ACT-Wazalendo jiepusheni kuwa wa kwanza kuripoti matukio yenye utata

Azizi Mussa

JF-Expert Member
May 9, 2012
9,172
7,428
Kwa sasa kama ilivyo kwa vyama vingine vya upinzani, ACT nao wanakimbizana na matukio. Hatuwalaumu sana kwa hilo kwa sababu mbalimbali lakini kuna tatizo kubwa Zaidi ambalo sasa linajitokeza. Changamoto kubwa zaidi ni kwamba; baadhi ya viongozi wa ACT wamekuwa na utaratibu wa kukimbilia kuwa 'wakwanza' kuripoti matukio yenye utata kwa habari wanazozipata mtandaoni.

Tunawashauri kama watashawishika na kuona hoja tutakazozitoa hapa zina uzito,basi hata kama wamechagua kukimbizana na matukio; angalau wajiepushe kukimbilia kuwa wakwanza kuripoti matukio yanayojitokeza mitandaoni na hasa ambayo ni 'negative'. Hii ni kwa sababu zifuatazo;-


  • Asilimia fulani ya taarifa zinazoanzia mitandaoni juu ya matukio tata zinakuwa za uongo.

  • Viongozi wakubwa wa vyama wanaposema kitu halafu kikawa si sahihi, namna ya kurudishia na kuendelea kuaminika inakuwa ngumu kidogo. Kwa hiyo kwa mfano, kama taarifa imetolewa na viongozi wa chama na baadae kubainika ni uongo, ni tatizo kubwa.na

  • Viongozi wakubwa wanatakiwa kujiepusha na ishu ndogo ndogo ili kupata muda wa kutosha kutafakari na kushughulikia ishu kubwa.
Kwa hiyo, hata kama kuna hamasa flani ya kuwa ‘wa kwanza’ kuripoti matukio tete, ni bora kuachia watu wa kawaida ili hata inapobainika taarifa si ya kweli linakuwa si tatizo sana.Sisi wengine tungependa kuona vyama vya upinzani vikiipa CCM vitu 'positive' vya kujifunza.
 
Tunatoa ushauri huu tukiamini kwamba uwepo wa upinzani unaojielewa na unaoonesha uwezo wa kiuongozi katika level ya vyama husika huonyesha ‘u mbadala’ ambao kwao CCM inaweza kujiangalia kama kioo na kujipima. Vinginevyo CCM inakosa mahali pa kujipimia na hivyo kujikuta ikiwa kama tajiri wa kijiji ambaye anamiliki corolla
 
Miaka ya 2015, kulikuwa na ushauri kwamba ACT wajitahidi kufanya siasa za masuala, misingi na ajenda na wajikite kwenye kuwajengea wanachama wao uwezo wa uongozi ili waweze kuonesha ‘u mbadala’. Hata hivyo wazo hilo halijafanikiwa hadi sasa. Pengine mbeleni linaweza likafanikiwa.Lakini tunaamini angalau hili la leo ni jepesi na watalielewa na kulifanyia kazi kama wakiamua kufanya hivyo maana kila kitu huanza na uamuzi.
 
Back
Top Bottom