Achilia mbali ruzuku na michango, CHADEMA ina vyanzo gani vya mapato? | Page 5 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Achilia mbali ruzuku na michango, CHADEMA ina vyanzo gani vya mapato?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Petro E. Mselewa, May 17, 2017.

 1. Petro E. Mselewa

  Petro E. Mselewa Verified User

  #1
  May 17, 2017
  Joined: Dec 27, 2012
  Messages: 7,665
  Likes Received: 10,711
  Trophy Points: 280
  Binafsi naamini kuwa chama cha siasa ni taasisi. Naamini hivyo pamoja na kutowahi maishani mwangu kujiunga na chama chochote cha siasa hapa Tanzania na kwingineko. Kama taasisi,chama hujiendesha kwa gharama.

  Kuna kuwalipa waajiriwa wa chama,kugharimia shughuli za kila siku za chama,kugharimia ziara na operesheni za kichama na kadhalika. Taasisi hujiendesha katika hali ghali. Chama,ili kupambana na changamoto za kiuendeshaji na kisiasa,kinapaswa kuwa na vyanzo vya mapato

  Kwa uelewa wangu,chama kama CCM kinamiliki mali mbalimbali kama majengo na viwanja vya mpira. Hizo pekee,ingawa kuna mengine,ni vyanzo vya mapato ya chama. Vipi kuhusu CHADEMA,kama chama kikuu cha upinzani nchini na taasisi muhimu kidemokrasia?

  Achilia mbali ruzuku kwa vyama vya siasa na michango ya wanachama,wafuasi,wapenzi,wakereketwa,wafurukutwa na wafia chama,CHADEMA ina vyanzo gani vingine vya mapato? Ina mipango gani ya kujiimarisha kiuchumi?

  Michango ya wanachama,hasa Wabunge wa CHADEMA,wakati mwingine ni mzigo na inakera. Ifike mahali CHADEMA iwe na vyanzo vyake vya mapato kama taasisi ili kujiimarisha na kuaminika. Ni kazi ya Bodi ya Wadhamini ya CHADEMA kusugua bongo

  Aione: Tumaini Makene ,Mmawia na wengineo
   
 2. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #81
  May 19, 2017
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 12,014
  Likes Received: 4,421
  Trophy Points: 280
  ndio ishakuwa vyao, ukilalamika haisaidii..akili ni kuja na mbadala na sio kulialia
   
 3. t

  treborx JF-Expert Member

  #82
  May 19, 2017
  Joined: Jul 11, 2015
  Messages: 4,498
  Likes Received: 2,061
  Trophy Points: 280
  Kwani ulitaka nao watumie fedha za ruzuku kuwekeza vitegauchumi? you bulling yourself...
   
 4. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #83
  May 19, 2017
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 12,014
  Likes Received: 4,421
  Trophy Points: 280
  haujui kutukana mkuu...unahitaji tuition, otherwise stay innocent as you are
   
 5. YEHODAYA

  YEHODAYA JF-Expert Member

  #84
  May 19, 2017
  Joined: Aug 9, 2015
  Messages: 11,430
  Likes Received: 10,836
  Trophy Points: 280
  Umeanza kuonyesha wazi Uchadema wako toka bosi wako chuo kikuu kabudi aondoke kabla hajaondoka hii ID ya verified user ulikuwa soft ila ukiitumia ile ingine kule ndiko ulikuwa hujifichi msimamo wako saa hii umejitoa waziwazi kuonyesha Your True color ile ID ingine naona huitumii sana umeiacha
   
 6. tanga kwetu

  tanga kwetu JF-Expert Member

  #85
  May 19, 2017
  Joined: May 12, 2010
  Messages: 2,169
  Likes Received: 1,138
  Trophy Points: 280
  if you're serious, njia sahihi ya kupata chanzo cha mapato ya chama cha kisiasa eg CHADEMA ni hapa JF? Hesabu za mwaka za kila chama hukaguliwa na wakaguzi wa ndani na nje (I am sure hili unalijua) na inawezekana hizo hesabu ziko-accessible na kama ni unaccessible basi naona sio sahihi. Nachojua mimi vyanzo vya mapato vya vyama vya siasa hapa nchini vinafanana tofauti ni depth and width ya hivyo vyanzo. Navyo ni kama vile ada za wanachama, michango ya hiari ya wanachama na wadau wengine, misaada ya wahisani/marafiki wa chama wa ndani na nje ya nchi na faida katika vitega uchumi vyao. CCM (kama chama-dola) kwa upande wa michango ya "hiari" kutoka kwa wanachama/wadau wako vizuri maana huwa naona wanapopitisha bakuli hapa mkoani kwa wafanyabiashara kwa gia ya mchango wa "hiari" na ole yake atakayekataa LIKEWISE ole yake mfanyabiashara atakayekuwa anachangiachangia chama cha upinzani. Hutokea hata ofisi/taasisi/idara ya serikali/umma kuichangia kwa kificho au waziwazi shughuli ya CCM. In conclusion, kwa mtazamo wangu vyama vya siasa vya upinzani vinajitahidi sana kwenye ku-solicit fund kwa sababu playground haiko level sawa. Binafsi, nawapongeza kufanikisha shughuli zao katika "mminyo" huu ambao wenzao CCM wanapeta tuu hawajui shida yoyote
   
 7. YEHODAYA

  YEHODAYA JF-Expert Member

  #86
  May 19, 2017
  Joined: Aug 9, 2015
  Messages: 11,430
  Likes Received: 10,836
  Trophy Points: 280
  Ninachosema ni kuwa wakati wa chama kimoja CCM ilikuwa ikipata ruzuku na kuchangiwa na wanachama ikaamua kutumia kuwekeza vitega uchumi na inaendelea kufanya hivyo vyama vingine ikiwemo chadema nao wanapata ruzuku na kuchangiwa na wanachama na Wafadhili hawawekezi wanazila zote.Ndio maana wamewafanya wabunge wao ndio miradi ya kukipa pesa chama. Kupanga ni kuchagua chama kikipata ruzuku kinatakiwa kizitafune zote au kiwekeze ni kuchagua. Nimaloweza kusema viongozi wa chadema hawana uchungu na chama hata kikifa kwao sawa tu mradi wamekula ruzuku ndio maana hawana mradi hata wa kuuza bagia.
   
 8. t

  treborx JF-Expert Member

  #87
  May 19, 2017
  Joined: Jul 11, 2015
  Messages: 4,498
  Likes Received: 2,061
  Trophy Points: 280
  Mkuu, be careful and do yourself a very good justice by stop telling lies. Kwamba CCM iliwekeza kutokana na michango ya wanachama wake???? are you serious? Yaani kiwanja cha Mpira cha Kirumba Mwanza kilijengwa kwa michango ya wanachama wa CCM??? You can't be this moron....
   
 9. YEHODAYA

  YEHODAYA JF-Expert Member

  #88
  May 19, 2017
  Joined: Aug 9, 2015
  Messages: 11,430
  Likes Received: 10,836
  Trophy Points: 280
  Kilijengwa kwa michango ya wanachama Na wapenzi wa CCM Wa Ndani na nje ya nchi ikiwemo michango Ya chama cha kikomunisti cha China na ruzuku. Unadhani kilijengwa na chadema?
   
 10. t

  treborx JF-Expert Member

  #89
  May 19, 2017
  Joined: Jul 11, 2015
  Messages: 4,498
  Likes Received: 2,061
  Trophy Points: 280
  You are so pathetic...
   
 11. G

  Gizz New Member

  #90
  May 19, 2017
  Joined: Apr 4, 2017
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Rambirambi
   
 12. M

  Mgango JF-Expert Member

  #91
  May 19, 2017
  Joined: Oct 27, 2016
  Messages: 2,349
  Likes Received: 1,038
  Trophy Points: 280
  Apart from kutaifisha hivyo viwanja wanapata hata za misiba. Wewe jiulize lini k utakuwa na msiba mwingine wa ki taifa au utatokea mkoa gani mwingine mkusanye michango mingine. Ya ngoswe mwachie ngoswe mwenyewe
   
 13. M

  Mkwaruu JF-Expert Member

  #92
  May 19, 2017
  Joined: Mar 13, 2017
  Messages: 2,490
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  Hakina haja vyanzo vya kuzulumu maeneo ya wazi na Viwanja vilivyojengwa na wananchi wote pasipo itikadi
   
 14. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #93
  May 19, 2017
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,310
  Likes Received: 7,524
  Trophy Points: 280
  Mohamed, kidogo umerudisha moyo na kauli zako zimekuwa njema tunaongea
  Sisi wengine adabu hufunzwa tangu funda la kwanza la maziwa ya mama, ni sehemu ya utamaduni

  Hili la Kaptula uliwahi kuleta picha ukishadidi. Liliamsha hisia kwa baadhi kutokana na ushabiki na si vazi.

  Tulijua wakati wa ukoloni ilikuwa ni fashion. lakini wewe ulichomeka katika kuhakikisha unamdhalilisha Nyerere ili Abdul apande. Tuliache kwasababu kuliongelea wengi watajifunza mabaya

  Pili, yapo maandishi tukiyavuta hapa JF yatakuvunjia heshima.
  Umesema Dosa alifilisika kutokana na rasilimali zake kutumika katika kuhudumia chama.

  Chonde tuliache, ukibisha tutavuta uzi na kukuacha bila heshma, ushanfahamu

  Tatu, kuna hili la Mshume Kiyate unakwepa kulijibu.
  Mimi sina uhusiano na ukoo wa Nyerere, maisha yalinifikisha maeneo nilijikuta na marafiki mbali mbali.

  Kwa mfano, viwanja sitini Iafkara ni kwangu, Nanjoka Tunduru ni kwangu.
  Nyamuswa ni kwangu, Ikizu nikifika ni nyumbani hata Butiama na Kyabakari

  Naulizwa na watu sijui ni wajuu ,vitukuu au vijana sijui ni marafiki kuhusu hili la Mshume

  Katika maandiko umesema Mshume alikutana na Nyerere pale Faya akampa Sh 200 wakati nyerere anakwenda Sokoni, ndiyo maana tunakuuliza, Unasimama nalo au umebadili kabla ya toleo jipya?

  Kule kwetu Muheza, ukimpa mtu kipande cha nguru basi ni wewe na kauli yako.
  Wazee wetu wakisema ukitoa kwa mkono wa kulia ikiwezekana wa kushoto usione.

  Leo sh 200 zinaandikwa katika makabrasha na kusmbazwa katika Africa Bibliography, Havard n.k. kwingine zikieleza jinsi Mwalimu alivyokuwa anahanja kwenda sokoni, akakutana na Kiyate aliyempa sh 20 zikisemwa nyingi wakati huo akanunue Ng'onda, vitoga, matembele, pishi ya mchele na kibaba cha unga

  Aaah! Mohamed, tukisoma hayo ya sh 200 ambayo hutaki kuyazungumzia kwasababu unajua ni dhalili uliyoandika dhidi ya Mwalimu unadhani wajukuu wa Mwl na familia yake itapenda kuona chama cha siasa kikipokea misaada binafsi ya mapesa tena!

  Sihitaji hadhithi za flani flani, nipo katika point.

  Mohamed Said Salum , eleza jamvi na umma
  Je si kweli Msume alitoa sh 200 kumpa Nyerere akanunue mboga wakati anachanja mbuga kwenda sokoni ?
   
 15. YEHODAYA

  YEHODAYA JF-Expert Member

  #94
  May 19, 2017
  Joined: Aug 9, 2015
  Messages: 11,430
  Likes Received: 10,836
  Trophy Points: 280
  OK tukujibu kwa data mzee sabodo aliwapa mabilioni mosi wajenge chuo cha siasa cha chadema pili wajenge visima maeneo mbalimbali pamoja na mzee wa watu kuziwekea masharti walizila zote hakuna hata ardhi tu ya chuo feki ambayo wangemzuga mzee wa watu na Hanna hata kisima kimoja walichochimba. Nakuhakikishia uchaguzi 2020 pesa Ya lowasa na matajiri wengine wa ndani na nje Hawatawachangia walikuwa hawajui kuwa chadema kuna mchwa.2020 nyie wapiga kelele tutaona mtatoa pesa wapi mtakoma
   
 16. Ronal Reagan

  Ronal Reagan JF-Expert Member

  #95
  May 19, 2017
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,838
  Likes Received: 1,546
  Trophy Points: 280
  1. Kwanza nikiri nimelisoma bandiko lako na kuona haja ya kuchangia kwa sehemu.

  2. Pili niweke bayana kuwa mimi sio mwanachama wa CHADEMA au chama chohote cha siasa Tanzania.

  3. Tatu nikiri wazi kuwa mimi ni wa mrengo wa upinzani, naipinga na kuichukia CCM sio kwa rangi yake bali kwa matendo yake maovu na mafu.

  4. Haihitiajiki mamlaka ya mahakama wala chombo chochote kutuambia tuliokuwepo hai wakati ule (mimi nilishiriki kazi ktk baadhi ya hizo ulizozitaja kama mali za CCM ile miaka ya 70, wengi tuliambiwa ni za jamii/umma na sio za chama) kuwa mali nyingi za CCM zilikuwa za Serikali na/au za wananchi lakini zikaporwa na kumilikishwa CCM.

  5. Kuthibitisha kuwa CCM na ufisadi na rushwa ni damu moja, kwa nini ufisadi na rushwa vimeendelea kukua na kuongezeka nchini toka kuanzishwa kwa CCM mwaka 1977?

  6. Asilimia zaidi ya 90 ya wote waliowahi kufikishwa kwenye Mahakama ya Sheria kwa rushwa na ubadhirifu wa mali ya umma ni wana CCM. Kwa hiyo kujilimbikizia mali ya dhuluma na kisha kujitapa ni tabia/asili yao ambayo ambayo wapumbavu tu ndio wataisifia.

  7. Mwisho, hiyo CCM na hizo "mali na vyanzo vya mapato" vimekuwa na tija gani mtambuka kwa Taifa letu? Kwa nini wawe na huo (unaodhaniwa ni) ukwasi halafu kila siku waibe na kufisadi mali za umma/wananchi ????
   
 17. YEHODAYA

  YEHODAYA JF-Expert Member

  #96
  May 19, 2017
  Joined: Aug 9, 2015
  Messages: 11,430
  Likes Received: 10,836
  Trophy Points: 280
  Slaa pia alikuwa chanzo chao kikubwa cha mapato kutoka kwa wazungu Ya pesa za kigeni wamemtimua kasepa Na matajiri wake Wafadhili wa ulaya na marekani na canada sasa hivi kutwa wanakamua wabunge. Nakuhakikishia usione lowasa yuko Kimya He is not ready kudish out Money kama alivyofanya uchaguzi uliopita .2020 kila mgombea chadema atabeba furushi lake ndio Maana hata ofisi hazijengwi wala vitega uchumi wanajua hii ruzuku Kubwa yaweza kuwa ya mwisho mwaka 2020 chadema yaweza dorora hivi wanachukua chao mapema
   
 18. YEHODAYA

  YEHODAYA JF-Expert Member

  #97
  May 19, 2017
  Joined: Aug 9, 2015
  Messages: 11,430
  Likes Received: 10,836
  Trophy Points: 280
  Chadema chanzo kikuu Kingine kilikuwa Lowasa mkiimba kidogo lowasa eeee lowasa wee mnakatiwa maburungutu yale hayarudi tena.anzeni kujiandaa kisaikolojia sasa hivi kakomaa hasikilizi nyimbo wala sanaa za kudeki barabara
   
 19. Mohamed Said

  Mohamed Said Verified User

  #98
  May 19, 2017
  Joined: Nov 2, 2008
  Messages: 11,231
  Likes Received: 6,397
  Trophy Points: 280
  Nguruvi3,
  Umechomwa moyo na hili la ''kaptula,'' na nimekuambia mimi sijapatapo
  kuandika kuhusu kaptula lakini umeshikilia kuwa nimeandika.

  Uamuzi wa mvutano huu ni wewe kuyaweka hayo maneno niliyoandika kuhusu
  ''kaptula,'' na wala sipatapo kuweka picha inayohusu, ''kaptula,'' ikiwa unao
  ushahidi wa hayo yote tafadhali uweke hapa sote tuushuhudie.

  Hii mosi.
  Pili umenifurahisha kitu kimoja.

  Unakuja na vitisho.
  Unanitisha kuwa utafanya hivi ikiwa sitofanya hiki na hiki.

  Dossa alifilisika katika siasa.
  Sasa timiza hivyo vitisho vyako.

  Sijaogopa kueleza juu ya urafiki wa Mzee Mshume na Nyerere, nilichosema
  ni kuwa kisa kizima nimekieleza katika kitabu cha Abdul Sykes.

  Kukudhihirishia kuwa sijaogopa kueleza kisa kile sasa nakiweka hapo chini kisa
  chenyewe:

  [​IMG]

  Kama nilivyokwisha kusema awali historia hii ya wazee wetu inakuchoma roho
  na ndiyo haya maneno ya ''kuhanja,'' ''DAB, Oxford na Harvard.''

  Umewasahau Cambridge Journal of African History.
  Na huko niko pia.

  Hii inaweza kusabishwa na kitu kimoja tu.
  Hasad.
   
 20. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #99
  May 19, 2017
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,310
  Likes Received: 7,524
  Trophy Points: 280
  Mzee Said hivi unakumbuka ulileta picha ya wazee wetu na wako wakiwa pamoja na Nyerere. Picha ile ilileta sintofahamu kwasababu lengo lilikuwa kuonyesha kaptula.
  Ni miaka mingi kiasi nadhani ilikuwa kati ya 2010-2011.

  Tutafunua makabrasha kama hayajaliwa na panya, tulia tu

  Hili la Mshume sasa umeliweka wazi kabisa na nashukuru sana.
  Ulikuwa hutaki ukijua kufanya hivyo si jambo la kiungwana.

  Well, wajukuu wa Mwalimu wanasoma babu yao alivyochacha kiasi cha kwenda sokoni bila kujua ana kitu gani mfukoni, basically alikuwa anahanja hanja! yarabi!

  Historia ya wazee wetu na wako hainichomi moyo inanipa faraja na ninawashukuru sana
  Kinachosumbua ni jinsi ambavyo pengine wasingependa baadhi ya mambo yaandikwe

  Katika jitihada yapo mengi wamefanya na sijui la ng'onda , matembele na vibaba vya unga na kuhanja hanja wangalipenda yaelezwe kama sehemu ya mchango wao zaidi ya utu wao.

  Kilichomsukuma Mshume ni utu na ubinadamu wake, kwa namna flani utu huo sasa unaandikwa katika mithili ya kuhalalisha maandiko ya kihistoria.

  Sijui kama ndilo lilikuwa lengo la Mzee Kiyate zaidi ya kusaidi shibe kwa familia

  Hili la sokoni na kuhanja hanja kwa mwl kwa njaa nadhani linasomeka vema katika nukuu yako

  Tuwaachie wasomaji waamue kwa fikra zao kama ilikuwa ni lazima kufanya hivyo

  Hili la Dossa nalo limekwisha kwasababu umekiri kuwa alifilisika katika siasa.

  Ndio msingi wa mada isifike mahali watu wakajitolea katika vyama na kubaki na lawama
  Wanachama wachangie vyama kwa ridhaa na mapenzi yao wakiongozwa na utu kama wa Dossa

  Kuna hili la sherehe za miaka 50. Bin Said umesema hakuna aliyejua aseme nini.

  Kwakweli zaidi ya shukrani kwa wazee wetu na wako, hakukuwa na la ziada
  Pengine lingesemwa jambo Nyerere angetamalaki na vema hawakusema

  Historia ya nchi hii itaandikwa kwa kila kalamu, jina la Nyerere halikwepeki

  Jitihada za kulinganisha utu hazisaidii, mchango wa kila mmoja ulikuwa muhimu wakti huo
  Iwe alitoa matembele, nguruka, ng'onda , kibaba n.k. yote ni michango

  Nyerere kapumzika, kila siku jina lake at least linatwajwa kama si kusomwa mahali

  Hakuna wa kumsemea, jina linajisemea lenyewe na maandiko yanajibu hoja kutoka alikopumzika
   
 21. Mohamed Said

  Mohamed Said Verified User

  #100
  May 19, 2017
  Joined: Nov 2, 2008
  Messages: 11,231
  Likes Received: 6,397
  Trophy Points: 280
  Nguruvi3,
  Unakusudia hii piacha ya waasisi wa TANU hapo chini:

  [​IMG]
  Ndiyo leo nasikia kuwa picha hii inadhalilisha.
  Kabla ya leo sikupatapo kujua hili.

  Ikiwa wewe unaona hii picha inadhalilisha napenda nikuambia kuwa ukiingia CCM Dodoma
  hii picha ipo tena imekuzwa ipo pale CCM Dodoma kubwa sana.

  Je umeshawapa indhar CCM kuwa hiyo picha inadhalilisha?
  Ati nimekataa kuzungumza habari za Mshume Kiyate.

  Mzee Kiyate mimi ni shujaa wangu na nimemwandika kwingi sana.
  Soma hii:
  ''Ukitaka watu wenye noti zisizo na kikomo utamkuta John Rupia, ‘’The Bank,’’ Waziri Dossa Aziz, Abdul na Ally Sykes kisha wazee wao wa mjini Mwinjuma Mwinyikambi, Max Mbwana na Mshume Kiyate wazee karim hujapatapo kuona.''

  [​IMG]
  Kulia: Mshume Kiyate, Julius Nyerere, Max Mbwana na Mwinjuma Mwinyikambi

  Chuo Cha Kivukoni waliandika historia ya TANU wakaliacha jina la Abdul Sykes nadhani
  sote tumeyaona matokeo yake.

  Kalamu nyingi zitaandika habari za Nyerere katika uhuru wa Tanganyika lakini hawataweza
  kulikwepa jina la Kleist Sykes na watoto wake.

  Wakiigusa TANU lazima majina haya yatakuwapo.

  Abdul alifanyiwa njama na jina lake likafutwa katika historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika.
  Leo Abdul tanamzungumza yeye akiwa kaburini.
  Mohamed Said: KUTOKA JF: AFRICA EVENTS LILIPOCHAPA KUMBUKUMBU YA ABDUL SYKES 1988

  Historia yake ndiye hii hapa tunaijadili na inasomeshwa vyuo vingi Ulaya na Marekani.
  Mohamed Said: TOWN CLERK MZUNGU ALIVYOKERWA NA KADI ZA TANU KUUZWA OFISINI KWA MARKET MASTER ABDUL SYKES, 1954
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...