ACT Maendeleo kabla ya kikao na msajili walihubiri katiba mpya baada ya kikao wanahubiri tume huru kulikoni?

Lord OSAGYEFO

JF-Expert Member
Feb 19, 2021
3,086
4,881
Hakika inashangaza sana Kuona Chama cha ACT MAENDELEO wakibadili GIA ANGANI na kuanza kuhubiri TUME HURU badala ya KATIBA MPYA. Tukio hili limetokea Mara tu baada ya KIKAO na MSAJILI wa VYAMA. Najiuliza kwanini Wameacha MADAI ya KATIBA MPYA kama CCM ambavyo HAITAKI?

KATIBA ni Sheria Mama hata hiyo TUME lazima itokane na KATIBA kwanini ACT hawaitaki KATIBA MPYA? Watanzania Tuamke Hiki Chama cha ACT sio Chama cha Kutupatia MAGEUZI TUYATAKO hiki CHAMA na KIONGOZI Wake ZITTO KABWE kipo kwa Ajili ya Kuvipotosha Vyama vya Upinzani ili KUILINDA CCM
"TUKISHTUKIE"

Sent from my SM-J600F using JamiiForums mobile app
 
Maandalizi ya katiba mpya yanaitaji bunge liandae kanuni kwa akili yako bunge hili la 100% Chama kimoja itakuwaje
Labda nikuulize swali, Afica ya Kusini walipofikia makubaliano ya kuutokomeza ubaguzi wa rangi baada ya miaka mingi ya mapambano, ndani ya bunge lao kulikuwa na wanachama wangapi wa ANC? Hoja za ACT ni kama za vibaraka wa wakati huo. Shauku yao ni kuwa na uwakilishi bungeni hata kama ni kwa haramu.
 
Demokrasia ni kuheshimu mawazo ya wengine hata kama uyapendi.

Wapo waliowahi kuhoji imekuwaje CHADEMA imempokea Lowasa na Sumaye, hakuna majibu yaliyowahi tolewa yakaridhisha.

ACT kwa sasa yenyewe inaona tume huru ndio ngazi ya kufikia katiba mpya, sasa hapo mtqbishana wee ila wote nia yenu ni katiba mpya.
 
Tume huru ya uchaguzi bila katiba mpya ni sawa na kuziba mashimo ya panya kwa mikate!

Maana Tanzania uchaguzi ni mfumo sio tume tu.Nguvu ya Rais na wateule wake, polisi, TISS, Jeshi, Tume, Tamisemi na wengineo lazima viangaliwe kwa pamoja kupitia katiba mpya.

Hiki kinachoitwa ni Tume huru ya uchaguzi ni changa la macho kwa wajinga ambao ndiyo wengi kwenye hii nchi.
 
Demokrasia ni kuheshimu mawazo ya wengine hata kama uyapendi.

Wapo waliowahi kuhoji imekuwaje CHADEMA imempokea Lowasa na Sumaye, hakuna majibu yaliyowahi tolewa yakaridhisha.

ACT kwa sasa yenyewe inaona tume huru ndio ngazi ya kufikia katiba mpya, sasa hapo mtqbishana wee ila wote nia yenu ni katiba mpya.
Kuhoji haimaanishi kutokuheshimu
 
KURA ya MAONI ya kupitisha KATIBA MPYA itasimamiwa na tume IPI ? Unaiamini Tume hii
Sio lazima NEC hii ndio ihusike kwenye kura ya maoni, inaweza kuundwa tume maalum ya kusimamia huo mchakato kama lilivyoundwa bunge maalum la katiba.
 
Back
Top Bottom