ACT hakiwezi kuwa chama kikuu cha Upinzani 2020, isipokuwa siku zijazo

Aiseee umeelezea vizuri Sana na nimekuelewa vizuri pia...
Ila hofu yangu ni idadi ya Wabunge wa CHADEMA, hapo umekadiria wanaweza kupungua Wabunge 15.

Mashaka yangu ni kwamba wanaweza wakapungua zaidi ya hiyo idadi hasa wale waliopata viti kwa nguvu ya EL, pia kuna wale ambao tayari walikwisha achia viti inamaana idadi ilishapungua pia. Bado watakaonunuliwa hatujui idadi kwa sababu naamini bado wapo watakaokubali kununuliwa. Haya ndio mashaka yangu tu...

Lakini pamoja na haya yote bado naamini huku bara CHADEMA itaendelea kuwa chama imara na mshindani wa kweli 2020.

GOD BLESS OUR NEXT PRESIDENT TUNDU ANTIPUS LISSU...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ebu jaribu kumpinga kwa hoja tuone akili yako ukubwa wake ukoje.
CCM tutamwachia baadhi ya majmbo CUF washinde kirahisi,ACT wazalendo tutawaacha washinde maeneo Wana nguvu , chadema tutawabana mbavu kuhakikisha tunapambana nao Barabara Kila watakapogombea.Matokeo CCM namba one,Act wazalendo namba mbili,CUF namba tatu , Chadema namba nne.Mchezo umeisha tukutane uchaguzii wa 2025.Act wazalendo ndio chama kikuu cha Upinzani 2020
 
Usitumie takwimu za 2015.Huo mwaka kura chadema walipata ni sababu ya Lowassa factor ambayo haipo Chadema tena.Sasa hivi ni Seif Sharif Hamad factor ndio italeta wabunge wengi kuliko Chadema.Chadema hakitakuwa chama kikuu cha Upinzani tena kuanzia mwakani nafasi yake itachukuliwa na ACT wazalendo kupitia Seif Sharif Hamad factor
We ni nani hadi umwambie asitumie takwimu za 2015?
 
Huyo Zitto mwenyewe unayemsema hana uhakika 100% kama atarudi 2020 Bungeni
Hahaha... Uko sahihi mkuu, Ila Zitto sio kama mnavyomdhania. Nasoma thread na post nyingi humu za watu humu nacheka. ACT ilidhaminiwa na Serikali 2015 kwenye kampeni na Maalim kwenda ACT sio bahati mbaya.Siasa ni mchezo wa hatari sana. Maalim Seif yupo kwenye Payroll miaka yote,Zitto pia. Lipumba ndo kashaivuruga CUF, hapa anayetafutwa ni CDM. Ngoja nikwambie kitakachotokea, dakika za mwisho ACT itakataa kuungana na Vyama vingine na itasimamisha wagombea wake nchi nzima, CUF pia. Zamu hii CDM itapata wabunge wachache Sana kuliko Vyama vingine.Itazidiwa na ACT na CUF. Pengine isiweze hata kupata ruzuku. Hawa wote ACT na CUF ni CCM B, na CCM C. Tatizo lingekuwa Maalim Seif angejiunga CDM. Ila alisetiwa aingie ACT kimkakati. Weekend hii watengeneza mazengwe wa CCM watafanya tafrija mpango umekamilika.Watu watabeza haya maelezo,watatukana ila December 2020 ndo wataelewa nilichomaanisha hapa.Kwa jicho la juu juu huwezi kunielewa.Tuombe uzima.
 
Badala ya kujadili sera za Chama na namna gani kinaweza kuwa chama dola, tunajielekeza zaidi kwenye ushabiki na kuitakia CDM mabaya...
Act haiwezi kukua tu kwa hisia zetu, lazima wajipange.... Hata kama Obama atahamia kule, kama hawajajipanga na kuwa na sera eleweki watabaki kuwa na mbunge mmoja.
Hizi kelele ni kwa sababu kuna Chadema au?
 
Aiseee umeelezea vizuri Sana na nimekuelewa vizuri pia...
Ila hofu yangu ni idadi ya Wabunge wa CHADEMA, hapo umekadiria wanaweza kupungua Wabunge 15.

Mashaka yangu ni kwamba wanaweza wakapungua zaidi ya hiyo idadi hasa wale waliopata viti kwa nguvu ya EL, pia kuna wale ambao tayari walikwisha achia viti inamaana idadi ilishapungua pia. Bado watakaonunuliwa hatujui idadi kwa sababu naamini bado wapo watakaokubali kununuliwa. Haya ndio mashaka yangu tu...

Lakini pamoja na haya yote bado naamini huku bara CHADEMA itaendelea kuwa chama imara na mshindani wa kweli 2020.

GOD BLESS OUR NEXT PRESIDENT TUNDU ANTIPUS LISSU...

Sent using Jamii Forums mobile app
Sifa moja ya wafuasi wengi hampendi kujiambia ukweli ili mjiandae mapema, ukweli ni kwamba Lissu hawezi kuwa Raisi wa nchi hii.Sio 2020 bali Kamwe(Never).Na kama CDM itapata wabunge 10 mwakani washukuru Mungu. Hili ninalosema sibahatishi nina uhakika nalo 100%.Waweza kubeza na kudharau maelezo yangu lakini ndo ukweli wenyewe. 2015 ulikuwa mwaka mzuri kwa upinzani na ndo uchaguzi mwepesi kwa upinzani pekee ambao hautatokea kwa miaka kadhaa ijayo.Pengine hata miaka 30. Zama za CHADEMA mwisho wake ni 2020, baada ya hapo chama kitabaki dormant kama NCCR na TLP. Si kwamba hakitakuwa na wafuasi, NO watakuwepo wengi ila kikibaki na wabunge 3 bila ruzuku ya kueleweka ndo mwisho wenyewe.Kubenea ataendelea na uandishi wa habari, Mdee atatafuta ajira nyingine, Mbowe atakuwa mjasiriamali(mfanyabiashara), kila mtu atarudi kwenye fani yake na maisha yatasonga kama kawaida. Usiniulize kwanini itakuwa hivyo,sababu ni moja tu ndo imeshapangwa hivyo na itakuwa HIVYO.
 
Hahaha... Uko sahihi mkuu, Ila Zitto sio kama mnavyomdhania. Nasoma thread na post nyingi humu za watu humu nacheka. ACT ilidhaminiwa na Serikali 2015 kwenye kampeni na Maalim kwenda ACT sio bahati mbaya.Siasa ni mchezo wa hatari sana. Maalim Seif yupo kwenye Payroll miaka yote,Zitto pia. Lipumba ndo kashaivuruga CUF, hapa anayetafutwa ni CDM. Ngoja nikwambie kitakachotokea, dakika za mwisho ACT itakataa kuungana na Vyama vingine na itasimamisha wagombea wake nchi nzima, CUF pia. Zamu hii CDM itapata wabunge wachache Sana kuliko Vyama vingine.Itazidiwa na ACT na CUF. Pengine isiweze hata kupata ruzuku. Hawa wote ACT na CUF ni CCM B, na CCM C. Tatizo lingekuwa Maalim Seif angejiunga CDM. Ila alisetiwa aingie ACT kimkakati. Weekend hii watengeneza mazengwe wa CCM watafanya tafrija mpango umekamilika.Watu watabeza haya maelezo,watatukana ila December 2020 ndo wataelewa nilichomaanisha hapa.Kwa jicho la juu juu huwezi kunielewa.Tuombe uzima.
Mkuu dah aisee mpaka nimeshtuka
 
Badala ya kujadili sera za Chama na namna gani kinaweza kuwa chama dola, tunajielekeza zaidi kwenye ushabiki na kuitakia CDM mabaya...
Act haiwezi kukua tu kwa hisia zetu, lazima wajipange.... Hata kama Obama atahamia kule, kama hawajajipanga na kuwa na sera eleweki watabaki kuwa na mbunge mmoja.
Hizi kelele ni kwa sababu kuna Chadema au?
Kwanini hilo usilijadili wewe mkuu?
 
Sifa moja ya wafuasi wengi hampendi kujiambia ukweli ili mjiandae mapema, ukweli ni kwamba Lissu hawezi kuwa Raisi wa nchi hii.Sio 2020 bali Kamwe(Never).Na kama CDM itapata wabunge 10 mwakani washukuru Mungu. Hili ninalosema sibahatishi nina uhakika nalo 100%.Waweza kubeza na kudharau maelezo yangu lakini ndo ukweli wenyewe. 2015 ulikuwa mwaka mzuri kwa upinzani na ndo uchaguzi mwepesi kwa upinzani pekee ambao hautatokea kwa miaka kadhaa ijayo.Pengine hata miaka 30. Zama za CHADEMA mwisho wake ni 2020, baada ya hapo chama kitabaki dormant kama NCCR na TLP. Si kwamba hakitakuwa na wafuasi, NO watakuwepo wengi ila kikibaki na wabunge 3 bila ruzuku ya kueleweka ndo mwisho wenyewe.Kubenea ataendelea na uandishi wa habari, Mdee atatafuta ajira nyingine, Mbowe atakuwa mjasiriamali(mfanyabiashara), kila mtu atarudi kwenye fani yake na maisha yatasonga kama kawaida. Usiniulize kwanini itakuwa hivyo,sababu ni moja tu ndo imeshapangwa hivyo na itakuwa HIVYO.
Huo "ukweli" wako tunauthibitishaje au tukuamini tu hivihivi kama vile tuko kwa kalmanzila?
 
ACT itabaki kupunguza kura za CHADEMA kama kilivyokusudiwa tangu mwanzo, hakitapata wabunge Bara, kama zitto asipogombea kigoma. Kwa Zanzibar wanaweza pata viti lakini havitatosha kuing'oa ccm, kwa sababu kwa sasa serikali itakuwa macho zaidi ya ilivyokuwa 2015. Waliponea chupuchupu hivyo msitarajie ubwete. hata ikibidi kura zihesabiwe na jeshi na matokeo yatangazwe na jeshi, lakini siyo CCM ishindwe Zanzibar.
 
Sifa moja ya wafuasi wengi hampendi kujiambia ukweli ili mjiandae mapema, ukweli ni kwamba Lissu hawezi kuwa Raisi wa nchi hii.Sio 2020 bali Kamwe(Never).Na kama CDM itapata wabunge 10 mwakani washukuru Mungu. Hili ninalosema sibahatishi nina uhakika nalo 100%.Waweza kubeza na kudharau maelezo yangu lakini ndo ukweli wenyewe. 2015 ulikuwa mwaka mzuri kwa upinzani na ndo uchaguzi mwepesi kwa upinzani pekee ambao hautatokea kwa miaka kadhaa ijayo.Pengine hata miaka 30. Zama za CHADEMA mwisho wake ni 2020, baada ya hapo chama kitabaki dormant kama NCCR na TLP. Si kwamba hakitakuwa na wafuasi, NO watakuwepo wengi ila kikibaki na wabunge 3 bila ruzuku ya kueleweka ndo mwisho wenyewe.Kubenea ataendelea na uandishi wa habari, Mdee atatafuta ajira nyingine, Mbowe atakuwa mjasiriamali(mfanyabiashara), kila mtu atarudi kwenye fani yake na maisha yatasonga kama kawaida. Usiniulize kwanini itakuwa hivyo,sababu ni moja tu ndo imeshapangwa hivyo na itakuwa HIVYO.
Inavyoonekana kura 2020 ulishapiga tiyari
 
Usitumie takwimu za 2015.Huo mwaka kura chadema walipata ni sababu ya Lowassa factor ambayo haipo Chadema tena.Sasa hivi ni Seif Sharif Hamad factor ndio italeta wabunge wengi kuliko Chadema.Chadema hakitakuwa chama kikuu cha Upinzani tena kuanzia mwakani nafasi yake itachukuliwa na ACT wazalendo kupitia Seif Sharif Hamad factor

Lowassa aliipunguzia CDM kura wala hakuiongezea,pia Lowassa aliipunguzia CDM viti vya ubunge!
Jinsi ambavyo Dr Slaa alivyo ijenga CDM na jinsi ambavyo CCM iligawanyika,kama CDM ingeweka tiketi ya Dr Slaa na Halj Duni wangepata kura zaidi na wabunge zaidi!
CDM walikosea mno kumtoa Dr Slaa!

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Huo "ukweli" wako tunauthibitishaje au tukuamini tu hivihivi kama vile tuko kwa kalmanzila?
Mkuu naamini kwa knowledge yako Ile ya vitabu vyako + uzoefu wako na awamu hii tangu November 9 - 2015 + za kuambiwa changanya na za kwako utapata majibu ukweli ni upi. Hata kama hautakufurahisha ila uzuri muda ukifika utaona mwenyewe kwa macho.
 
Inavyoonekana kura 2020 ulishapiga tiyari
Zamu hii hakuna kura, hiyo ni zuga tu. Naona bado mpaka sasa hamjaelewa mnadili na watu wa namna gani. Ukiamua kutangazia Kijiji kizima kwamba baba yako ni mbabe sana nyumbani, hata kama kuna mahali alikuwa anajilegeza atahakikisha anakuwa mbabe kweli ili kuitendea haki Ile sifa uliyomsambazia kijijini.Na Kijiji hakiwezi kumfanya kitu sababu atakufanyia ubabe usioacha alama. Mfano, waweza kulishwa ugali maharage asubuhi na jioni wiki nzima akidai ndo chakula kilichopo.Naomba niishie hapa.
 
Kwanza nianze kwakupongeza uamuzi wa busara wa Maalim Seif na wanamageuzi wote toka CUF walioporwa chama chao na CCM kwakushirikiana na Dola kujiunga na ACT kuendeleza mapambano. Ukomavu huu umewaacha hoi ccm wasiamini matokeo haya kwa kazi kubwa waliyoifanya kwa miaka minne ambapo inahitimishwa kwakiimarisha upinzani nchini badala ya kuubomoa.

Kwa zaidi ya masaa 24 sasa nimeona maoni ya jumla ya wadau wa siasa na wengine wasomi wazuri wakihitimisha kuwa sasa 2020 ACT kitakuwa ndio chama kikuu cha Upinzani nchini. Nimestaajabu sana huu muono unatako wapi? Nikajaribu kufuatilia kwa undani, nikajiridhisha ni propaganda iliyobuniwa na walioratibu kifo cha CUF, kwakuwa lengo lao ilikuwa ni kuua upinzani na upinzani wa kweli kwao ilikuwa ni CHADEMA.

Hii sio busara ya kiuchambuzi kubeba maoni ya mtaani nakufanya ndio tafakuri tanzu ya kisiasa, Mimi kama mwanasiasa mwanamajumui, nakubaliana kwamba ujio mpya wa Maalim Seif utazaa siasa mpya Bara, lakini naamini kwa dhati ya moyo na akili, Zanzibar itabaki ileile ya Maalim Seif ya 1995 hadi 2020. Hapa aliyeliwa ni CCM, Hesabu zao zimebuma na katika hili chama cha maoinduzi na dola yao wamepoteza pesa na muda kutwanga maji kwenye kinu.

Kwamba Maalim kuhamia ACT basi hii nihitimisho kwamba ACT kitakuwa chama kikuu cha upinzani 2020, huu ni upungufu wa ufikiri, Maalim alikuwa CUF, Je CUF kilikuwa chama kikuu cha upinzani? Chama cha ACT uchaguzi wa 2015 kilipata asilimia 0.2, je hii ni tafsiri kwamba Maalim kujiunga kitakuwa chama kikuu cha Upinzani? Majibu haya hoja hizo hayajibiwi kisiasa bali kwa namba na sayansi ya siasa.

Hatuzungumzi haya kwa kuhisia tu bali siasa ni namba, tukirejea takwimu za uchaguzi mkuu Tanzania 2015, matokeo ya jumla tunaona wazi ya kwamba uchaguzi wa mwaka huo uliohusisha majimbo 258 kati ya 262, CCM ilishinda ubunge katika majimbo 188, CUF 35, Chadema 34, NCCR–Mageuzi kiti kimoja. NLD haikupata kiti wakati ACT – Wazalendo ilipata kiti kimoja.

Kwamsingi huo, CCM ilipata viti maalumu 64, Chadema 36 na CUF 10. Kwa hesabu hiyo, Chadema ilifikisha wabunge 70 kutoka 48 wa mwaka 2010, CUF ilifikisha wabunge 45 kutoka 36 wa mwaka 2010 wakati NCCR-Mageuzi ilishuka kutoka wabunge wanne wa 2010 hadi mmoja na kufanya idadi ya wabunge wa Ukawa kuwa jumla 116. CCM ilifikisha wabunge 252.

Sasa turejee idadi ya wabunge 45 wa CUF, Wabunge 3 wamejivua uanachama na kujiunga CCM, nakufanya wabaki 39 tu. Na kati ya hao 39, wabunge 27 wa majimbo kati yao 22 kutoka Zanzibar, Wabunge 3 wa bara na Mbunge 1 wa viti maalumu hawa wanamuunga mkono Maalim Seif yaani hawa wamehamia ACT. Huku wabunge 4 wa majimbo na 9 wa viti maalumu hawa wako na Lipumba.

Sasa ili chama kiwe chama kikuu cha Upinzani ni lazima kiwe na idadi kubwa ya wabunge wa upinzani katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Na katika kutilia mkazo hilo, katiba ya Jamhuri ya Watu wa Zanzibar na kanuni za baraza la wawakilishi Zanzibar zimeweka utaratibu mzuri wa uwakilishi kutoka Zanzibar.

Kifungu cha 142 (1) cha Kanuni za Baraza la wawakilishi Zanzibar kimeeleza kuwa kutakuwa na wajumbe watano watakaochaguliwa na Baraza, kwa mujibu
wa masharti ya 66(1) (c) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ili kuliwakilisha Baraza katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kwanadharia hiyo, utaratibu wakuwapata wajumbe hao watano kwa Zanzibar umeelezwa katika katiba ya zanzibar, na kwa desturi utaratibu umekuwa ukitoa wajumbe wawili kutoka CUF na watatu kutoka CCM. Nakudanya idadi ya wawakilishi watano kutimia kutoka visiwani humo.

Sasa tukirejea kwenye namba tunapata kuona kwa tafsiri ya kawaida hadi dakika hii uchaguzi ungefanyika na wabunge walewale toka CUF wakashinda na kuwa wabunge toka ACT, Hii inamaana ACT itakuwa na wabunge 27 na Zitto 1 ambapo inakuwa 28. Viti maalumu wanaweza kupata 18, Sasa Jumla kuu wanakuwa na 38. Je hii inaweza kukiondoa CHADEMA chenye wabunge 70, kilichopata 36% ya kura uchaguzi 2015? Utoto huo. Zingatia ACT ilipata kura 0.2% tu.

Tutumie njia mbadala, tufanye wabunge 15 wa Chadema hawatarejea Bungeni, hivyo kufanya Chadema ipate wabunge 55 tu, na tufanye ACT itaongeza idadi ya Wabunge 15 hivi nakufikisha 53. Je itawezaje kuwa Chama kikuu cha upinzani kwa wabunge 53 tu dhidi ya Chadema yenye wabunge 55 baada ya kuporwa majimbo 15? Labda tunaishi katika fikra ndogo na kuogopa kufikiri kikubwa. Kuwa chama kikuu cha Upinzani Zanzibar au kuwa Chama Tawala Zanzibar hakukupi tiketi ya mojakwamoja kuwa chama kikuu cha upinzani Tanzania.

Hapa tathimini inafanyika huku Chama kizima cha Chadema kiko mahakamani, yaani viongozi wote na wanachama wake wote wenye ushawishi wako mahakamani kwa miaka minne mfululizo, Viongozi wakuu washakaa gerezani kwa zaidi ya miezi mitatu, Mikutano ya kisiasa imefungwa isipokuwa kwa ccm tu, Uhuru wa kutoa maoni umefungwa isipokuwa kwaccm tu. Bado Chadema itaendelea kuwa Chama kikui cha upinzani kama sikuwa chama Tawala 2020, na ikiwa kutakuwa na umoja katika upinzani, ni dhahiri kuwa kwa 99.9 CCM itaondoka madarakani ama itahitaji serikali ya mseto ili kuongoza nchi. Bunge litaamuliwa na upinzani.

Nimalize kwakuwatakia safari njema wale wanaohitaji kuhama vyama vyao, muda uliosalia ni mchache, kwani sheri ya vyama vya siasa ikishasainiwa mlazimika kubaki katika vyama vyenu hadi 2022.

Kama hujawahi kushuhudia uchaguzi mgumu na wahatari zaidi duniani, basi 2020 jiandae kushuhudia Rais Magufuli akikabidhi ofisi kwa njia ya amani kuipisha Chadema chini ya Rais Tundu Antipas Lissu. Hutaki unaacha!

Na Yericko Nyerere

View attachment 1049416
Kuna viti vya ubunge mliwadhulumu CUF kwa mwamvuli wa UKAWA...wait to face the music..eneo la Kaskazini mtapoteza zaidi ya nusu ya majimbo,hata Dar akina watu kama akina Kubenea hawarudi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama ungejua kuwa chama cha ACT-Wazalendo hakijawahi kuwa tatizo kwa CCM nadhani hata hii analysis yako usingepoteza muda kuijengea hoja. Hata baada ya kuingia kwa Maalim Seif na kundi lake, ACT-Wazalendo haitakuwa tatizo kwa CCM.

Tatizo lenu ni kuukataa ukweli hata kama ukitumia akili ya kawaida (common sense) kama unayo unaweza kuuona.

Kwa mwendo huu ACT-Wazalendo utakuwa chama kikuu cha upinzani Tanzania kama ilivyokuwa CUF baada ya Uchaguzi Mkuu 2000.

Kama kawaida historia inajirudia katika siasa za Tanzania.
Na hayo malengo yenu nyie mnaopanga haya ya kuua vyama.
Free and fair election hiyo sahau.
LAKINI
Mkiamua kwa dhulma kama kawaida yenu ,MTAWEZA.
Si itatamkwa tu kuwa chadema wasipate hata kiti kimoja na itaamuliwa ACT wapewe viti kadhaa?
Haya yote yakifanyika tunatambua ya kuwa toka awali
Zuberi Ruyagwa ni MTU wenu ndani ya sistim.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom