ACT Wazalendo imesema nguvu za pamoja zinahitajika kufanikisha vita ya ulinzi wa rasilimali za taifa

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,498
9,279
Chama cha ACT Wazalendo kimesema zinahitajika nguvu za pamoja katika kufanikisha vita ya ulinzi wa rasilimali zetu ili ziweze kutumika kwa manufaa ya maendeleo ya taifa na siyo vinginevyo.

Mwenyekiti wa taifa wa ACT Wazalendo Yeremiah Maganja ameyasema hayo mjini Bunda wakati wa kikao chake cha ndani kati yake na viongozi wa mchama hicho mkoani Mara.

Mratibu wa Uchaguzi wa chama hicho taifa Mohamed Magala akaelezea mikakati ya chama katika uchaguzi wa viongozi wake.

Mwenyekiti wa ACT Wazalendo mkoa wa Mara Thomas Magero pamoja na wanachama Samuel Chure na Mwera Nyanguru wakatoa maoni yao.

Chanzo; ITV
 
Kumbe Kipo.
Nasikia Mwanzilishi Wake Amebaki
Yatima Ngoja Alelewe Na Baba Wa
Kambo Toka Magogoni.
Hata Kama Kwa Mputamputa Tu.
 
Zitto kabwe huwa anaikosoa serikali ambayo sehemu yake ni kitila mkumbo na anna mghwira

Hii inaitwa chichi dodo,ndege mmoja anayechukia sana kinyesi lakini anapenda kula funza wanaotokea baada ya kinyesi kuoza

Mama mghirwa amepelekwa Kilimanjaro akawakomoe akina mbowe kwa kumfukuza zitto chadema
 
Ahahaha mkuu umenikumbusha mbali sana kuhusu Chichidodo mambo ya "The Beautiful Ones Are Not Yet Born" namkumbuka Sangatiti pia
 
Back
Top Bottom