ACT- Tanzania baada ya kupata usajili wa kudumu wamefungua matawi mangapi?

Uongo kusema kwamba mnahangaika na ACT - Tanzania badala ya kujenga chama chenu. ACT -Tanzania hawana sababu yoyote ya kuja kwako kukueleza wanafanya nini, ishi maisha yako acha na wengine waishi wanavyodhani inafaa cha msingi wasivunje sheria za nchi

Ule msingi wa UWAZI wa ACT unawafanya wengi wautafute huo UWAZI. Kumbe ACT hawana sababu ya kueleza wanafanya nini japo wanaongozwa na msingi wa UWAZI?

Hapa tunakwazika.

By the way, lini mtakuwa WAZI kuhusu mambo ya pesa ambazo zimewezesha usajili? Mmepata wapi, na kiasi gani, na mmetumiaje?

Au UWAZI una maana tofauti?
 
Salaam wanajamvi,

Napenda kujua chama cha ACT-Tanzania mpaka sasa kimefungua matawi mangapi,na katika mikoa gani?Maana juzi nilikuwa Mbeya sijabahatika kuona bendera ya
ACT-Tanzania,hata Arusha,Dodoma,Morogoro,Iringa,Songea kote huko nimepita sijafanikiwa kuiona bendera hata moja ya ACT-Tanzania au hawajafika bado mikoa hii na kama hawajafika watashirikije uchaguzi wa serikali za mtaa utakaofanyika hivi karibuni au wamejitoa?

Naomba kuwasilisha.
ranfi moto ndio katibu mwenezi labda atakuwa na majibua
 
Ule msingi wa UWAZI wa ACT unawafanya wengi wautafute huo UWAZI. Kumbe ACT hawana sababu ya kueleza wanafanya nini japo wanaongozwa na msingi wa UWAZI?

Hapa tunakwazika.

By the way, lini mtakuwa WAZI kuhusu mambo ya pesa ambazo zimewezesha usajili? Mmepata wapi, na kiasi gani, na mmetumiaje?

Au UWAZI una maana tofauti?

Sema unakwazika sio tunakwazika kumbuka generalizaton is faras. Naomba usikwazike, Ofisi za ACT - Tanzania zipo ubungo NHC, karibu sana pale ndipo zilipo nyaraka zote za chama, majibu ya maswali yako yapo wazi. kama unahitaji kujua kweli wakaribishwa na utajuzwa nani kachangia nini na nini kimietumika. kwa kifupi mapato ya ACT - Tanzania yanatokana na michango ya wanachama na wapenzi wa ACT -Tanzania. Kumbuka uwazi sio uholela na kuwa wazi haimaanishi ACT - Tanzania waje nyumbani kwako kukupatia taarifa ya mapato na matumizi yao. Ikiwa ni shida kutembelea ofisi za ACT -Tanzania waweza kumtafuta mtanzania yeyote aliyekichangia chama atakupatia taarifa kwakuwa ni utaratibu wa ACT - Tanzania kutoa taarifa binafsi kwa aliyekichangia chama kumuonyesha namna fedha alizozichanga zilivyotumika, mimi ni mmoja wa waliochangia ACT - Tanzania na nilipewa taarifa ya maandishi namna mchango wangu ulivyotumika. Natambua inawasumbua sana kwa kuwa hamjazoea na hamjazoeshwa maisha ya uwazi. Pia ni busara kutambua na kuheshimu watu wengine msifikiri mnajua nyinyi tu. ACT - Tanzania hawajaanza operation mnaweweseka ninauhakika wakianza mtapata tabu zaidi. Muhimu ni hawa watu wa ACT hawakurupuki ndio maana mnawatusi lakini wanacheka, hiyo ni gentleman way ya kuonyesha dharau za kiwango cha juu. Waacheni wanawadharau
 
Tawi kubwa lipo Mwandiga, lingine lipo Ujiji.

Tawi dogo lipo Lumumba opposite na Ofisi za CCM
 
Kumbuka uwazi sio uholela na kuwa wazi haimaanishi ACT - Tanzania waje nyumbani kwako kukupatia taarifa ya mapato na matumizi yao.
Sasa hapo mbona mko sawa na wengine tu?

Mmeshaanza kisingizio cha UHOLELA, kuhalalisha kutokuwa WAWAZI? Hao waanzilishi walipokuwa kwenye vyama vingine hicho mnachoita UHOLELA sasa, ndicho walichokipigia kelele kuwa ni KUKOSA UWAZI. Double standards!!!

Kwa nini msifungue Website ambayo hata kama niko UGHAIBUNI naweza kupata taarifa zote. Si tumeambiwa mmekuja kidijitali ati.

Karibuni katika uwanja wa SIASA, si rahisi kama mlivyodhani.
 
ACT - Tanzania ni chama cha mabadiliko na uwazi, inasikitisha kuona hata vitu vidogo vinasumbua kueleweka, kumbuka hakuna taasisi isiyokuwa na utaratibu. Mahesabu ya ACT - Tanzania hayatakuwa kwenye website tu kama unavyoshauri yatawekwa katika vyombo vyote ili mradi kila mtanzania alieko kijijini na mjini ajue yanayotendeka na ACT - Tanzania. Ninaamini watakapoanza kutekeleza mipango yao kwa mujibu wa utaratibu waliojiwekea mtatambua kuwa wasaliti ni hao waliowaita wenzao wasaliti. Nashauri itafuteni taarifa ya mkaguzi na mdhibiti wa hesabu za serikali (CAG) ili mjue hao wanaowatumeni kuwatukana na kuwakejeli wazalendo wanafanya nini na rasilimali zenu
 
Unapofanya uenezi wa siasa lazima uwe na uvumilivu. Usitegemee wote ni wa akili kubwa, wengine ni wa kuelewa taratibu na utuchukulie hivyo. Jizuie kuhukumu kuwa anayehoji ametumwa. Sasa mbona hayo hayo ndio mnayolalamikia vyama vingine kuwa haviruhusu kuhoji. Mimi ni mtanzania mwenye uhuru wa kuhoji chochote na situmwi na yeyote. Ukinijibu vema unajenga chama chako.

Pia kumbuka UZALENDO sio label inayobandikwa kwa mtu. Uzalendo ni zaidi ya tabia, ni haiba na inathibitika kwa matendo ya mtu si maneno. Kama nahoji mapato na matumizi tu umekosa subira tayari, kuna kazi kubwa.

Ukinijibu kwa USTAARABU, UUNGWANA, UVUMILIVU, na UKWELI utanivuta mimi na wengine wengi. Si tumeambiwa hizo ndizo tabia za wana ACT.

Tunapenda tuzione kwa matendo.
 
Mimi situmwi na yeyote.

Pia kumbuka UZALENDO sio label inayobandikwa kwa mtu. Uzalendo ni zaidi ya tabia, ni haiba. Kama nahoji mapato na matumizi tu umekosa subira tayari, kuna kazi kubwa.

Ukinijibu kwa USTAARABU, UUNGWANA, UVUMILIVU, na UKWELI utanivuta mimi na wengine wengi.

Si tumeambiwa hizo ndizo tabia za wana ACT. Tunapenda tuzione kwa matendo.

UMEWAKABA hadi WANAKIMBIA ! SAFI SANA .
 
Hatuwezi kupoteza muda kujenga cha cha waigizaji yaani Tanzania act, hivi ma actress wanao wangapi mpaka hivi sasa , wangemchukua Shonza mama wa Mitusi angewafaa maana ccm ametumika akaisha wakatupa kuleeee dust bin
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom