Binti Maringo
JF-Expert Member
- Jul 4, 2007
- 2,804
- 85
Kwa wanajumuiya wote wa Kitanzania,
salaaam!!
Tunapenda kutumia nafasi hii kuwaomba radhi jamii ya Watanzania wote waliojitokeza kwa mamia yao kwenye sherehe ya "OldSchool" mjini Columbus tarehe 5/7/2008.
Hakuna kina cha maneno au upambaji wa hoja unaoweza kuelezea masikitiko yetu kwa kushindwa kufanya siku hiyo kuwa ya kukumbukwa kwa uzuri wake, burudani yake na zaidi ya yote muziki wake mzuri, muziki wa zamani ambao wengi waliutarajia.
Licha ya maandalizi yetu yote tunaweza kukiri kwamba jukumu la kuandaa shughuli hiyo lilizidi mara nyingi sana uwezo wetu kama waandaji na hilo peke yake limekuwa funzo kubwa kwetu. Funzo la kwamba, tukitaka kuandaa kitu kizuri kwa Watanzania wenzetu hatuna budi kufanya na zaidi ya kufanya maandalizi yetu kuwa ya hali ya juu, bora, na ambayo yanaendana na viwango vya kimataifa.
Tulishindwa katika kuwapatia burudani ya muziki ambao wengi waliutarajia. Licha ya kwamba nyimbo zenyewe zilikuwa ni zile zilizopendwa miaka "ile" tatizo la uwezo mdogo wa nguvu ya umeme katika jengo tulilofanyia tafrija ilisababisha vyombo vilivyotumika kutumia nguvu nyingi ya umeme na hivyo kusababisha muziki kukatika katika. Hii ilikuwa ni kero ya dhahiri na jambo ambalo liliongeza kero zilizotangulia.
Kuna mengine mengi ambayo tungeweza kuyaeleza na kuwaomba radhi kwayo lakini kwa kifupi ni kuwa kama waandaji tunabeba mzigo wote wa kuwajibika kwa kushindwa kufanikisha kwa kiwango cha kuridhisha na zaidi ya kuridhisha yaani kuzikosha roho zenu pale Columbus siku ile ya Jumamosi. Funzo tulilolipata ni kubwa, na kwa pamoja na mmoja mmoja tunakubali makosa na mapungufu yote na ni sisi tu wenye kustahili kubeba lawama hizo zote.
Tunawashukuru kwa moyo wenu wa ukarimu na ukaribu, na zaidi ya yote kuchukiliana nasi katika mapungufu hayo. Tunawashukuru zaidi kwa kuja kwenu na kuweza kujumuika na kukutana na watanzania wengine katika mkusanyiko huu. Tunawashukuru wale wote waliojaribu kwa namna yao kutengeneza kilichoharibika. Mapungufu ya muziki yaliyojitokeza si kosa la Ma DJ tuliowaalika bali ni makosa ambayo hata wao yalikuwa nje ya uwezo wao, na kwa niaba yao tunawaombeni radhi ninyi nyote.
Tunaahidi kuwa kabla ya kuandaa kitu kingine kama hiki tutakaa chini na kujifunza (take a course) na kuhakikisha kuwa katika uchanga wa shughuli zetu hizi tutaweza muda si mrefu ujao kufanya tafrija ambayo siyo tu itakidhi matarajio ya wageni wetu bali itapita kila njozi yao na kufanya ndoto zao za tafrija zote kutimia. Tunahakikisha tunapata mawazo ya watu wengine waliobobea katika mambo kama haya.
Hilo tunawaahidi na mapungufu ya safari hii tunaomba mtuchukilie kama uchanga wa shughuli hizi kubwa lakini pia msisite kutupa nafasi inayostahili tutakapoweza kuwathibitishia pasipo shaka kuwa tumekomaa kufanya shughuli kama hizi.
Tunatanguliza Shukrani Zetu za dhati kwa uwezo wenu mkubwa wa kuelewa suala hili kwani Kufanya Kosa Sio kosa bali kurudia kosa ndio kosa.
Aksanteni nyote
Waandaji, (Tina Lupembe, Phanuel Ligate, Peter Kirigit, Lucas Mukami)