Ugonjwa wa Vidonda vya Tumbo (Peptic Ulcers Disease): Kinga, tiba na ushauri

Wadau hivi kuna kipimo cha huu ugonjwa? Maana nauliza kwa kuwa sehemu nyingi madaktari wanaishia kuniuliza "una vidonda vya tumbo?" Badala ya kunifanyia vipimo...
Wengi wamekuwa wakiguess tu na kuniandikia dawa! Je kama kuna vipimo gharama yake ni kiasi gani? Je kuna tiba sahihi ya hizi dawa za hospitali?

NB; Nimekuwa nikisumbuliwa na tumbo kwa miaka sasa!!
Nenda Hospitali kubwa hapo ulipo ukapime na ukitumia dawa za hospitali kujitibia hayo maradhi yako na hujapona nitafute mimi nipate kukutibia upate kupona haraka.Ukihitaji tiba toka kwangu
Ukiwa na Shida yoyote ile
Usipo pona kwa Dawa za Hospitali nitafute mimi nipate kukutibia upate kupona ukihitaji matibabu yangu
Unaweza kunitafuta kwa Mawasiliano Herbalist Dr. MziziMkavu Email barua ya pepe. fewgoodman@hotmail.com What's App na Viber +905344508169
 
Endoscopy ndio kipimo sahihi cha kudetect vidonda vya tumbo mikoani hakuna hicho kipimo labda hosp kubwa kama kcmc bugando mbeya muhimbili regency agakhan dar na hizo kubwa kubwa za dar regency ni 160000 kama haijapanda ni bei ya mwaka jana na kote wanakubali bima ya afya pia, madaktar huwa wanakuuliza ili kama ulishapima uwape jibu wajue dawa za kukuandikia unaweza tu kuwajibu sijawahi kupimwa haitakugharim kitu kwa jibu hilo
 
Atumie vyakula visivyoungwa asitumie majani ya chai asitumie nyanya asile ndizi viazi mviringo mihogo machinese embe nanasi soda tumia zaidi tangawizi mdalasini changanya na asali lamba au mafuta ya mkia wa kondoo changanya na asali lamba au blueband changanya na asali lamba au unga wa ngano koroga na maji meza kijiko cha chai mara 2 kwa siku na tumia rabeprazole na relcer utasndikiwa na wataalamu hiki kitu kimenitesa sana toka 2012 sasa sina vidonda tena nimebaki na acid inazalishwa kwa wingi, zingatia muda wa kula usikae njaa epuka limao ndimu wine nk
 
Asilimia 90% ya vidonda vya tumbo vinasababishwa na bacteria aina ya helicobacter pylori kwa hiyo vipimo vinavyotumika ni
1. H. pylori test-Rapid test(test ya haraka)
2. Barium Meal-(Radiology-Inahusisha X-ray, yaani unachukua maji lita moja unachanagnya na barium sulpahte then unayanywa kisha wanakupiga X-ray)
3.Endoscopy-Ni kifaa kinacho ingizwa tumboni kupitia mdomoni na koo la chakula daktari huwa anakuwa na monitor pembeni inayomwezesha kuona kilichopo ndani,(It is the best investigation bcoz it can act not only diagnostic but also treatment)

Matibabu katika hospitali zetu ni
1.First line-Triple therapy(Dawa aina tatu-Amoxicillin, Omeprazole na Metronidazole up to 2 weeks) if fails
2.Second line-Triple therapy(Dawa aina tatu-Clarythromycin, lansoprazole na tinidazole up to 2 weeks) hupenda hutumia neno "helgo kit"
 
Pole sana mkuu. Kwanza, ni muhimu kufahamu sababu kubwa za vidonda vya tumbo (Peptic Ulcer Disease-PUD). Vidonda vinasababishwa na
(i) Kuambukizwa vijidudu vijulikanavyo kama Helicobacter pylori
(ii) Mawazo yaliyopitiliza, yani, "Excessive stress"
(iii) Utumiaji wa dawa zijulikanazo kama Non Steroidal AntiInflammatory drugs (NSAIDS) mfano Diclofenac, Diclopar, Aceclofenac etc
(iv) Unywaji pombe uliopitiliza.
Kwa Africa, tafiti nyingi zinaonyesha sababu kubwa kwetu ni infection ya huyo mdudu aitwaye H. pylori.

Vipimo vya muhimu vya kufanya kwa mtu anayesemekana kuwa na tatizo la vidonda vya tumbo ni
i. Serology for H pylori, ambapo damu yako itatolewa na utapimwa kuona kamaumeathiriwa na huyo mdudu na labda OGD (OesophagoGastroDuodenoscopy)/ Endoscopy kwa ajili ya kuangalia Koo lako ikiwa limeathiriwa na Tumbo lako pamoja na sehemu ya kwanza ya utumbo mdogo (Duodenum). Pia, unaweza kufanyiwa Barium Meal (inaweza kuona kama kuna kidonda) au Abdominal Ultrasound kwa ajili ya kuondoa uwezekano wa sababu nyinginezo za maumivu ya tumbo.
Ikiwa utaonekana kuwa na vidonda na sababu ikawa ni H pylori (yani Serology for H pylori ikawa Positive), basi matibabu ni kwa ajili ya vidonda na pia kwa ajili ya H pylori. Ikiwa H pylori ikiwa negative, basi matibabu yatakuwa kwa ajili ya vidonda tu. Lakini ikiwa hutokuwa na majibu ya Hpylori, basi matibabu yatakuwa kama mtu mwenye H pylori, maana wengi wetu wenye vidonda tunakuwa tuko infected na huyo mdudu.

Sasa, matibabu yako namna hii kwaupande wa dawa (Pharmacological treatment) kwa mtu mwenye H pylori na vidonda:

i. Proton pump inhibitor, mfano, Omeprazole au Esoneorazole au Rabeprazole. Kati ya hizo tatu, kali zaidi ni Rabeprazole.
Dozi, tukichukua mfano wa Rabeprazole (unatumia dawa moja tu, si zote tatu) ni:
Rabeprazole 20mg PO BD kila siku kwa wiki 6

ii. Antibiotics 2, zote unatumia kwa pamoja. Dozi zake ni:
a. Amoxycillin 1g PO BD kila siku kwa wiki 2 na
b. Azithromycin 500mg PO OD kila siku kwa wiki 2. Ikiwa una uwezo, badala ya kutumia Azithromycin unaweza kutumia

c. Clarithromycin 500mg PO OD kila siku kwa wiki 2.
OD=Unakunywa mara moja kwa siku
BD=Unakunywa mara mbili kwa siku
PO=Unameza (unakunywa kwa mdomo)...ni vidonge.

Aidha, tumbo likiwa linauma uma unaweza kutumia
a. Magnesium Trisilicate au
b. Relcer gel au Lucid Suspension au Mucogel 15mls PO TDS

Pia, kaa mbali na vyakula vyenye acid, kwa mfano, maharage na vyakula vyote vya jamii ya maharage, matunda machachu, ndizi mbivu na kuendelea. Pia, kaa mbali na pombe na kaa mbali na dawa za aina ya NSAIDs (Aspirin, Diclofenac, Diclopar, Aceclofenac etc). Pia jaribu kupunguzakuwa na msongo wa mawazo au kukaa na njaa kwa muda mrefu. Ukifuata yote hayo una uwezekano mkubwa wa kupona in notime. Best of luck & pole sana mkuu!
 
Zamani, dawa mojawapo kwenye hiyo triple therapy ilikuwa Metronidazole (Flagyl), ila kuna utafiti ulifanyika nchini na madaktari wa KCMC na kugundua kuwa mdudu anayesababisha vidonda (huyo H. pylori) amekuwa sugu (resistant) kwa Metronidazole, hivyo dawa hiyo imetolewa kwenye utaratibu wa kutibu vidonda vya tumbo vinavyohusiana na H. pylori
 
Wadau hivi kuna kipimo cha huu ugonjwa? Maana nauliza kwa kuwa sehemu nyingi madaktari wanaishia kuniuliza "una vidonda vya tumbo?" Badala ya kunifanyia vipimo...
Wengi wamekuwa wakiguess tu na kuniandikia dawa! Je kama kuna vipimo gharama yake ni kiasi gani? Je kuna tiba sahihi ya hizi dawa za hospitali?

NB; Nimekuwa nikisumbuliwa na tumbo kwa miaka sasa!!
vipimo vipo inabidi uende ukapige endoscopy kwenye hospital kubwa coz hicho kipimo wanaingiza mirija tumboni then wanaanza kuangalia tatizo kwenye compyuta bei yake sh.laki na elfu ishirini(120,000) but ukiwa nabima unatumia bima,coz mi mwenyewe icho kipimo nimepima nilitumia bima bugando hospital
 
Asilimia 90% ya vidonda vya tumbo vinasababishwa na bacteria aina ya helicobacter pylori kwa hiyo vipimo vinavyotumika ni
1. H. pylori test-Rapid test(test ya haraka)
2. Barium Meal-(Radiology-Inahusisha X-ray, yaani unachukua maji lita moja unachanagnya na barium sulpahte then unayanywa kisha wanakupiga X-ray)
3.Endoscopy-Ni kifaa kinacho ingizwa tumboni kupitia mdomoni na koo la chakula daktari huwa anakuwa na monitor pembeni inayomwezesha kuona kilichopo ndani,(It is the best investigation bcoz it can act not only diagnostic but also treatment)

Matibabu katika hospitali zetu ni
1.First line-Triple therapy(Dawa aina tatu-Amoxicillin, Omeprazole na Metronidazole up to 2 weeks) if fails
2.Second line-Triple therapy(Dawa aina tatu-Clarythromycin, lansoprazole na tinidazole up to 2 weeks) hupenda hutumia neno "helgo kit"
Heligo kit
 
Endoscopy ndio kipimo sahihi cha kudetect vidonda vya tumbo mikoani hakuna hicho kipimo labda hosp kubwa kama kcmc bugando mbeya muhimbili regency agakhan dar na hizo kubwa kubwa za dar regency ni 160000 kama haijapanda ni bei ya mwaka jana na kote wanakubali bima ya afya pia, madaktar huwa wanakuuliza ili kama ulishapima uwape jibu wajue dawa za kukuandikia unaweza tu kuwajibu sijawahi kupimwa haitakugharim kitu kwa jibu hilo
Kwa kuongezea hospitali ambapo vipimo vya endoscopy kinapatikana ni Kairuki na Alfa Clinic.
 
Mkuu mcheki huyu jamaa:0775048911.
Jamaa anakupa kama lita1 hivi unaenda kujaribu.
Ukiona inakusaidia ndio anakupa gharama zake.
Mie ilinisaidia sana na sasa niko poa.
Dumu la lita5 anakufanyia kwa 50,000-70,000 kutegemea na msimu maana jamaa haichukulii kama biashara bali kama kusaidia watu tu.Ni miti shamba.
Jamaa yupo Ukonga Dar.
 
Asante Cienfuegos maelezo yako yamekaa vizuri sana wengi tuna hilo tatizo umetusaidia sana nilitumia KIT kwenda kupima tena wakakuta hakuna vidonda ila acid ni nyingi mno ndio nahangaika nayo kuiondoa mwenye kujua dawa ya kuondoa acid aniambie hata kama miti shamba nimetumia sana asali mdalasini na tangawizi wapi
 
Back
Top Bottom