acid nyingi mwillini....

The Boss

The Boss

JF-Expert Member
Joined
Aug 18, 2009
Messages
37,832
Likes
23,161
Points
280
The Boss

The Boss

JF-Expert Member
Joined Aug 18, 2009
37,832 23,161 280
hivi nini kinasababisha acid kuwa nyingi mwilini?
madhara yake?

uhusiano wa acid nyingi na vidonda vya tumbo ukoje???

tatizo la acid nyingi linatibika?????

vyakula vipi mtu asile?kwa mda gani??????
 
Globu

Globu

JF-Expert Member
Joined
Jan 12, 2011
Messages
8,065
Likes
283
Points
180
Globu

Globu

JF-Expert Member
Joined Jan 12, 2011
8,065 283 180
Subiri wenye fani yao watakuja si muda mrefu.
 
kapotolo

kapotolo

JF-Expert Member
Joined
Sep 19, 2010
Messages
3,729
Likes
98
Points
145
kapotolo

kapotolo

JF-Expert Member
Joined Sep 19, 2010
3,729 98 145
The Boss,

Vidonda vya tumbo (peptic ulcer disease) hutokea kwenye mfuko wa chakula (gastric ulcers) na pia kwenye sehemu ya kwanza ya utumbo mdogo (duodenal ulcers). Tumbo ni kati ya sehemu mwilini ambazo huzalisha acid kwa jili ya kusaidia kwenye uyeyushaji wa chakula na katika kulinda utumbo na uambukizo wa vimelea vinavyoleta magonjwa.

Kama tujuavyo acid hii yaweza kuunguza sehemu hii ya utumbo na hivyo kusababisha madhara. Kuna njia tumboni ambazo zinaulinda utumbo usiweze kupata madhara haya ya acid, mojawapo ikiwa ni utando wa mucous tumboni lakini pia regulation katika utengenezaji wa acid ili isije ikazidi. regulation hii ni automatic mwilini. Regulation na uzalishaji wa acid hufanywa chini ya matakwa ya mfumo wa neva. Kwa hiyo acid lazima iwepo kwa ajili ya umuhimu wake, lakini isiwepo kwa kiwango kinachoweza kuleta madhara (hii ndio essence ya regulation).

Vidonda vya tumbo hutokea pale ambapo kunakuwa na uzalishaji mwingi wa acid kupita kiasi au pale ulinzi wa tumbo dhidi ya acid unapopungua. Acid hutengenezwa na chembe hai tumboni zinazoitwa parietal cells.

Sababu za vidonda vya tumbo
1. uzalishaji wa acid nyingi tumboni - hii husababishwa na kuongezeka kwa chembe hai zinazozalisha acid, chembe hizi zaweza kuongezeka kwa sababu ya cancer (gastrinoma - husababisha ugonjwa wa acid nyingi unaoitwa Zollinger - Ellison Syndrome), lakini chembe hizi pia zaweza kujigawanya bila mpangilio (hyperplasia) hivyo zikawa nyingi na kusababisha uzalishaji wa acid kuongezeka.
2. Kutokuwepo na uwiano kwenye regulation ya uzalishaji wa acid, kunatakiwa kuwe na uwiano kati ya vile vitu vinavyoamuru uzalishaji wa acid na vile vinavyozuia. Inapotokea vile vinavyoamuru uzalishi vikavizidi nguvu vile vinavyozuia uzalishaji basi acid huzalishwa kwa wingi na hivyo kusababisha vidonda.
3. uambukizo wa bacteria aina ya Helicobacter pylori . Hawa huharibu ule utando unaolinda utumbo na hivyo kufanya acid iweze kupenya na kusababisha vidonda
4. Kuna dawa pia ambazo mgonjwa akitumia sana zaweza kumsababishia michubuko na vidonda tumbo, dawa hizi ni zile za jamii ya NSAIDs (Non steroidal anti-inflammatory disease) kama aspirin, brufen, indomethacin (indocid) na zote za jamii hii.

Mechanism ya utokeaji wa vidonda ni complex na nadhani nimeelezea kwa kifupi na lugha ambayo naamini imeeleweka.

Matibabu yapo ambayo hukusisha dawa zinazopunguza utengenezaji wa acid, dawa zinazoua bacteria wa H. Pylori lakini na upasuaji endapo hizi dawa zitashindwa. Vidonda vya tumbo hupona kabisa endapo mtu atapata matibabu sahihi.

Ili upate matibabu sahihi inabidi kwanza upate uchunguzi sahihi na ugonjwa sahihi ujulikane. Kwa yeote mwnye dalili za ugonjwa huu tafadhali usinunue dawa pharmacy, nenda hospitali, unaweza kufanyiwa uchunguzi na ukapewa tiba muafaka. Kipimo kiitwacho gastroscopy ndicho hutumiwa kupima na kugundua vidonda vya tumbo kwa uhakika.

The Boss, yangu ni hayo tu.
 
O

omy100

Member
Joined
Jul 24, 2011
Messages
27
Likes
0
Points
0
Age
38
O

omy100

Member
Joined Jul 24, 2011
27 0 0
mtaalam yaani,shukran sana,kwa maelezo ya acid tumboni,kwa sasabu,mimi ni mgonjwa wa blood pressure,kila mwezi nikienda checking ananipa,dawa za bp na asprin,kwa ajili ya mzunguko wa damu,hebu nipe ushauri
 
Riwa

Riwa

JF-Expert Member
Joined
Oct 11, 2007
Messages
2,599
Likes
247
Points
160
Riwa

Riwa

JF-Expert Member
Joined Oct 11, 2007
2,599 247 160
The Boss,

Vidonda vya tumbo (peptic ulcer disease) hutokea kwenye mfuko wa chakula (gastric ulcers) na pia kwenye sehemu ya kwanza ya utumbo mdogo (duodenal ulcers). Tumbo ni kati ya sehemu mwilini ambazo huzalisha acid kwa jili ya kusaidia kwenye uyeyushaji wa chakula na katika kulinda utumbo na uambukizo wa vimelea vinavyoleta magonjwa.

Kama tujuavyo acid hii yaweza kuunguza sehemu hii ya utumbo na hivyo kusababisha madhara. Kuna njia tumboni ambazo zinaulinda utumbo usiweze kupata madhara haya ya acid, mojawapo ikiwa ni utando wa mucous tumboni lakini pia regulation katika utengenezaji wa acid ili isije ikazidi. regulation hii ni automatic mwilini. Regulation na uzalishaji wa acid hufanywa chini ya matakwa ya mfumo wa neva. Kwa hiyo acid lazima iwepo kwa ajili ya umuhimu wake, lakini isiwepo kwa kiwango kinachoweza kuleta madhara (hii ndio essence ya regulation).

Vidonda vya tumbo hutokea pale ambapo kunakuwa na uzalishaji mwingi wa acid kupita kiasi au pale ulinzi wa tumbo dhidi ya acid unapopungua. Acid hutengenezwa na chembe hai tumboni zinazoitwa parietal cells.

Sababu za vidonda vya tumbo
1. uzalishaji wa acid nyingi tumboni - hii husababishwa na kuongezeka kwa chembe hai zinazozalisha acid, chembe hizi zaweza kuongezeka kwa sababu ya cancer (gastrinoma - husababisha ugonjwa wa acid nyingi unaoitwa Zollinger - Ellison Syndrome), lakini chembe hizi pia zaweza kujigawanya bila mpangilio (hyperplasia) hivyo zikawa nyingi na kusababisha uzalishaji wa acid kuongezeka.
2. Kutokuwepo na uwiano kwenye regulation ya uzalishaji wa acid, kunatakiwa kuwe na uwiano kati ya vile vitu vinavyoamuru uzalishaji wa acid na vile vinavyozuia. Inapotokea vile vinavyoamuru uzalishi vikavizidi nguvu vile vinavyozuia uzalishaji basi acid huzalishwa kwa wingi na hivyo kusababisha vidonda.
3. uambukizo wa bacteria aina ya Helicobacter pylori . Hawa huharibu ule utando unaolinda utumbo na hivyo kufanya acid iweze kupenya na kusababisha vidonda
4. Kuna dawa pia ambazo mgonjwa akitumia sana zaweza kumsababishia michubuko na vidonda tumbo, dawa hizi ni zile za jamii ya NSAIDs (Non steroidal anti-inflammatory disease) kama aspirin, brufen, indomethacin (indocid) na zote za jamii hii.

Mechanism ya utokeaji wa vidonda ni complex na nadhani nimeelezea kwa kifupi na lugha ambayo naamini imeeleweka.

Matibabu yapo ambayo hukusisha dawa zinazopunguza utengenezaji wa acid, dawa zinazoua bacteria wa H. Pylori lakini na upasuaji endapo hizi dawa zitashindwa. Vidonda vya tumbo hupona kabisa endapo mtu atapata matibabu sahihi.

Ili upate matibabu sahihi inabidi kwanza upate uchunguzi sahihi na ugonjwa sahihi ujulikane. Kwa yeote mwnye dalili za ugonjwa huu tafadhali usinunue dawa pharmacy, nenda hospitali, unaweza kufanyiwa uchunguzi na ukapewa tiba muafaka. Kipimo kiitwacho gastroscopy ndicho hutumiwa kupima na kugundua vidonda vya tumbo kwa uhakika.

The Boss, yangu ni hayo tu.
Hii shule ya haja Kapotolo...bravo!
 
The Boss

The Boss

JF-Expert Member
Joined
Aug 18, 2009
Messages
37,832
Likes
23,161
Points
280
The Boss

The Boss

JF-Expert Member
Joined Aug 18, 2009
37,832 23,161 280
but je vyakula vipi mtu haruhusiwi kula?kwa mda gani?
 
Donnie Charlie

Donnie Charlie

JF-Expert Member
Joined
Sep 16, 2009
Messages
7,394
Likes
1,709
Points
280
Donnie Charlie

Donnie Charlie

JF-Expert Member
Joined Sep 16, 2009
7,394 1,709 280
nimefaidika nami kupitia darasa hili, asante mwanzilishi wa mada na wataalamu wa waliotoa mchango wao.
 
Fadhili Paulo

Fadhili Paulo

Verified Member
Joined
Sep 1, 2011
Messages
3,237
Likes
87
Points
135
Fadhili Paulo

Fadhili Paulo

Verified Member
Joined Sep 1, 2011
3,237 87 135
hivi nini kinasababisha acid kuwa nyingi mwilini?
madhara yake?

uhusiano wa acid nyingi na vidonda vya tumbo ukoje???

tatizo la acid nyingi linatibika?????

vyakula vipi mtu asile?kwa mda gani??????

[FONT=&amp]‘Mwili wa binadamu unapopungukiwa maji, hutoa ishara (indicators), tumeziita ishara hizo kuwa ni magonjwa. Hauumwi, una kiu, usiitibu kiu kwa madawa – dr.Batmanghelidj'.[/FONT]

Ukiwaza kutaka kula chakula fulani, au ukikiona chakula au kama unakaribia hivi mezani kutaka kuanza kula; tumboni mwako huzarishwa kitu kinaitwa haidrokloriki asidi ambayo ni mhimu kusaidia mfumo wa mmeng'enyo wa chakula. Lakini hadrokloriki asidi hiyo lazima ipunguzwe makali yake (has to be neutralized) ili isilete madhara katika tumbo na kuta zake. Ikiwa haitapunguzwa makali yake basi taratibu itaanza kuleta asidi kuzidi tumboni na hatimaye kushambulia kuta za tumbo ikiandaa daraja kuelekea vidonda vya tumbo.

Inapunguzwaje makali?,
kwa kunywa glasi mbili za maji (500 ml) kila nusu saa kabla ya chakula.
Ukiacha maji/chumvi, matunda na mboga za majani ambavyo ni vyakula vyenye alkalini, vyakula vingine karibu vyote vilivyobaki ni asidi; nyama, pasta, mikate, mayai na kadharika vyote ni asidi.

Mlo wa binadamu kwa siku unapaswa kuwa asilimia 80 mboga za majani na matunda na asilimia 20 iliyobaki vyakula vingine ambavyo si matunda au mboga mboga. Lakini kwa sehemu kubwa sisi huishi kinyume chake!!!.

Asidi kuzidi mwilini si ugonjwa,
wala mtu hapaswi kukuuzia dawa kwa sababu hii. Asidi kuzidi mwilini ni ishara kuwa mwili unapungukiwa maji kwa kuwa tunakunywa maji baada ya kusikia kiu tena ya baridi kabisa!!.

Soma maelezo yafuatayo taratibu................

MAJI YATAZUIA NA KUPONYA KABISA MAUMIVU MBALIMBALI MWILINI:

Ishara za mwanzo kabisa za asidi kuunguzwa ndani katikati ya seli au kwa maneno mengine asidi kuzidi kwenye seli za mwili na madhara ya kijenetiki ambayo yanaweza kujionesha, ni maumivu mbalimbali yanayozidi kujitokeza katika mwili.
Kutegemea na kiasi cha upungufu wa maji mwilini na namna na eneo lenyewe asidi ilipojijenga (ambayo ingeondolewa kwa kuongeza kunywa maji tu), maumivu maalumu ya mwili hujitokeza. Maumivu hayo yanajumuisha; kiungulia (heart burn), maumivu ya moyo (angina), maumivu sehemu ya chini ya mgongo (lower back pain), yabisi (rheumatoid), maumivu ya kichwa (migraine headaches), homa za asubuhi kwa kina mama wajawazito n.k

Watu wengi siku hizi hawawezi kuishi bila kumeza aina fulani ya dawa ya kupunguza maumivu.
Ni rahisi kuelewa namna gani maumivu ambayo hayajasababishwa na ajari au maumbukizo yanaweza kujitokeza mwilini.

‘Namna hii rahisi ya namna maumivu yanavyotengenezwa mwilini imetupumbaza wengi wetu sisi katika taaluma ya madawa tangu binadamu alipoanza kutafuta suluhu ya maumivu ya mwili kwa kutumia dawa – dr Batmanghelidj'.

Viwanda vya madawa vinatumia mabilioni ya fedha kutafiti dawa hizi na zile za kuondoa maumivu na mabilioni mengine zaidi hutumika kutangaza aina fulani ya dawa za kuondoa maumivu.
Upungufu wa maji mwilini (dehydration) unaweza kutibiwa kwa kuongeza kunywa maji tena bure bila gharama yeyote.

Ili kuuelewa mfumo wa utengenezwaji wa maumivu mwililini, tunahitaji kwanza kujifunza namna usawa wa asidi na alkalini unavyofanya kazi mwilini.
Hali ya uasidi husababisha kuunguzwa kwa baadhi ya miishio ya neva mwilini. Kunapotokea hayo, ubongo huonywa juu ya mabadiliko hayo ya kikemekali ya kimaeneo, ambayo sote hutafusiri kama MAUMIVU. Kwa maneno mengine, hali ya uasidi ndani ya mwili ndiyo hupelekea kusikia maumivu.

Kwa kawaida wakati damu yenye maji ya kutosha inapoizunguka seli, baadhi ya maji huingia ndani ya seli na kutoa nje molekuli za haidrojeni. Maji huisafisha asidi toka ndani ya seli na kuiacha sehemu ya ndani ya seli katika hali ya ualikalini ambayo ni hali yake ya kawaida na ya mhimu.

Kwa afya bora kabisa, mwili unatakiwa kubaki katika hali ya 7.4 katika kipimo cha ph (potential hydrogen).
Hali hii huhamasisha afya kwa sababu ndiyo hali inayoviwezesha vimeng'enya vinavyofanya kazi ndani ya seli ambavyo hupata ufanisi mzuri katika ph hii. Utiririkaji wa kutosha wa maji ndani na nje ya seli huifanya sehemu ya ndani ya seli kubaki na kuhimili hali yake ya kiafya ya kiualikalini.

Ndani ya miili yetu, figo husafisha haidrojeni iliyozidi ambayo husababisha asidi toka katika damu na kuiweka katika mkojo unaozarishwa. Kadiri mkojo unavyozarishwa kwa wingi ndivyo mwili unavyojiweka katika hali ya ualikalini kirahisi zaidi. Hii ndiyo sababu mkojo unaokaribia rangi ya uweupe ni kiashiria cha kufanikiwa kwa mfumo wa uondoaji wa asidi wakati mkojo wa rangi ya njano au chungwa ni ishara ya kuunguzwa kwa asidi mwilini.

Watu wanaodhani kwenda uani kwa ajili ya haja ndogo mara mbili au tatu kwa siku ni usumbufu kwao na hivyo kuacha kunywa maji ili kuzuia hilo hawana uelewa wa namna wanavyohatarisha miili yao.

Ubongo unalindwa vizuri zaidi dhidi ya asidi kutokana na ukweli kuwa unapata umhimu wa kwanza katika kusambaziwa maji kwa ajili ya mahitaji yake yote. Sehemu zingine za mwili haziwezi kuwa na bahati hii wakati maji yanapokuwa yanapatikana kwa njia ya mgawo. Ingawa upungufu wa maji unapobaki kwa muda mrefu, ubongo pia huathiriwa kutokana na hali ya uasidi katika seli, hivyo hali kama za kupoteza kumbukumbu na magonjwa ya mishipa hujitokeza.

Maumivu ambayo hayakusababishwa na jeraha au ajari, ni kiashiria kuwa tishu, ogani, maungio na seli vina asidi iliyozidi ambayo inahitaji kufanywa alkalini.

Kwa kunywa glasi moja (ml 250) ya maji halisi na kuchukua kipande cha chumvi ya baharini, kutapunguza kama siyo kuondoa kabisa maumivu. Jaribu hii kwa kunywa glasi moja ya maji na kisha kuiweka chumvi mwishoni mwa ulimi wako na kuiacha iyeyuke kwa dakika na kisha isafishe kwenda chini na glasi ya pili ya maji. Kwa mjibu wa dr.Batman, kitendo hiki kitabadili PH ya damu, tishu, ogani na seli ndani ya mwili.

Nitumie email yako niku-attachie file lenye orodha ya vyakula vyote duniani linaloonesha kiasi cha alkalini na asidi katika kila chakula.

Tembelea: maajabuyamaji2.artisteer.net
 
K

KIJIJI CHA HAKI

Senior Member
Joined
Apr 10, 2012
Messages
101
Likes
7
Points
35
Age
33
K

KIJIJI CHA HAKI

Senior Member
Joined Apr 10, 2012
101 7 35
asante kwa elimu hii.

je, uric acid nasababishwa na nini na tiba yake ni nini?
 
Forum statistics

Threads 1,249,419
Members 480,661
Posts 29,697,547