Achunguzi ufanywe kwa Rais Magufuli au kwa Serikali ya awamu ya tano?

Freddie Matuja

JF-Expert Member
Jul 21, 2018
1,466
2,860
Waslaam wakubwa

Naomba nianze na swali la msingi ambalo limekuwa sehemu ya mjadala. JSerikali ya awamu ya Tano ni nini au ni nani?

Swali la serikali ni nini? bila shaka huu ni mfumo wa utawala wa pamoja, mfumo wa kitaasisi ambapo kiongozi akishirikiana na wenzake wengi kuunda serikali.

Awamu ya tano ni nani? Bila shaka ni Rais na kwa mfumo wa Tanzania Rais na Makamu wa Rais japo inaongozwa na watu wawili tofauti ila imeunganikana kwa maana ya Rais anapogombea anakuwa na Makamu wa Rais kama mgombea mwenza.

Rais anakula kiapo na Makamu wa Rais nae anakula kiapo siku hiyo hiyo na ndani ya saa hilo=hilo katika tukio moja na uwanja mmoja.

Pengine tujiulize, serikali ya awamu wa tano walikuwepo akina nani?

Rais John Magufuli (2015-2021 March 17,)

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, kawa VP kwa muda wote wa awamu ya Tano (leo ni Rais wa nchi wa awamu ya 6)

Waziri Mkuu Kasim Majaliwa, kawa PM kwa wakati wote wa awamu ya 5 (na sasa bado ni waziri mkuu awamu kwa awamu ya 6)

Waziri wa Fedha Philip Mpango (leo ni Makamu wa Rais)

Waziri wa Ulinzi Dr. Hussein Mwinyi (2020-todate ni Rais wa Zanzibar) ni mjumbe wa cabinet kwa nafasi yake mpaka sasa kwa mujibu wa katiba.

Waziri wa utawala Bora George Mkuchika awamu ya tano (Mpaka sasa bado ni waziri ofisi ya Rais)

Waziri wa Utumishi, George Simbachawene na baadae akawa waziri wa mambo ya ndani na mpaka sasa awamu ya sita anatumika kwa nafasi kwa wazara hiyohiyo

Waziri wa Kilimo na Mifugo Mwigulu Nchemba, baadae akawa waziri wa mambo ya ndani, waziri wa sheria na sasa ni waziri wa fedha awamu ya sita

Waziri wa Viwanda wa sasa Kitila Mkumbo alikuwa katibu Mkuu (W) Maji awamu ya tano

Waziri wa Sheria Prof. Kabudi alikuwa waziri wa Sheria awamu ya Tano, akawa waziri wa mambo ya nje, awamu ya 6 karejea wizara ya sheria

Waziri wa Afya awamu ya 5 Ummy Mwalimu ni waziri wa TAMISEMI awamu ya 6

Waziri wa Kilimo wa sasa Prof. Mkenda kawa waziri awamu ya 5 na 6 na kabla ya hapo kawa katibu mkuu wa Wizara kadhaa awamu ya 5

Waziri wa Kazi na ajira Jenista Mhagama kawa hapo toka awamu ya 5 mpaka sasa awamu ya 6 amekalia kiti hicho hicho.

Orodha ni ndefu ukigusa wakuu wa mikoa, wilaya na wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama ambao bado wana-serve awamu ya 5 na 6.

Gavana wa Fedha alikuwa Prof. Beno Ndulu (aliaga dunia baada ya kustaafu) na sasa yupo Prof Luoga ambae alikuwepo awamu ya 5 na anaendelea na majukumu yake

Bunge kama likiamua kuchunguza awamu ya 5, litaichunguza ikulu pekee kwa kuangalia mkopo wa mabilioni ya fedha yalitumika Ikulu ikiwa ni ofisi ya Rais pekee au watachunguza kila wizara ambayo ilipokea fedha

Yawezekana kweli mabilioni yalitumika na JPM pekee ili ababe msalaba huko aliko?
Je yalipitia account zipi ili ku-trail zikatumikaje mpaka senti ya mwisho?

Huyu anaelaumu/mtoa hoja nae alikuwa sehemu ya serikali kama waziri; nae akikutwa na makandokando hata ya kutumia vibaya thumni, nae atawajibika kwa kiwango gani?

Ni maswali ya msingi kujiuliza na ni vema alikuja na hoja awe na orodha ya akina nani ni sehemu ya serikali ya awamu ya 5 na wengi wao wapo awamu ya 6 pia.

Weekend njema wakubwa
 
Nape yeye lengo lilikuwa kujipendekeza kwa Hangaya,uwaziri mtamu.

Anasahau kuwa Hangaya ndo alikuwa msaidizi wa JPM awamu ambayo anadai haikuwa na uwazi.
Na ndiyo maana hata urais alionao ni mwendelezo hatujafanya uchaguzi.
 
Kwani kinachotakiwa si uchunguzi wa kawaida wa hela za kodi zetu!? Sasa INA maana kuwa waziri na pato LA taifa unalimiliki!?
 
Back
Top Bottom