Achomwa kisu baada ya kummwagia mwenzake maji machafu kwenye birthday

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,495
9,275
MWANAFUNZI wa mwaka wa tatu katika Chuo cha Ufundi Trade Peramiho wilayani Songea, Grayson Maselin (23), amejeruhiwa na mwanafunzi mwenzake Mosses Ngole (23), kwa kuchomwa kisu shingoni baada ya kummwagia maji machafu siku ya kumbukizi ya kuzaliwa kwake (birthday).

6439024838d8cd5e485eccafbf266337

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma, Simon Maigwa Ngole, mwanafunzi wa mwaka wa nne katika chuo hicho, anadaiwa kumchoma kisu shingoni mwanafunzi mwenzake huyo na kumsababishia jeraha na kuvuja damu nyingi kwenye sherehe hiyo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma, Simon Maigwa, alidai tukio hilo lilitokea Jumatano majira ya saa saba mchana katika chuo hicho.

Alidai kuwa, siku ya tukio, Ngole alikuwa analazimishwa kumwagiwa maji na kupakwa matope na wanafunzi wenzake ndipo alipopandisha hasira na kufikia uamuzi wa kumchoma kisu mwanafunzi mwenzake huyo.

Kamanda Maigwa alidai mtuhumiwa anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kumjeruhi mwanafunzi mwenzake, ambaye kwa sasa amelazwa Hospitali ya Kanisa Peramiho.

Chanzo: IPP Media
 
Juzi juzi tu kuna dada mmoja jirani yangu ameteleza kwenye ngazi na kujigonga vibaya sehemu za kisogoni wakati akijaribu kuwakimbia marafiki zake waliokua na ndoo ya maukoko na maji machafu wakimkimbiza ili wammwagie. Mdada alichanika sehemu ya nyuma ya kichwa na ilibidi majirani tuingilie kati kumkimbiza hospitali ambapo alishonwa nyuzi kadhaa huku wale waliokua wanamkimbiza wakiishia kutoa tu mimacho kama mataahira bila kumpa msaada wowote.
 
Moja ya upuuzi ndio huo. Huu utamaduni wa kizungu tunaubeba na upumbavu wake.

Hivi jitu zima na kitambi mbele kama umbo la parachichi unasubiri watu wakuimbie happy birthday, baada ya hapo unamwagiwa maji.

Shame upon you and your family

Hizi birthday zimegeuka vituko, kuna watu wanakopa pesa kufanya sherehe ya birthday.
 
Moja ya upuuzi ndio huo

Huu utamaduni wa kizungu tunaubeba na upumbavu wake

Hivi Jitu zima na kitambi mbele kama umbo la parachichi unasubiri watu wakuimbie happy birthday, Baada ya hapo unamwagiwa maji

Shame upon you and your family

Hizi birthday zimegeuka vituko, kuna watu wanakopa pesa kufanya sherehe ya birthday
Si wote huwa wanakubaliana na kufanyiwa party bali huwa surprise party ambayo unashtukizwa na mayai viza usoni
 
Moja ya upuuzi ndio huo

Huu utamaduni wa kizungu tunaubeba na upumbavu wake

Hivi Jitu zima na kitambi mbele kama umbo la parachichi unasubiri watu wakuimbie happy birthday, Baada ya hapo unamwagiwa maji

Shame upon you and your family

Hizi birthday zimegeuka vituko, kuna watu wanakopa pesa kufanya sherehe ya birthday
Afu ukute hata nyumba halina limepanga, lina maisha ya kawaida afu mbaya zaidi halijawahi kufanya hata ibada tangu lizaliwe. Huu upuuzi sana yani naonaga hata pale ofisini kwetu jitu zima eti limekuja na keki na kisu ofisin eti afanyiwe birthday, lina miaka kama 45 HV pumbav kabisa.
 
Polisi msimuonee kijana wa watu,hivi mlitaka afanye nini?

Hivi angekuja kuripoti kwenu kuwa amemwagiwa maji machafu bila ridhaa yake si mngemkejeli tu!!

Ifike mahali ujinga huu,upigwe marufuku vyuoni maana ni moja ya utamaduni wa kishenzi sana.
 
Zamani tulikuwa tunatumiana kadi tuuu siku hizi Mambo yamekuwa mengi tena ya kipumbavu.
 
Huu ni ujinga mkubwa San! Mwaka Jana nilikua NIT Mabibo asubuhi saa NNE nikakuta kijana mmoja anammwagia maji binti mmoja hivi kwenye bomba!

Nikajiuliza, huyu vipi? Nikajua labda yule binti ni mgonjwa tena mgonjwa wa akili maana anamwagiwa maji lakini yuko kimya!

Nikavumilia weee ikabidi nishuke kwenye Gari nikaenda kuuliza, Jamani kulikoni? Kama ni mgonjwa nisaidie nimpeleke zahanati, nikashangaa wananicheka! Dah mara wanasema oogh ni birthday yake! Walllah sijawahi kuelewa dhana ya kumwagiwa maji na birthday...

Kumbe hata wapare ni washamba kama Wasukuma.....
 
Wapumbavu sana hao wanaomwagia watu maji,acha wajifunze adabu ili waache ujinga
 
MWANAFUNZI wa mwaka wa tatu katika Chuo cha Ufundi Trade Peramiho wilayani Songea, Grayson Maselin (23), amejeruhiwa na mwanafunzi mwenzake Mosses Ngole (23), kwa kuchomwa kisu shingoni baada ya kummwagia maji machafu siku ya kumbukizi ya kuzaliwa kwake (birthday).

6439024838d8cd5e485eccafbf266337

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma, Simon Maigwa Ngole, mwanafunzi wa mwaka wa nne katika chuo hicho, anadaiwa kumchoma kisu shingoni mwanafunzi mwenzake huyo na kumsababishia jeraha na kuvuja damu nyingi kwenye sherehe hiyo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma, Simon Maigwa, alidai tukio hilo lilitokea Jumatano majira ya saa saba mchana katika chuo hicho.

Alidai kuwa, siku ya tukio, Ngole alikuwa analazimishwa kumwagiwa maji na kupakwa matope na wanafunzi wenzake ndipo alipopandisha hasira na kufikia uamuzi wa kumchoma kisu mwanafunzi mwenzake huyo.

Kamanda Maigwa alidai mtuhumiwa anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kumjeruhi mwanafunzi mwenzake, ambaye kwa sasa amelazwa Hospitali ya Kanisa Peramiho.

Chanzo: IPP Media
Hatari sana ... Ameshafikishwa mahakamani? Vipi chuo kimeshatoa tamko la kumfukuza chuo mtuhimiwa? Au wanasubiri mzazi wa mtuhumiwa atie figisu figisu?
 
Back
Top Bottom