ACT-Tanzania kutoshiriki uchaguzi serikali za mitaa

Malata Junior

JF-Expert Member
Nov 29, 2011
3,101
2,536
Wakati leo ni siku ya mwisho kwa wagombea kurejesha fomu,hakuna mwanchama yeyote wa ACT aliyejitokeza! hii ni aibu sana.
 
kwa vile wewe ni mhongo' mumbea'mpenda mjungu
.napenda kukwambia kuwa kila wilaya.kila mkoa.kila mtaa tuna wagombea na wamerudisha FORMU zao jana.tusubili uchaguzi 14/12/2014
 
Hii ni udhibitisho kwamba hiki chama kimeanzishwa kuivuruga cdm na wala si kutwaa dola!
 
kwa vile wewe ni mhongo' mumbea'mpenda mjungu
.napenda kukwambia kuwa kila wilaya.kila mkoa.kila mtaa tuna wagombea na wamerudisha FORMU zao jana.tusubili uchaguzi 14/12/2014
i

Wewe unajua unachokiandika hicho.Ni wapi au ni kijiji,kitongoji/mtaa gani ACT mlipoweka mgombea????.
 
ACT NI CCM B kama CCM wamekuja kuchukua fomu ndo hao hao ACT
 
mumuogope mungu au ni dunia inaisha nani kakuambia ACT ni ccm au unaumwa

ACT ni ccm b kuazia kuundwa kuanzishwa kulipiwa ada mbalimbali na hata gharama za kujiendesha hili halina ubishi wala vitisho vya MWOGOPE MUNGU, Mungu hapaswi kujumuishwa hapa tunaishi kwenye dunia ambayo neno SIRI halina maana tena
 
Samahani ndugu ivi ww ni mutu ya wapi DRC ,RWANDA au BURUNDI?Nijibu please!!
Katika ukurasa huu nitakuwa nikileta tafakuri mbalimbali kumhusu Mhe. Sana Jaji Warioba na Waziri Mkuu Mstaafu. Kiini cha kuleta tafakuri juu yake ni nafasi yake kama alama pekee katika nchi yetu kwa sasa ya kiongozi aliyetukuka ambaye bado tunaishi naye. Yeye ndiye anabaki kuwa alama ya uzalendo kwa nchi yetu, heshima ya nchi yetu, utu, uhuru, uongozi bora na mambo mengine yaliyolifanya taifa letu kupata heshima kubwa ulimwenguni enzi za utawala wa awamu ya kwanza ya baba wa taifa marehemu Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Kama alama, Warioba anatofautiana na wengine wengine (wanaoishi kwa sasa) waliofuatia katika awamu zingine na wanaolitawala taifa letu kwa sasa. Watawala hao wengine wamelifanya taifa letu kuwa la aibu, lisiloheshimika na ambalo linakumbatia udhalimu wa aina mbalimbali.

Nikimtafakari Warioba simumalizi. Anauzalendo wa hali ya juu,utu, msimamia kweli ya wananchi, mkarimu kiasi kwamba anafanya kazi kama mtumishi wa wananchi. Ukianzia katika utumishi wake kama mwenyekiti wa tume ya rais ya katiba mpya unaona utu wake. Warioba amewaongoza wenzake kuachana na ubinafisi na kuwatumikia wananchi wa Tanzania katika kuwaletea rasimu ya katiba (aka Rasimu ya Jaji Warioba) ambayo imesheheni maslahi ya wananchi. Warioba ameendelea kuwa mtulivu katika kuhakikisha kuwa ndoto ya wananchi kupata katiba yao wanayoitaka inafikiwa. Kwake Warioba, kinachoitwa kudhalilishwa katika kufafanua katiba ya wananchi wanayoitaka ni ushindi, utumishi na alama ya kuwawakilisha vemawananchi. Amejishusha kutoka kuwa kiongozi hadi kuwa mtumishi mvumilivu kwa wananchi, akihamasishwa na ndoto yao wananchi ya kupata katiba wanayoitaka.

Katika tafakuri inayofuata, nitaeleza ninavyomuelewa Warioba, namana alivyoenenda akiwa mwenyekiti wa tume ya katiba na katika kongamano la katiba lililovamiwa na kuvunjwa na mazalio ya utawala uliolifanya taifa letu kuwa kichekesho na aibu kubwa ulimwenguni.
 
Chama hakina hata katiba wala viongozi wa kitaifa kitafanyaje uchaguzi! anayebisha anitajie katibu mkuu wa hiyo ACT ni nani?
 
kwa vile wewe ni mhongo' mumbea'mpenda mjungu
.napenda kukwambia kuwa kila wilaya.kila mkoa.kila mtaa tuna wagombea na wamerudisha FORMU zao jana.tusubili uchaguzi 14/12/2014
wewe ndio muongo, mbona hapa mtaani kwetu katika kijiji cha Lingusenguse hakuna mgombea wa ACT!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom