Achomwa moto kwa kudaiwa kusambaza ukimwi. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Achomwa moto kwa kudaiwa kusambaza ukimwi.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Bujibuji, Oct 6, 2010.

 1. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #1
  Oct 6, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,416
  Likes Received: 22,302
  Trophy Points: 280
  *Atuhumiwa kusambaza ukimwi.


  KATIKA kile kinachoonesha wananchi wamekata tamaa na kuamua kujichukulia sheria mkononi, wananchi wenye hasira kali wamevamia katika nyumba ya Grace Mremi (30), mkazi wa Kilema, na kuchoma moto nyumba yake kwa petroli kisha kusababisha kifo chake.

  Imedaiwa kuwa wananchi hao walivamia usiku katika nyumba hiyo kwa madai kuwa wamechoshwa na vitendo vyake vya kusambaza ugonjwa hatari wa UKIMWI kwa makusudi.

  Kwa mujibu wa mwenyekiti wa kikundi cha watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI cha Nia Njema aliyefahamika kwa jina moja la Erick mkoani humo, alipokea malalamiko kutoka kwa wananchi wa kijiji hicho kuhusiana na vitendo vya mwanachama mwenzao kutokana na tabia yake ya kueneza ugonjwa huo kwa vijana.

  Mwenyekiti huyo alisema baada ya kupata malalamiko hayo walizungumza na mtuhumiwa huyo ambaye alikana kuhusika na vitendo hivyo na kudai kuwa anasingiziwa.

  Mwenyekiti wa kijiji cha Kilema alikokuwa akiishi marehemu huyo, ambaye amekataa kutaja jina lake akidai kuwa yeye si msemaji, amesema ni kweli binti huyo alikuwa akieneza ugonjwa huo kwa makusudi.

  Amesema amekuwa akipokea malalamiko ya vitendo hivyo mara kwa mara na baada ya kufanya uchunguzi alibaini uchafu uliokuwa ukifanywa na mwanamke huyo.

  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Lucas Ngh'oboko, amethibitisha kutokea kwa kifo hicho kilichotokea usiku wa kuamkia leo.

  Amesema mwanamke huyo alikufa kwa moto baada ya watu wasiofahamika kumwagia petroli katika nyumba yake kisha kulipua kiberiti.

  Ameonya wananchi kuacha kujichukulia sheria mkononi kwani uchunguzi wa awali umeonesha kuwa mwanamke huyo aliuawa na watu hao baada ya kutuhumiwa kusambaza virusi vya UKIMWI kwa makusudi.

  Amesema jeshi lake linaendelea na upelelezi kuwabaini watuhumiwa hao na kufikishwa mbele ya sheria.
   
 2. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #2
  Oct 6, 2010
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Africa bana, sometimes huwa nakubaliana na usemi tulivyo!!!
   
 3. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #3
  Oct 6, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,416
  Likes Received: 22,302
  Trophy Points: 280
  Kweli Wachagga ni noma, yaani wanaua kwa sababu za kijinga kabisa.
  Hapo inatakiwa Mwenyekiti wa kijiji akamatwe na kuhojiwa.
  Maana maneno aliyoyaongea ni mazito mno.
   
 4. Sumbalawinyo

  Sumbalawinyo JF-Expert Member

  #4
  Oct 6, 2010
  Joined: Sep 22, 2009
  Messages: 1,286
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0
  Tatizo wenye viti wa wavijiji wanajipa mamlaka makubwa kuliko hata raisi.
  Wapewe elimu ya uraia na haki za binaadamu.
  Wapewe vijikozi vidogo vya uongozi,
  jitu halikumaliza hata darasa la saba ndilo linapewa uongozi wa kijiji.
  Unadhani ataongozaje?
   
 5. N-handsome

  N-handsome JF-Expert Member

  #5
  Oct 6, 2010
  Joined: Jan 23, 2008
  Messages: 2,317
  Likes Received: 128
  Trophy Points: 160
  RIP Grace maana hukubaka mtu walikua wanakuja wenyewe atiiiiiiiii
   
 6. Kiby

  Kiby JF-Expert Member

  #6
  Oct 6, 2010
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 5,209
  Likes Received: 1,012
  Trophy Points: 280
  Damu ya huyu binti itawasumbua sana maana wamemuua asiye hatia. Hivi tu kwa akili ya kawaida jamani kuna mtu analazimishwa kwenda kwa mwanamke au ni hiari yake mwenyewe inamsukuma kwenda kuitengua amri ya sita? Ndivyo basi umeamua kuivunja amri ni jukumu la nani la kubeba zana za kujikinga? Kwa nini bado tubaki kwenye ujinga wa kujitakia? Kama serikali ina nia ya kweli ya kujinasua na hivi vitendo vya kibaribariki ni lazima wale wote walioenda kulalama wakamatwe pamoja na huyu m/kiti wa kijiji na kufikishwa mbele ya sheria kwani. hawa ndio mastermind wa tukio.
   
 7. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #7
  Oct 6, 2010
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Tatizo siyo yeye ni hao wanaojuwa kuwa ana UKIMWI halafu wanakubali kutembea naye, inatisha sana!
   
 8. BabaDesi

  BabaDesi JF-Expert Member

  #8
  Oct 6, 2010
  Joined: Jun 30, 2007
  Messages: 2,795
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  .....halafu wanaishia kumuua! Nilitaka kusema hivyo hivyo.
   
Loading...