Achinjwa Kwa Shoka Kwa Kutembea na Mpenzi wa Mtu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Achinjwa Kwa Shoka Kwa Kutembea na Mpenzi wa Mtu

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by MziziMkavu, Jul 1, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Jul 1, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  MKAZI wa Uru Kusini mkoani Kilimanaro, aliyetambulika kwa jina la JAMES Kiwale (28), ameuawa kikatili baada ya kupigwa na shoka ya kichwa kwa kilichodaiwa kuwa ana uhusiano wa kimapenzi na mchumba wa mtu. James alikutwa na mkasa wakati alipokuwa akitoka makaburini kwenye mazishi ya jirani yake.

  Akitoa taarifa hiyo, Kamanda wa Polisi mkoani Kilimanjaro, Bw.Lucas Ng'oboko, amesema kuwa marehemu alipigwa na shoka kichwani na kupelekea kutenganishwa kati ya mwili na kichwa na kijana mmoja aliyefahamika kwa jina la Joachim.

  Alisema kijana huyo huyo aliamua kumpiga shoka mwenzake baada ya kumshuku kuwa alikiwa akitembea na mchumba wake aitwae Maria kitendo ambacho yeye hakukiafiki na kuchukua maamuzi hayo.

  Aliendelea kusema kuwa ilidaiwa kuwa, marehemu wakati wa uhai wake alikuwa akitamba kuwa atahakikisha kuwa anatembea na mwanamke huyo jambo lililomsababishia hasira kali mtuhumiwa na kufanya kitendo hicho cha unyama.

  Alisema mtuhumiwa huyo alimwekea mtego marehemu wakati anatoka kumzika jirani yake na kufanikiwa kumpiga shoka ya kichwa na kupelekea kichwa hicho kugawanyika mara mbili.

  Alisema mara baada ya kufanya kitendo hicho mtuhumia huyo alikimbia na juhudi za jeshi hilo zinaendelea kumsaka ili hatua za kisheria zifuate mkondo wake

  chanzo NIFAHAMISHE Tanzania news portal .: Habari za Tanzania :.

  Jamani tuache kuwatongoza wapenzi wa watu mwisho wake ndio huo. Mungu amlaze pema marehemu.
   
 2. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #2
  Jul 1, 2010
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  Hi habari mbaya, na pole kwa wafiwa.
  Lakini kung'ang'ania mchumba wa mtu....!mhh inahitaji moyo.

  Na huyo mchumba (binti) yuko ktk hali gani
   
 3. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #3
  Jul 1, 2010
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  mwache auwawe mkware huyu..wala asi rest in peace.
   
 4. Da Womanizer

  Da Womanizer JF-Expert Member

  #4
  Jul 6, 2010
  Joined: May 24, 2010
  Messages: 1,561
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Duh!
   
 5. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #5
  Jul 6, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  Kigogo una uhakika kama ni kweli alikuwa na mahusiano hayo??:A S 39:
   
 6. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #6
  Jul 9, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,809
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180
  Mpaka amefikia kutamba; ndio yale ya Mfanyabiashara kuzaa na mke wa mtu!:mad:
   
 7. DMussa

  DMussa JF-Expert Member

  #7
  Jul 11, 2010
  Joined: Sep 24, 2007
  Messages: 1,301
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Job well done..... This should be taken as a lesson on how much infidelity hurts!
   
 8. Bourgeoisie

  Bourgeoisie JF-Expert Member

  #8
  Jul 11, 2010
  Joined: Mar 26, 2009
  Messages: 611
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  Njia za kidemokrasia mara zote zinapendekezwa ili kumaliza migogoro ya aina yoyote. Madhara ya kuchukua hatua kama hii ni mabaya mno.Unaweza usifurahie tena umri wako uliobakia.
   
 9. Ras

  Ras Senior Member

  #9
  Jul 11, 2010
  Joined: Mar 16, 2007
  Messages: 126
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Laiti kama huyu jamaa hakutamba hapo awali ningekuwa na mtizamo mwingine lakini ilhari alitamba nadhani hilo lilompata Lamfaa sabau kuna wakware wengi hupenda kuharibu mahusiano ya watu bila sababu za msingi.
   
 10. b

  bitimkongwe JF-Expert Member

  #10
  Jul 11, 2010
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 3,034
  Likes Received: 211
  Trophy Points: 160
  Jamani wanaume mutahadhari na misifa yenu hiyo munayoona kwa kuchukua wachumba za watu.

  Hata kama alikuwa hatembei nae ile tabia ya kutamba tu ni ukosefu wa heshima. Kuna wengine hujisifu wametembea na fulani hata kama sio kweli ili kumkera mwenye mali yake. Wengine hasira zao ziko nje nje na matokeo yake ndiyo hayo ya kuuwawa kwa mashoka.

  Sio kwamba naona kitendo hicho ni kizuri, ingekuwa vyema kama akafanya uchunguzi, akiona ni kweli akaachana na huyo binti ijapokuwa hapo ni pachungu sana.
   
 11. Kafara

  Kafara JF-Expert Member

  #11
  Jul 11, 2010
  Joined: Feb 17, 2007
  Messages: 1,392
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 145
  huyo joachim (muuwaji) angekuwa shujaa au aliamini anafanya jambo la haki
  angebaki papo hapo. kwa kutimka anaonyesha ni muoga na hajiamini asilani.
  sasa huko alikokimbilia ataendelea kuuwa tu?

  huyu anayedaiwa kumegwa ni mchumba na sio hata mke. jamaa angeweza kuchomoa
  na kumshukuru mola wake kwa kumuonyesha mapema ukweli (kama kweli maria alikuwa$anamegwa na
  mtu mwengine) hivyo kumuepusha na machungu kwenye ndoa.

  sasa kaua na amekuwa mtuhumiwa wa mauaji. na akikamatwa kipindi atakachokuwa lupango maria
  ataendelea kumegwa na yeye vilevile wasela wa lupango wanaweza kumuwowa vilevile.

  ama kweli hasira hasara
   
 12. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #12
  Jul 11, 2010
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  RIP James, nadhani hukumbaka Maria ni makubaliano tu! Sheria Ichukue mkondo wake na Joachim naye ahukumiwe kufa
   
 13. K

  KABAZI JF-Expert Member

  #13
  Jul 12, 2010
  Joined: Apr 19, 2010
  Messages: 303
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Dawa ya watu wa tabia hiyo ndio hiyo. Alifikiri ni ushujaa kuiba vya wenzake!!
   
 14. Nyamayao

  Nyamayao JF-Expert Member

  #14
  Jul 12, 2010
  Joined: Jan 22, 2009
  Messages: 6,980
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0
  Amen....
   
 15. Joste

  Joste Senior Member

  #15
  Jul 12, 2010
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 117
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Maisha na wanawake wa siku hizi utachnga wangapi


   
Loading...