Ugonjwa wa Vidonda vya Tumbo (Peptic Ulcers Disease): Kinga, tiba na ushauri

Dawa ya vidonda vya tumbo Kutumia Dawa ya Hii ya Kienyeji Ukiamka Asubuhi kabla ya kula kitu akojowe mkojo wake mwenyewe kwa kipimo cha Glasi moja awe anakunywa mkojo wake kila siku Asubuhi kabla ya kula kitu kwa muda wa Siku Saba kisha Aende kupima hivyo Vidonda vya Tumbo Vitapona na kukauka kabisa jaribu kutumia hiyo Dawa itakusaidia Sana
 
ukiwaza kutaka kula chakula fulani, au ukiona chakula au kunusa harufu ya chakula, au unapokaribia mezani kutaka kuanza kula chakula; Tumboni mwako HAIDROKLORIKI ASIDI hutengenezwa kusaidia mfumo wa umeng'enyaji wa chakula. hadrokloriki asidi hii lazima ipunguzwe makali (it has to be neutralized). inapunguzwaje?, kwa kunywa glasi mbili za maji ya kawaida katika joto la kawaida kila nusu saa kabla ya kula chochote. ikiwa haitapunguzwa makali (kama ufanyavyo kila siku kula chakula bila kunywa maji kabla), basi haidrokloriki asidi huziunguza kuta za tumbo na taratibu kupelekea kile unachokiita vidonda vya tumbo!!!. tembelea: Home | maajabu ya maji
 
proloc vidonge ni vizuri sana kwa vidonda vya tumbo na pia uache kula vitu vya mafuta pilipili ndimu yai kundekunde chips vitu vya kukaanga pia cabbage,wali uliochemshwa nyama ya ngombe vitunguu nyanya mbichi usile kunywa maziwa kwa wingi na mbogamboga kama mchemsho
 
Vidonda vya tumbo
Jitahidi kukimbia vyakula vyenye tindikali?? (Acid) kama Limau, ndimu, binzari, maharage, pombe kali au pombe kwa ujumla nk ...1. Tiba ya Vidonda vya tumbo

Dawa yenyewe ni hivi, chukua kokwa la parachichi, likatekate vipande vidogo vidogo kisha anika juani mpaka likauke. Baadae saga ili kupata unga laini. Chukua yai la kuku wa kienyeji, pasua utoe kile kiini chenye rangi ya njano, changanya na ule unga ambao umeandaa awali, koroga ili kupata mchanganyiko mzuri.

Kisha mpe mgonjwa wako anywe kijiko kimoja mara tatu, baada ya siku tatu atakuwa amepona.

Baada ya hapo akitaka kujua kama amepona au la, anaweza kufanya test ya kawaida kabisa kwa kula maharage, au chakula chenye pili*2 au akaenda kupima hospitali kabisa.

2. Dawa ya vidonda vya tumbo tumia Dawa ya Hii ya Kienyeji - Ukiamka Asubuhi kabla ya kula kitu kojowa mkojo wako mwenyewe kwa kipimo cha Glasi moja uwe anakunywa mkojo wako kila siku Asubuhi kabla ya kula kitu kwa muda wa Siku Saba kisha uende kupima hivyo Vidonda vya Tumbo Vitapona na kukauka kabisa Mwambie jaribu kutumia hiyo Dawa itakusaidia Sana.

View attachment 36242

Asante sana! tutafaidika wengi, nitajaribu njia zote mbili.
 
hivi nini kinasababisha acid kuwa nyingi mwilini?
madhara yake?

uhusiano wa acid nyingi na vidonda vya tumbo ukoje???

tatizo la acid nyingi linatibika?????

vyakula vipi mtu asile?kwa mda gani??????
 
The Boss,

Vidonda vya tumbo (peptic ulcer disease) hutokea kwenye mfuko wa chakula (gastric ulcers) na pia kwenye sehemu ya kwanza ya utumbo mdogo (duodenal ulcers). Tumbo ni kati ya sehemu mwilini ambazo huzalisha acid kwa jili ya kusaidia kwenye uyeyushaji wa chakula na katika kulinda utumbo na uambukizo wa vimelea vinavyoleta magonjwa.

Kama tujuavyo acid hii yaweza kuunguza sehemu hii ya utumbo na hivyo kusababisha madhara. Kuna njia tumboni ambazo zinaulinda utumbo usiweze kupata madhara haya ya acid, mojawapo ikiwa ni utando wa mucous tumboni lakini pia regulation katika utengenezaji wa acid ili isije ikazidi. regulation hii ni automatic mwilini. Regulation na uzalishaji wa acid hufanywa chini ya matakwa ya mfumo wa neva. Kwa hiyo acid lazima iwepo kwa ajili ya umuhimu wake, lakini isiwepo kwa kiwango kinachoweza kuleta madhara (hii ndio essence ya regulation).

Vidonda vya tumbo hutokea pale ambapo kunakuwa na uzalishaji mwingi wa acid kupita kiasi au pale ulinzi wa tumbo dhidi ya acid unapopungua. Acid hutengenezwa na chembe hai tumboni zinazoitwa parietal cells.

Sababu za vidonda vya tumbo
1. uzalishaji wa acid nyingi tumboni - hii husababishwa na kuongezeka kwa chembe hai zinazozalisha acid, chembe hizi zaweza kuongezeka kwa sababu ya cancer (gastrinoma - husababisha ugonjwa wa acid nyingi unaoitwa Zollinger - Ellison Syndrome), lakini chembe hizi pia zaweza kujigawanya bila mpangilio (hyperplasia) hivyo zikawa nyingi na kusababisha uzalishaji wa acid kuongezeka.
2. Kutokuwepo na uwiano kwenye regulation ya uzalishaji wa acid, kunatakiwa kuwe na uwiano kati ya vile vitu vinavyoamuru uzalishaji wa acid na vile vinavyozuia. Inapotokea vile vinavyoamuru uzalishi vikavizidi nguvu vile vinavyozuia uzalishaji basi acid huzalishwa kwa wingi na hivyo kusababisha vidonda.
3. uambukizo wa bacteria aina ya Helicobacter pylori . Hawa huharibu ule utando unaolinda utumbo na hivyo kufanya acid iweze kupenya na kusababisha vidonda
4. Kuna dawa pia ambazo mgonjwa akitumia sana zaweza kumsababishia michubuko na vidonda tumbo, dawa hizi ni zile za jamii ya NSAIDs (Non steroidal anti-inflammatory disease) kama aspirin, brufen, indomethacin (indocid) na zote za jamii hii.

Mechanism ya utokeaji wa vidonda ni complex na nadhani nimeelezea kwa kifupi na lugha ambayo naamini imeeleweka.

Matibabu yapo ambayo hukusisha dawa zinazopunguza utengenezaji wa acid, dawa zinazoua bacteria wa H. Pylori lakini na upasuaji endapo hizi dawa zitashindwa. Vidonda vya tumbo hupona kabisa endapo mtu atapata matibabu sahihi.

Ili upate matibabu sahihi inabidi kwanza upate uchunguzi sahihi na ugonjwa sahihi ujulikane. Kwa yeote mwnye dalili za ugonjwa huu tafadhali usinunue dawa pharmacy, nenda hospitali, unaweza kufanyiwa uchunguzi na ukapewa tiba muafaka. Kipimo kiitwacho gastroscopy ndicho hutumiwa kupima na kugundua vidonda vya tumbo kwa uhakika.

The Boss, yangu ni hayo tu.
 
mtaalam yaani,shukran sana,kwa maelezo ya acid tumboni,kwa sasabu,mimi ni mgonjwa wa blood pressure,kila mwezi nikienda checking ananipa,dawa za bp na asprin,kwa ajili ya mzunguko wa damu,hebu nipe ushauri
 
Hii shule ya haja Kapotolo...bravo!
 
nimefaidika nami kupitia darasa hili, asante mwanzilishi wa mada na wataalamu wa waliotoa mchango wao.
 
hivi nini kinasababisha acid kuwa nyingi mwilini?
madhara yake?

uhusiano wa acid nyingi na vidonda vya tumbo ukoje???

tatizo la acid nyingi linatibika?????

vyakula vipi mtu asile?kwa mda gani??????

‘Mwili wa binadamu unapopungukiwa maji, hutoa ishara (indicators), tumeziita ishara hizo kuwa ni magonjwa. Hauumwi, una kiu, usiitibu kiu kwa madawa – dr.Batmanghelidj'.

Ukiwaza kutaka kula chakula fulani, au ukikiona chakula au kama unakaribia hivi mezani kutaka kuanza kula; tumboni mwako huzarishwa kitu kinaitwa haidrokloriki asidi ambayo ni mhimu kusaidia mfumo wa mmeng'enyo wa chakula. Lakini hadrokloriki asidi hiyo lazima ipunguzwe makali yake (has to be neutralized) ili isilete madhara katika tumbo na kuta zake. Ikiwa haitapunguzwa makali yake basi taratibu itaanza kuleta asidi kuzidi tumboni na hatimaye kushambulia kuta za tumbo ikiandaa daraja kuelekea vidonda vya tumbo.

Inapunguzwaje makali?,
kwa kunywa glasi mbili za maji (500 ml) kila nusu saa kabla ya chakula.
Ukiacha maji/chumvi, matunda na mboga za majani ambavyo ni vyakula vyenye alkalini, vyakula vingine karibu vyote vilivyobaki ni asidi; nyama, pasta, mikate, mayai na kadharika vyote ni asidi.

Mlo wa binadamu kwa siku unapaswa kuwa asilimia 80 mboga za majani na matunda na asilimia 20 iliyobaki vyakula vingine ambavyo si matunda au mboga mboga. Lakini kwa sehemu kubwa sisi huishi kinyume chake!!!.

Asidi kuzidi mwilini si ugonjwa,
wala mtu hapaswi kukuuzia dawa kwa sababu hii. Asidi kuzidi mwilini ni ishara kuwa mwili unapungukiwa maji kwa kuwa tunakunywa maji baada ya kusikia kiu tena ya baridi kabisa!!.

Soma maelezo yafuatayo taratibu................

MAJI YATAZUIA NA KUPONYA KABISA MAUMIVU MBALIMBALI MWILINI:

Ishara za mwanzo kabisa za asidi kuunguzwa ndani katikati ya seli au kwa maneno mengine asidi kuzidi kwenye seli za mwili na madhara ya kijenetiki ambayo yanaweza kujionesha, ni maumivu mbalimbali yanayozidi kujitokeza katika mwili.
Kutegemea na kiasi cha upungufu wa maji mwilini na namna na eneo lenyewe asidi ilipojijenga (ambayo ingeondolewa kwa kuongeza kunywa maji tu), maumivu maalumu ya mwili hujitokeza. Maumivu hayo yanajumuisha; kiungulia (heart burn), maumivu ya moyo (angina), maumivu sehemu ya chini ya mgongo (lower back pain), yabisi (rheumatoid), maumivu ya kichwa (migraine headaches), homa za asubuhi kwa kina mama wajawazito n.k

Watu wengi siku hizi hawawezi kuishi bila kumeza aina fulani ya dawa ya kupunguza maumivu.
Ni rahisi kuelewa namna gani maumivu ambayo hayajasababishwa na ajari au maumbukizo yanaweza kujitokeza mwilini.

‘Namna hii rahisi ya namna maumivu yanavyotengenezwa mwilini imetupumbaza wengi wetu sisi katika taaluma ya madawa tangu binadamu alipoanza kutafuta suluhu ya maumivu ya mwili kwa kutumia dawa – dr Batmanghelidj'.

Viwanda vya madawa vinatumia mabilioni ya fedha kutafiti dawa hizi na zile za kuondoa maumivu na mabilioni mengine zaidi hutumika kutangaza aina fulani ya dawa za kuondoa maumivu.
Upungufu wa maji mwilini (dehydration) unaweza kutibiwa kwa kuongeza kunywa maji tena bure bila gharama yeyote.

Ili kuuelewa mfumo wa utengenezwaji wa maumivu mwililini, tunahitaji kwanza kujifunza namna usawa wa asidi na alkalini unavyofanya kazi mwilini.
Hali ya uasidi husababisha kuunguzwa kwa baadhi ya miishio ya neva mwilini. Kunapotokea hayo, ubongo huonywa juu ya mabadiliko hayo ya kikemekali ya kimaeneo, ambayo sote hutafusiri kama MAUMIVU. Kwa maneno mengine, hali ya uasidi ndani ya mwili ndiyo hupelekea kusikia maumivu.

Kwa kawaida wakati damu yenye maji ya kutosha inapoizunguka seli, baadhi ya maji huingia ndani ya seli na kutoa nje molekuli za haidrojeni. Maji huisafisha asidi toka ndani ya seli na kuiacha sehemu ya ndani ya seli katika hali ya ualikalini ambayo ni hali yake ya kawaida na ya mhimu.

Kwa afya bora kabisa, mwili unatakiwa kubaki katika hali ya 7.4 katika kipimo cha ph (potential hydrogen).
Hali hii huhamasisha afya kwa sababu ndiyo hali inayoviwezesha vimeng'enya vinavyofanya kazi ndani ya seli ambavyo hupata ufanisi mzuri katika ph hii. Utiririkaji wa kutosha wa maji ndani na nje ya seli huifanya sehemu ya ndani ya seli kubaki na kuhimili hali yake ya kiafya ya kiualikalini.

Ndani ya miili yetu, figo husafisha haidrojeni iliyozidi ambayo husababisha asidi toka katika damu na kuiweka katika mkojo unaozarishwa. Kadiri mkojo unavyozarishwa kwa wingi ndivyo mwili unavyojiweka katika hali ya ualikalini kirahisi zaidi. Hii ndiyo sababu mkojo unaokaribia rangi ya uweupe ni kiashiria cha kufanikiwa kwa mfumo wa uondoaji wa asidi wakati mkojo wa rangi ya njano au chungwa ni ishara ya kuunguzwa kwa asidi mwilini.

Watu wanaodhani kwenda uani kwa ajili ya haja ndogo mara mbili au tatu kwa siku ni usumbufu kwao na hivyo kuacha kunywa maji ili kuzuia hilo hawana uelewa wa namna wanavyohatarisha miili yao.

Ubongo unalindwa vizuri zaidi dhidi ya asidi kutokana na ukweli kuwa unapata umhimu wa kwanza katika kusambaziwa maji kwa ajili ya mahitaji yake yote. Sehemu zingine za mwili haziwezi kuwa na bahati hii wakati maji yanapokuwa yanapatikana kwa njia ya mgawo. Ingawa upungufu wa maji unapobaki kwa muda mrefu, ubongo pia huathiriwa kutokana na hali ya uasidi katika seli, hivyo hali kama za kupoteza kumbukumbu na magonjwa ya mishipa hujitokeza.

Maumivu ambayo hayakusababishwa na jeraha au ajari, ni kiashiria kuwa tishu, ogani, maungio na seli vina asidi iliyozidi ambayo inahitaji kufanywa alkalini.

Kwa kunywa glasi moja (ml 250) ya maji halisi na kuchukua kipande cha chumvi ya baharini, kutapunguza kama siyo kuondoa kabisa maumivu. Jaribu hii kwa kunywa glasi moja ya maji na kisha kuiweka chumvi mwishoni mwa ulimi wako na kuiacha iyeyuke kwa dakika na kisha isafishe kwenda chini na glasi ya pili ya maji. Kwa mjibu wa dr.Batman, kitendo hiki kitabadili PH ya damu, tishu, ogani na seli ndani ya mwili.

Nitumie email yako niku-attachie file lenye orodha ya vyakula vyote duniani linaloonesha kiasi cha alkalini na asidi katika kila chakula.

Tembelea: maajabuyamaji2.artisteer.net
 
Ndg zangu naomba msada nasumbuliwa na vidonda vya tumbo je tiba yake nini au siluhusiwi kutumia nin.nashukulu kwa ushilikiano wenu
 
Kwanz a pole sana. Pili muone Dr. Rahabu pale Buguruni anatibu vidonda vya tumbo sana, au kama vipi nenda kwa Ndodi
 
Vidonda vya tumbo vinatibika hata hospitali ndugu yangu,tafuta mshiko tafuta daktari bingwa atakufanyia uchunguzi,utaandikiwa dawa na utapona cha msingi ni kuzingatia masharti na kumaliza tiba,maana hapo ndo kwenye mtihani! Pamoja na matangazo ya dawa za kienyeji yanayoungwa mkono na baadhi ya wataalam MIMI SIKUSHAURI KUTUMIA DAWA ZA KIENYEJI KWA SABABU,tz hatuna technologia ya kutengeneza dawa kutoka miti shamba katika hali ya usafi unaokubalika,kwa hiyo unaweza kupona vidonda lakini ukapata tatizo la figo au ini SAWAAA!
 
Asanten ndugu zangu kwa ushauli wenu nawaahidi nitautendea kazi nawatakia usiku mwema wapendwa.asanteni ila mwenye elimu azidi kutuelimisha mchango wako ni muhimu nauhitaji na kusamini
 
Vidonda vya tumbo vinatibika hata hospitali ndugu yangu,tafuta mshiko tafuta daktari bingwa atakufanyia uchunguzi,utaandikiwa dawa na utapona cha msingi ni kuzingatia masharti na kumaliza tiba,maana hapo ndo kwenye mtihani! Pamoja na matangazo ya dawa za kienyeji yanayoungwa mkono na baadhi ya wataalam MIMI SIKUSHAURI KUTUMIA DAWA ZA KIENYEJI KWA SABABU,tz hatuna technologia ya kutengeneza dawa kutoka miti shamba katika hali ya usafi unaokubalika,kwa hiyo unaweza kupona vidonda lakini ukapata tatizo la figo au ini SAWAAA!

vp ndg yng je hapo kwenye masharti umenitisha nakuomba japo unidokeze japo kidogo nami nifahamu japo hata dondoo
 
Ndg zangu naomba msada nasumbuliwa na vidonda vya tumbo je tiba yake nini au siluhusiwi kutumia nin.nashukulu kwa ushilikiano wenu

Pole Eric....Vidonda vya tumbo (Peptic Ulcer Disease) vinasababishwa na kutolewa kwa acid nyingi sana tumboni (tumbo kwa kawaida hutoa acid ambayo husaidia kataika kumeng'enya chakula). Acid inapotolewa kwa wingi, na ukuta wa tumbo (gastric wall) ukiwa dhaifu, na mara nyingi akiwepo bakteria anaitwa helicobacter pylori...baasi utapata vidonda vya tumbo. Vinaweza viakawa tumboni kwenyewe (Gastric Ulcers), hivi mara nyingi vinauma baada ya kula kwani ndio acid hutolewa kwa wingi. Au vikawa mwanzoni mwa utumbo mdogo (Duodenal Ulcers), hivi mara nyingi vinauma ukiwa na njaa..ukila vinapoa!

Umejuaje una vidonda vya tumbo? Mara nyingi vidonda vya tumbo huwa na dalili za maumivu ya tumbo kwenye chembe ambayo unayasikia kama yanaendelea mpaka mgongoni, maumivu yake yanakuwa ya kuchoma (kama kiungulia kikali). Kipimo cha kuthibitisha kinaitwa 'OesophagoGastroDuodenoscopy" au OGD, ambapo unaingizwa kama kampira fulani kadogo chenye kamera mdomoni, so kana piga picha kwenye koo (Oesophagus), tumbo na mwanzo wa utumbo mdogo..na vidonda vinaonekana. Pia kipimo cha damu cha kuangalia kama kuna huyo bacteria H.Pylori (serology for H.Pylori).

Matibabu yake mara nyingi ,i dawa za kumeza...inakuwa mchanganyiko wa dawa tatu ukijumuisha anti-acid 1 (Omeprazole, Lansoprazole, Pantoprazole, au Esomeprazole etc.) na antibiotics 2 (mara nyingi Clarithromycin na Amoxycillin). siku hizi kuna dawa ambayo imechanganya zote hizo pamoja inatwa 'Heligo Kit'. Huo mchanganyiko ni kwa siku saba tyhen unaendelea na anti-acid kwa muda mrfu kidogo mpaka utakaposhauriwa na daktari wako vinginevyo.

Japokuwa vidonda vya tumbo vinauma sana, unashuriwa usimeze dawa za kupunguza maumivu aina ya NSAIDs (mfano diclofenac, brufen etc) ambazo zinatumika sana kwa maumivu kwani zinafanya vionda vichimbike zaidi. Pia usitumie Aspirin na Steroids kwa muda mrefu.

Epuka vyakula vyenye asili ya acid mfano matunda yenye uchachu kama embe, machungwa, limau, ndimu, passion etc..navyakula vinasababisha acid itoke kwa wingi kama maharage, viungo vikali kwenye chakula, pilipili etc..
 
vp ndg yng je hapo kwenye masharti umenitisha nakuomba japo unidokeze japo kidogo nami nifahamu japo hata dondoo

epuka vyakula vyenye acid:usile mboga za majani(kijani),vyakula vyakukaanga,maharagwe,pilipili,tomato na vyakula vyenye nyanya

tumia sana maziwa fresh,kabichi na vyakula vya mchemsho, nikikumbuka vingine nitarudi
 
9 Reactions
Reply
Back
Top Bottom