale ambapo chama hakijasimamisha mgombea, wanachama, wafuasi na wapenda demokrasia na mabadiliko ya kweli wahakikishe wanampigia kura mgombea wa upinzani ambaye ana nguvu katika eneo hilo

Tunawahimiza wanachama wetu na wapenzi wa demokrasia popote pale walipo katika kata zinazofanyika uchaguzi kuhakikisha wanaiondoa CCM kwa kuwachagua wagombea wa vyama vya upinzani kwa ajili ya maendeleo ya maeneo yao

Imetolewa na Abdallah Khamis

Afisa Habari ACT Wazalendo

30/12/2016
 
Safi sana lakini ACT Makao Makuu jitahidini kupokea simu, kuna mashabiki wa chama wanalalamika wanapiga simu makao makuu kuulizia mambo mbali mbali kuhusu chama na mahali ofisi zenu zilipo simu hazipokelewi.......yaani makao makuu wana nyodo utafikiri ni Taasisi ya kutoa mikopo....Acheni hizo chama hakiwezi kujengwa kwa kudharau wanachama jirekebisheni la sivyo jahazi litazidi kuzama
 
Safi sana lakini ACT Makao Makuu jitahidini kupokea simu, kuna mashabiki wa chama wanalalamika wanapiga simu makao makuu kuulizia mambo mbali mbali kuhusu chama na mahali ofisi zenu zilipo simu hazipokelewi.......yaani makao makuu wana nyodo utafikiri ni Taasisi ya kutoa mikopo....Acheni hizo chama hakiwezi kujengwa kwa kudharau wanachama jirekebisheni la sivyo jahazi litazidi kuzama
Sawa....ujumbe umewafikia.
 
Nimependa hapo waliposema pale ambapo chama hakitasimamisha wagombea wahakikishe wanawapigia wapinzani wenye nguvu
 
Back
Top Bottom