Ngongo
JF-Expert Member
- Sep 20, 2008
- 18,921
- 31,155
Wakuu wote heshima sana.
Sote tumekuwa tukifuatilia kesi ya UGAIDI inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA na watuhumiwa wengine watatu.
Jana baada ya upande wa mashtaka kuwaondoa mashahidi wanne,mtuhumiwa wa Ugaidi mwanajeshi mstaafu au ukipenda mstaafishwa alipanda kizimbani kwa minajili ya kujitetea.
Akiongozwa na wakili wa utetezi alibainisha wazi wakati wa ukamataji ACP Kingai alichukua simu zake na fedha kiasi cha Tsh 260,000.
Muungwana ni vitendo ni vyema Kingai akamrejeshea mtuhumiwa fedha zake bila kujali Mtuhumiwa atashinda au atashindwa kesi yake.
Ikiwa ACP Kingai alishatafuna fedha za mtuhumiwa na hali ya uchumi imemkalia vibaya basi atoe namba zake za simu Sisi waTanzania ni watu wenye huruma hakika tutachanga kama tunavyochangia watu wengine bila kinyongo wala hiyana.
Naomba kuwasilisha.