Achilia mbali ruzuku na michango, CHADEMA ina vyanzo gani vya mapato? | Page 6 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Achilia mbali ruzuku na michango, CHADEMA ina vyanzo gani vya mapato?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Petro E. Mselewa, May 17, 2017.

 1. Petro E. Mselewa

  Petro E. Mselewa Verified User

  #1
  May 17, 2017
  Joined: Dec 27, 2012
  Messages: 7,664
  Likes Received: 10,705
  Trophy Points: 280
  Binafsi naamini kuwa chama cha siasa ni taasisi. Naamini hivyo pamoja na kutowahi maishani mwangu kujiunga na chama chochote cha siasa hapa Tanzania na kwingineko. Kama taasisi,chama hujiendesha kwa gharama.

  Kuna kuwalipa waajiriwa wa chama,kugharimia shughuli za kila siku za chama,kugharimia ziara na operesheni za kichama na kadhalika. Taasisi hujiendesha katika hali ghali. Chama,ili kupambana na changamoto za kiuendeshaji na kisiasa,kinapaswa kuwa na vyanzo vya mapato

  Kwa uelewa wangu,chama kama CCM kinamiliki mali mbalimbali kama majengo na viwanja vya mpira. Hizo pekee,ingawa kuna mengine,ni vyanzo vya mapato ya chama. Vipi kuhusu CHADEMA,kama chama kikuu cha upinzani nchini na taasisi muhimu kidemokrasia?

  Achilia mbali ruzuku kwa vyama vya siasa na michango ya wanachama,wafuasi,wapenzi,wakereketwa,wafurukutwa na wafia chama,CHADEMA ina vyanzo gani vingine vya mapato? Ina mipango gani ya kujiimarisha kiuchumi?

  Michango ya wanachama,hasa Wabunge wa CHADEMA,wakati mwingine ni mzigo na inakera. Ifike mahali CHADEMA iwe na vyanzo vyake vya mapato kama taasisi ili kujiimarisha na kuaminika. Ni kazi ya Bodi ya Wadhamini ya CHADEMA kusugua bongo

  Aione: Tumaini Makene ,Mmawia na wengineo
   
 2. M

  Mbase1970 JF-Expert Member

  #101
  May 19, 2017
  Joined: Jun 11, 2015
  Messages: 3,706
  Likes Received: 2,327
  Trophy Points: 280
  Kwani ninyi watu wawili huu ubishi wenu umejikita katika nini zaidi maana sijawaelewa kabisa.. Naomba mnijulishe.
   
 3. M

  Mbase1970 JF-Expert Member

  #102
  May 19, 2017
  Joined: Jun 11, 2015
  Messages: 3,706
  Likes Received: 2,327
  Trophy Points: 280
  Kwani ninyi watu wawili huu ubishi wenu umejikita katika nini zaidi maana sijawaelewa kabisa.. Naomba mnijulishe.
   
 4. Mohamed Said

  Mohamed Said Verified User

  #103
  May 19, 2017
  Joined: Nov 2, 2008
  Messages: 11,231
  Likes Received: 6,397
  Trophy Points: 280
  Mbase,
  Nguruvi3
  hajafurahi mimi kuandika kitabu kinaitwa, ''The Life and Times of
  Abdulwahid Sykes (1924 - 1968) The Untold Story of the Muslim Struggle
  Against British Colonialism.''

  Hiki kitabu kilichapwa London, 1998 na kiko katika toleo la nne.
  Ukisoma kitabu hiki utaweza kufuatilia majadiliano haya.
   
 5. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #104
  May 19, 2017
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,300
  Likes Received: 7,492
  Trophy Points: 280
  Mohamed , bandiko 103, jaribu kuwa mkweli ili Mbase1970 aelewe.

  Hakuna mahali nimeonyesha au kuzungumzia vitabu vyako na kama kupo onyesha hapa.
  Inafikia mahali uwe mkweli na nitamweleza Mbase kiini cha mjadala huu

  Bandiko la mada linauliza vyanzo vya mapato vya vyama kama Chadema kwa kuangalia kuwa CCM ina vitega uchumi na hivyo huenda ni wakati vyama vingine vikaangalia utaratibu wao

  Mkuu JokaKuu akajibu asingependelea vyama vijiingize katika biashara akitoa sababu zake

  Nguruvi3 akamjibu JokaKuu, anakubaliana naye kwani kufanya hivyo kutaviweka vyama katika mikono ya wafanyabiashara na hilo linaweza kuwa tatizo. Mbali na hayo, vyama vitaondoka katika umiliki wa wanachama na kujali kitu badala ya utu. Tumejifunza kutoka historia

  Somo ni kama la mfanyabiashara aliyempa Mwalimu sh 200 za mboga wakati mwalimu anapuyanga bila senti kwenda kutafuta kitoweo na kibaba. Nikamnukuu Mohamed Said kama mwanazuoni aliyeeleza hilo

  Kuanzi hapo hoja yangu ikawa, vyama vichangiwe na wanachama kwa nyoyo zao ili mbele ya safari umiliki ubaki kwa wanachama, vijiondoe katika biashara na kujikita katika siasa

  Kwa namna ambayo siijui Mohamed Said kaja akiwa amecharuka, akitweta na kufuka

  Kaleta majina na vitabu vyake nje ya mada kama kawaida yake kukwepa hoja.
  Hapo ndipo nilipombana maana nipo naye siku nyingi najua red and blue corner, knock out ni kawaida

  Kibano cha kwanza kikamlazimu akiri na alete ushahidi kuwa maandiko yake yalilenga kumdhalilisha Mwalimu. Leo wajukuu wanasoma habari ambazo Mshume aliyetoa pesa asingependa ziwe hadharani

  Mohamed akaja na Abadul, nikamwambia kumdhalilisha Nyerere hakumfanyi Abdul awe bora

  Abdul ana zama zake , Nyerere ana zake. Ndipo nikamkumbusha picha ya siku nyingi aliyoleta kuonyesha Nyerere alikuwa anavaa Kaptula. Hilo liliambatana na fundi cherehani wa Mwl kumuonyesha alivyoanza kuvalishwa mjini. Katika mazingira ya kawaida dhalili hiyo kipimo chake hakijaundwa

  Hilo lilitokea miaka 5 iliyopita wakati wa jitihada za kumfanya Nyerere si lolote si chochote

  Hapo akawa amegusa nerve kwasababu Nyerere anabaki kuwa na kadi 1 licha ya Kaptula na njaa

  Nyerere aliongoza mapambano ya uhuru hata kama akina Mkwawa na Sykes walianzisha, ni historia
  Nyerere amekuwa Rais wa nchi hii, Abdul hakuwahi kuwa hata katibu mkuu
  Nyerere ni wa kitaifa na kimataifa, Abdul ni wa kidongo chekundu na tanda mti

  Hayo hayamfanyi mpigani uhuru yoyote na popote awe chini au mchango wake uwe mdogo
  Hata aliyetoa glasi ya maji ni mtu muhimu na wote tunawashukuru na kuthamini michango yao

  Tusichokipenda ni kuandika historia za kumdhalilisha fulani na kuzunguka duniani kana kwamba hilo ndilo liliwaweka wazee wetu pamoja. Wazee wetu walikuwa pamoja kwa faida ya vizazi ambavyo ni sisi

  Haya unayoona ya Mohamed ni katika hofu na kimuhe muhe, tunajuana na anajua nikikaa mguu sawa sio wale wa kukaa na kuhadithiwa wakiita. Ninahoji , nina fikira, nina ufahamu. Hilo analijua vema

  Alichokueleza hakina maana na kinasikitisha kwa hadhi yake. Pitia bandiko la kwanza hadi hili utaona

  Tumsamehe kwani ni uungwana na always yupo 'defensive' akidhani kuna attack ya maandiko yake
  Mohameda anachotaka ni watu wasome, wakae kimya , wamshangilie! hewalaaa mambo sawi

  Hapana! hilo si rahisi, tutahoji , tutachambua na tutafanya reference bila kuonea au kupendelea
   
 6. gwa myetu

  gwa myetu JF-Expert Member

  #105
  May 19, 2017
  Joined: Aug 18, 2014
  Messages: 4,336
  Likes Received: 4,340
  Trophy Points: 280
  Kwa akili yako chadema inaweza kufanya biashara mfano kiwanda au supermarket bila ccm kuweka mizengwe ya kodi kupitia Tra na Nemc hadi wakafunga hiyo biashara?
  Kama Arusha tu wanapoongoza jiji hawawezi hata kukusanyika kwenda kuwapa pole wafiwa ndo serikali hii ya kimaku itawarusuhu chadema kufanya biashara na kupata faida? Haiwezekani
   
 7. Cannibal OX

  Cannibal OX JF-Expert Member

  #106
  May 19, 2017
  Joined: Aug 27, 2014
  Messages: 2,083
  Likes Received: 2,220
  Trophy Points: 280
  Team Ulipo Tupo hadi Chooni inarudisha hela iliyotumika 2015.
  Ukitaka kula lazima uliwe
   
 8. Mohamed Said

  Mohamed Said Verified User

  #107
  May 19, 2017
  Joined: Nov 2, 2008
  Messages: 11,231
  Likes Received: 6,397
  Trophy Points: 280
  Nguruvi3,
  Ungefikaje kwa Mshume Kiyate kama nisingemwandika katika kitabu cha
  Abdul Sykes?

  Ungejuaje kama Nyerere ana kadi no. 1 aliyoandikiwa na Ally Sykes kama
  nisingesema hayo katika kitabu cha Abdul Sykes?

  Kama wewe ni bingwa wa kuhoji mimi ni bingwa wa kutafiti na kuandika
  ''corrective histrory.''

  Nimeisahihisha historia ya uhuru wa Tanganyika na sasa ile historia rasmi
  leo haina nafasi tena.

  Hapana mimi sikimbii maswali na ndiyo unaona mkisikia niko hapa mnajazana
  kuja kunisikiliza.

  Umelipenda sana suala la ''kaptula,'' lakini hiyo ni fikra yako tu ya dhana.

  Picha hiyo si mie niliyeipiga na historia yake iko ndani ya kitabu cha Abdul Sykes
  atakae anaweza kuisoma.

  Nyerere hakika aliongoza mapambano ya uhuru lakini mbona hawakutajwa na
  wale aliokuwa pamoja na yeye kama Sheikh Hassan bin Amir, Idd Faiz
  Mafungo,Tatu bint Mzee, Halima Selengia, Ali Migeyo, Dharura bint
  Abdulrahman, Salum Mpunga, Hamza Mwapachu, Joseph Kasella
  Bantu, Sheikh Yusuf Badi, Dr. Michael Lugazia
  haya ni kwa uchache.

  Wasomaji waliposoma kazi walizofanya watu hawa katika uhuru wa Tanganyika
  ndipo hapo kitabu kikawa kinakwenda kama maandazi ya moto.

  Wakajua kuwa walidanganywa waliyokuwa wanasoma si historia ya TANU.

  Mipango ilikuwa ya kumchagua Chief Kidaha Makwaia awe rais wa TAA 1950
  kisha waunde TANU haya yote yapo katika kumbukumbu za Sykes.

  Majina haya na mambo mengi muhimu hayakuwapo katika historia rasmi.

  Wangejuaje watu kuhusu mchango wa Earle Seaton katika hotoba aliyosoma
  Nyerere UNO 1955 kama nisingeeleza vipi Abdul Sykes alivyomuingiza TAA 1950.

  Sasa mimi vipi ati nikatae kuhojiwa na wasomaji wangu wanaponiuliza haya
  niliyoandika?

  Ati nisamehewe.
  Ati nataka kushangiliwa,

  Nikishangiliwa mwisho iwe nini?
  Kusahihisha makosa katika historia ya Tanganyika imekuwa kudhalilisha.

  Mimi sizunguki duniani kwa kujipeleka naalikwa kwa kile ambacho ninacho.
  Wakati mwingine hata mie hushagaa nawauliza mmnijuaje?

  Jibu tulikusikia ukizungumza pale mahali kadha, tumesoma kitabu chako,
  ''paper,'' yako fulani nk. nk.

  Mimi kusoma na kuandika ndiyo maisha yangu ndiyo maana unaiona hapa JF
  nimekuwa mashuhuri na wewe ukija na hoja najitahidi kukujibu kwa kadri ya
  uwezo wangu.

  Mimi nikuhofie wewe kwa kipi kaka?

  Andika kitabu na paper na wewe unijibu hapa JF utahangaika na mimi sana na
  kamwe hutaweza kunishinda.

  Hili nimekuambia na kukushauri siku nyingi sana.
   
 9. Kipigi

  Kipigi JF-Expert Member

  #108
  May 19, 2017
  Joined: Aug 20, 2012
  Messages: 733
  Likes Received: 226
  Trophy Points: 60
  Pokea ushauri mkaufanyie kazi, acha porojo
   
 10. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #109
  May 20, 2017
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,300
  Likes Received: 7,492
  Trophy Points: 280
  Thank you, hii ni tofauti na kauli kwamba nakataa vitabu vyako kinyume na mada iliyopo.
  Next time useme kuwa ubishi uliopo ni kwasababu Nguruvi amefanyia reference mmoja wa watajwa katika vitabu na kwasababu zipi. Huo ndio uungwana siyo kuzuesha yasiyokuwepo

  Hivi Mohamed , kadi ya Nyerere TANU ilikuwa siri? Mbona wajukuu wake wanajua hilo
  Hata mpuuzi anajua kwasababu TANU ni Nyerere na Nyerere ni TANU. Period
  'corrective' kwa mujibu wako.
  Period
  Fallacy! Abdul hakumuingiza Nyerere TANU. Nyerere alikuwa katika siasa akiwasiliana na wenzake kutoka Kampala. Alikuwa katibu wa Tawi Tabora na alihudhuria mkutano mkuu. Abdul alimshirikisha si kumuingiza katika siasa
  Ukialikwa usiende kumsumanga Nyerere na matembele, Vitoga, Nguruka n.k.
  Ndiko kushangiliwa nilikoongelea ambao kwako ni sehemu muhimu

  Mohamed, ukweli unaposwa kuishi nao ni huu. Post industrial revolution katika modern Politics Nyerere jina lake linaandikwa kwa kalamu nyingi sana na viwanda bado vinatengeneza kalamu.
  Hakuna kiwanda kitakachotengeneza 'kifuto' cha historia ya Nyerere hata siku moja

  Nyerere yupo UNO, AU, EAC, Tanzania na mitaani. Wapo wengine katika kanda za Africa kama akina Govan Mbeki, Mandela, Kimathi, Kabaka kwa uchache. Katika nchi wapo akina Mkwawa ambao Ujerumani wanajulikana, Mirambo n.k.

  Mitaani nako hawakosekani huko Tandamnti , Narung'ombe n.k.

  The bottom-line Nyerere ni icon katika modern politics za nchi yetu. Viatu vyake havijapata mvaaji, si jana , si leo
   
 11. Mohamed Said

  Mohamed Said Verified User

  #110
  May 20, 2017
  Joined: Nov 2, 2008
  Messages: 11,231
  Likes Received: 6,397
  Trophy Points: 280
  Nguruvi3,
  Hakuna anaekataa ukubwa na umaarufu wa Nyerere.
  Wala hilo halijapata kuwa tatizo kwangu.

  Hakika Nyerere kaandikwa na kalamu nyingi sana ila...

  Ila kalamu zilizomuandika Nyerere nchini petu zilikuwa na kasoro na hapo
  ndipo mimi nilipoingia kuandika historia kama ukweli ulivyokuwa kuanzia
  siku ya kwanza mipango ya kumtia Nyerere katika uongozi wa TAA
  inafanyika.

  Labda hujui lakini Nyerere alipelekwa kwa Abdul Sykes na Joseph
  Kasella
  Bantu akiwa na barua aliyopewa na Hamza Mwapachu amfikishie
  Abdul.

  Hii ilikuwa 1952 na nyumba aliyopelekwa Nyerere ilikuwa Mtaa wa Aggrey
  na Sikukuu alipokuwa akiishi Abdul Sykes na Nyerere alipoacha kazi ya
  ualimu Pugu, alikuja kukaa na Abdul katika nyumba hii hadi alipotafutiwa
  nyumba na Mzee John Rupia Magomeni Maduka Sita.

  Labda nikufahamishe jambo.

  Baba yangu alimuona Nyerere kwa mara ya kwanza hapo nyumbani kwa
  Abdul na Abdul akamwambia nini walikuwa wanataka kufanya na Nyerere
  katika TAA.

  Ninapokuambia kuwa hii ni historia ya wezee wangu unielewe.

  Katika barua ile Hamza Mwapachu anamwambia Abdul kuwa Nyerere
  atatufaa katika mipango ya kuipigania Tanganyika na akamueleza vipi amejuana
  na Nyerere.

  Hapa Abdul alikuwa kesharidhika kuwa Chief Kidaha Makwaia hatakuja TAA
  kama kiongozi waunde TANU na kudai uhuru.

  Sawa siasa za Kampala kama zilikuwapo ni historia yetu hatuwezi kuikataa lakini
  tuelezwe huko Kampala ilifanyika mipango gani ili tujue.

  Mimi hapa nimeeleza yale yaliyokuwa Dar es Salaam ambayo Abdul alihusika
  katika kuunda TANU kuanzia 1942 akiwa Burma na baada ya kurudi Burma.

  Mtaa huo huo wa Aggrey jirani na nyumba ya Abdul Sykes akiishi Tewa Said
  Tewa
  mmoja wa waasisi wa TANU kanieleza yote ya siku za mwanzo katika
  kuunda TANU na mpango ulioshindwa wa Chief Kidaha Makwaia.

  Lakini kabla ya mkutano wa mwaka wa TAA uliofanyika Arnautoglo tarehe 17 April
  1953 uliomuingiza Nyerere katika uongozi wa TAA ambao Nyerere alimshinda
  Abdul Sykes, Abdul na Ali Mwinyi Tambwe walikwenda Nansio kupata ushauri
  wa ''Kaka Mkubwa,'' Hamza Mwapachu kuhusu Abdul kumpisha Nyerere kwenye
  kiti cha urais wa TAA kisha waunde TANU.

  Haya hayakuandikwa katika historia rasmi.

  Haijapatapo hata siku moja kuwa nia yangu kuifuta historia ya Nyerere ila...ila nia
  yangu na ndiyo kilichonisukuma kunyanyua kalamu ni kuandika historia ya uhuru
  wa Tanganyika kama inavyostahili kuandikwa.

  Lakini simlazimishi mtu kuniamini.

  Anaweza kuendelea kuamini kuwa haya niliyoandika hayakutokea wala watu hawa
  hawajapatapo kuwepo katika TANU na historia ya kupigania uhuru wa Tanganyika.

  Mwisho nakueleza kitu na ningependa ukifahamu.

  Ingekuwa mimi kitabu changu nimeandika hayo unayosema kuhusu Nyerere kwa
  kejeli kwa kutaja, ''matembele,'' nk. nk. ningepuuzwa.

  Nimeingizwa katika mradi wa DAB Oxford na Harvard nikaalikwa Chuo Kikuu cha
  Northwestern University, Chicago ambao ni mabingwa duniani katika African History
  kwa kuwa nilichoandika kilikuwa kweli.

  Baada ya kuzungumza hapo Northwestern University nikaalikwa na Zentrum Moderner
  Oreint (ZMO) Berlin ambako nako nilizungumza haya ninayokufunulia hapa.

  Nafasi ikitokea In Shaa Allah nitakueleza huzuni iliyowagubika wenyeji wangu Berlin
  baada ya kunisikiliza.
   
 12. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #111
  May 20, 2017
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,250
  Likes Received: 4,692
  Trophy Points: 280
  Sheikh Mohamed Said.
  Nakusoma kwa ukaribu sana endelea kutoa darsa watu wengi wanafaidika kupitia kwako ilm ni bahari.
   
 13. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #112
  May 20, 2017
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,250
  Likes Received: 4,692
  Trophy Points: 280
  Nipo kipembeni hapa nimejibanza nakunywa kahawa na tende za Sharja huku nafuatilia mnakasha.
   
 14. m

  mkaruka ataja rinu JF-Expert Member

  #113
  May 20, 2017
  Joined: Aug 27, 2016
  Messages: 643
  Likes Received: 295
  Trophy Points: 80
  CCM haikutumia uharamia kupora viwanja vya mpira bali ilivimiliki tangu awali. Wakati ule wa chama kimoja cha siasa ambacho kilikuwa ni CCM,ilikuwa ni lazima kwa kila mtanzania aliyefikisha umri wa miaka 18 kujiunga na CCM kwa kusoma kwa kipindi cha miezi mitatu halafu anakabidhiwa kadi ya uwanachama wa CCM, zilipotokea shughuli za chama basi wanachama wote walipaswa kushiriki kuhakikisha zinafanikiwa,baada ya kuanzishwa vyaama vingi mwaka 1992, CCM ilibakiwa na mali zake na isingeweza kuzigawa maana ni mali zake pamoja na wanachama wake. Ni kama leo hii mtu awe Chadema,wafanikiwe kujenga ofisi ya chama na yeye akishiriki baada ya muda mtu huyo ajitoe kutoka Chadema,je atadai mgao wa ushiriki wake ktk ujenzi wa ofisi ya Chadema? Chadema wanapaswa kujitathimini kwa hilo lkn wakikalia oooh CCM walipora mali za umma watashindwa kufanya lolote maana mali hizo hazitarudishwa kamwe.
   
 15. m

  mkaruka ataja rinu JF-Expert Member

  #114
  May 20, 2017
  Joined: Aug 27, 2016
  Messages: 643
  Likes Received: 295
  Trophy Points: 80
  Huwa hakuna sheria ambayo ni ya hiari bali kila sheria ni lazima kuitekeleza,na mara zote sharia huwa ni kero kwa yule anayepaswa kuitekeleza
   
 16. M

  Makusudically JF-Expert Member

  #115
  May 20, 2017
  Joined: Feb 3, 2014
  Messages: 1,908
  Likes Received: 897
  Trophy Points: 280
  Kama unaona mali za CCM ni mali za Umma, si upeleke kiti kwenye majengo hayo ukidi kuwa umekwenda kukaa kwa vile na wewe ni sehemu ya umma?
   
 17. M

  Mbase1970 JF-Expert Member

  #116
  May 20, 2017
  Joined: Jun 11, 2015
  Messages: 3,706
  Likes Received: 2,327
  Trophy Points: 280
  Nimekuelewa Nguruvi umenielezea vizuri sana. Nina wasiwasi sana na hawa watunga vitabu hapa naona nao ni kama wanasiasa
  Mkuu nimekuuliza nijue nini machobishania na wewe unanipeleka kununua kitabu chako. Unataka kuwa kama Yericko Nyerere. Nimeshasoma majibu yako na ya Nguruvi na nimepata majibu kwanini mnabishana na ubishi wenu umeegemea wapi. Lakini nimeridhika zaidi na majibu ya Nguruvi3 kuliko yako.

  Badala ya kwenda kukinunua hicho kitabu chako niaangalia zaidi habari za huko nyuma.
   
 18. Mohamed Said

  Mohamed Said Verified User

  #117
  May 20, 2017
  Joined: Nov 2, 2008
  Messages: 11,231
  Likes Received: 6,397
  Trophy Points: 280
  Mbase1970,
  Ikiwa umeshapata jibu la swali lako hilo ni jambo zuri.

  Halikuwa jambo la wewe kununua kitabu ila kusoma
  kitabu.

  Mimi sibishani.

  Niko hapa kuandika na kueleza katika historia ya uhuru yale
  ambayo wengi hawakuwa wanayajua kabla ya kunisoma.
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...