Achilia mbali ruzuku na michango, CHADEMA ina vyanzo gani vya mapato? | Page 4 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Achilia mbali ruzuku na michango, CHADEMA ina vyanzo gani vya mapato?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Petro E. Mselewa, May 17, 2017.

 1. Petro E. Mselewa

  Petro E. Mselewa Verified User

  #1
  May 17, 2017
  Joined: Dec 27, 2012
  Messages: 7,588
  Likes Received: 10,467
  Trophy Points: 280
  Binafsi naamini kuwa chama cha siasa ni taasisi. Naamini hivyo pamoja na kutowahi maishani mwangu kujiunga na chama chochote cha siasa hapa Tanzania na kwingineko. Kama taasisi,chama hujiendesha kwa gharama.

  Kuna kuwalipa waajiriwa wa chama,kugharimia shughuli za kila siku za chama,kugharimia ziara na operesheni za kichama na kadhalika. Taasisi hujiendesha katika hali ghali. Chama,ili kupambana na changamoto za kiuendeshaji na kisiasa,kinapaswa kuwa na vyanzo vya mapato

  Kwa uelewa wangu,chama kama CCM kinamiliki mali mbalimbali kama majengo na viwanja vya mpira. Hizo pekee,ingawa kuna mengine,ni vyanzo vya mapato ya chama. Vipi kuhusu CHADEMA,kama chama kikuu cha upinzani nchini na taasisi muhimu kidemokrasia?

  Achilia mbali ruzuku kwa vyama vya siasa na michango ya wanachama,wafuasi,wapenzi,wakereketwa,wafurukutwa na wafia chama,CHADEMA ina vyanzo gani vingine vya mapato? Ina mipango gani ya kujiimarisha kiuchumi?

  Michango ya wanachama,hasa Wabunge wa CHADEMA,wakati mwingine ni mzigo na inakera. Ifike mahali CHADEMA iwe na vyanzo vyake vya mapato kama taasisi ili kujiimarisha na kuaminika. Ni kazi ya Bodi ya Wadhamini ya CHADEMA kusugua bongo

  Aione: Tumaini Makene ,Mmawia na wengineo
   
 2. Mwana Mtoka Pabaya

  Mwana Mtoka Pabaya JF-Expert Member

  #61
  May 17, 2017
  Joined: Apr 22, 2012
  Messages: 12,235
  Likes Received: 8,655
  Trophy Points: 280
  Mkuu, ni upuuzi kujifanya kuwa huelewi kuwa hizi zilikuwa mali za umma na CCM imezihodhi kwa hila. Sasa sijui una maana gani katika ulinganisho wako
   
 3. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #62
  May 17, 2017
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 44,463
  Likes Received: 14,101
  Trophy Points: 280
  Chanzo cha mapato ni Lowasa....
   
 4. YEHODAYA

  YEHODAYA JF-Expert Member

  #63
  May 17, 2017
  Joined: Aug 9, 2015
  Messages: 11,112
  Likes Received: 10,447
  Trophy Points: 280
  Wewe mbumbuMbu NGO yoyote iwe chama au Dini au yoyote kuwa sustainable lazima iwe Na mapato sustainable Ya kufinance shuguli zake ambayo ni certain ndio maana kanisa mfano katoliki lina miradi lukuki ya Shule , hospital nk Na CCM vilevile huwezi tegemea wanachama tu waweza Hama unataka chama kife? Ruzuku inategemea wabunge Na madiwani uliopata Na makusanyo ya kodi Ya serikali. vikiwa Low unataka chama kife? Argument yako sio Ya kisomi iko too low ni ya mtu anbaye anaegemea eneo fulani bila kushirikisha akili yake iwe ya kusoma au kuzaliwa. Naona una unafiki mkubwa kwenye nafsi yako baada ya kushambuliwa umeamua kuwa mnafiki
   
 5. kilambalambila

  kilambalambila JF-Expert Member

  #64
  May 17, 2017
  Joined: Nov 16, 2013
  Messages: 7,404
  Likes Received: 3,498
  Trophy Points: 280
  Baba Lowasa ni chanzo
   
 6. t

  treborx JF-Expert Member

  #65
  May 18, 2017
  Joined: Jul 11, 2015
  Messages: 4,442
  Likes Received: 2,031
  Trophy Points: 280
  Kweli... Kwa hiyo wakijenga majengo makubwa inakuwaje? What is your point?? au ulitaka kusema wakijenga majengo yao makubwa watarudisha yale ya wananchi waliyojimilikisha???? unasema siyo kweli nilichoandika hapo awali, but the next you write BS..
   
 7. m

  mambio JF-Expert Member

  #66
  May 18, 2017
  Joined: Mar 4, 2017
  Messages: 350
  Likes Received: 127
  Trophy Points: 60
  Hayo majengo si ndivyo vitega uchumi mkuu? Kwani wewe unatafsirije neno 'vitegauchumi?
   
 8. Mohamed Said

  Mohamed Said Verified User

  #67
  May 18, 2017
  Joined: Nov 2, 2008
  Messages: 11,212
  Likes Received: 6,362
  Trophy Points: 280
  Nguruvi3,
  Mimi ndiye niliye ueleza uzalendo wa Mshume Kiyate na hakuna popote
  nilipoandika kwa masimango.

  La kama umesoma mahali nimesema kuwa , ''Nyerere hakuwa na mboga,''
  lete hapa watu wote washuhudie.

  Hebu kwa wale wasiomjua Mzee Mshume wasome hapo chini:
  Mohamed Said: KITENDAWILI KATIKA KUTUNUKU MAJINA YA MITAA YA DAR ES SALAAM KWA WAPIGANIA UHURU WA TANGANYIKA

  MTAA WA MSHUME KIYATE ZAMANI MTAA WA TANDAMTI

  ''Ukweli ni kuwa Mtaa wa Mshute Kiyate haupo kwa sababu wahusika wamekataa kubadili kibao cha jina sasa yapata zaidi ya miaka 20. Kitwana Kondo alipokuwa Meya wa Jiji la Dar es Salaam ndiye aliyefanya mabadiliko ya majina ya mitaa kuwaenzi wazalendo waliopigania uhuru wa Tanganyika kwa kuipa majna yao ile mitaa waliokuwa wakiishi. Hivyo ndivyo Mtaa wa Kipata ujabadilishwa na kuitwa Mtaa wa Kleist Sykes, Mtaa wa Somali ukaitwa Omari Londo, Mtaa wa Aggrey ukaitwa Max Mbwana, Pugu Road ikaitwa Barabara ya Mwalimu Nyerere, Bi. Tatu binti Mzee akapata mtaa Ilala na Mtaa wa Tandamti ukabadilishwa jina na kuitwa Mtaa wa Mshume Kiyate. Lakini palizuka malalamiko kuwa kilichomsukuka Kitwana Kondo kubadili majina ni hisia za udini. Hii ni baada ya kuonekana wazalendo wengi waliopewa majina ya mitaa ni Waislam. Magazeti yakahoji ni michango gani wazalendo hawa walitoa? Kitwana Kondo katika mahojiano aliyofanya na marehemu Sarah Dumba wa Radio Tanzania Dar es Salaam (RTD) alijibu kwa kusema, ''Ikiwa hamjui michango ya watu hawa ulizeni mtaelezwa.''

  [​IMG]
  Waliosimama wa pili kulia ndiye Mzee Mshume Kiyate
   
 9. igp

  igp JF-Expert Member

  #68
  May 18, 2017
  Joined: Feb 16, 2015
  Messages: 840
  Likes Received: 393
  Trophy Points: 80
  Wewe unasema huna chama kwani ulitoka lini bavicha mkoa wa pwani.
   
 10. vitalis msungwite

  vitalis msungwite JF-Expert Member

  #69
  May 18, 2017
  Joined: May 11, 2014
  Messages: 831
  Likes Received: 895
  Trophy Points: 180
  Kuuza tisheti za matukio mbalimbali, mfano free Lema, lema for Justice, njaa, ukuta, free Ben, m4c n.k ila Mara nyingi mapato huwa ni ya watu binafsi.
   
 11. Petro E. Mselewa

  Petro E. Mselewa Verified User

  #70
  May 18, 2017
  Joined: Dec 27, 2012
  Messages: 7,588
  Likes Received: 10,467
  Trophy Points: 280
  Niliingia lini?
   
 12. Bowie

  Bowie JF-Expert Member

  #71
  May 18, 2017
  Joined: Sep 17, 2016
  Messages: 3,410
  Likes Received: 4,541
  Trophy Points: 280
  Kabla ya kuongelea michango wakupe breakdown ya matumizi ya Ruzuku.
   
 13. Zawadi B Lupelo

  Zawadi B Lupelo JF-Expert Member

  #72
  May 18, 2017
  Joined: Jul 19, 2015
  Messages: 2,065
  Likes Received: 2,799
  Trophy Points: 280
  Tangu Mzee wako Kabudi ateuliwe umebadilika sana
   
 14. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #73
  May 18, 2017
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,280
  Likes Received: 7,465
  Trophy Points: 280
  Mohamed, tulia punguza jazba umekuja juu sana

  Tulizana tuongee muungwana, kule Bonde i tukisema wawili wakiongea haliharibiki jambo.

  Mohamed ,Mzee Kiyate hakukutana na Nyerere wakati anaenda sokoni na kumpa sh 200 za wakati huo?

  Pili, mjadala uliopo ni kuhusu michango ya vyama kama alivyosema JokaKuu

  Nilichosema, michango yaweza kuwa na ni njema, katika ujenzi wa vyama inaweza kuwa na matatizo siku za mbeleni. Tumeona mifano mingi siku za nyuma . Kama hatujifunzi itakuwa kosa

  Wazee wetu walipigania uhuru wawe huru na watuachie nchi huru. Hilo ni jema na mwenyezi awahesabie

  Kinachotokea ni kama haya ya flani alitoa pesa, flani kitoweo, flani makazi, mwingine alimshonea suruali kiongozi aliyekuwa na kaptura. Mwingine, huyu bw kama hakutoa ng'onda hali ilikuwa tata n.k.

  Kwamba michango ya watu kiutu haitiliwi maana zaidi ya ile ya kitu

  Katika hilo nikamalizia kwa kusema vyama vijichangie na si kufanya biashara au kutegemea watu
  Tunayo mifano, tusifanye makosa ambayo tunajifunza tayari. Ndiyo hoja yangu

  Nimekosea wapi kufanya reference ya kauli za mwanazuoni?
   
 15. Mohamed Said

  Mohamed Said Verified User

  #74
  May 18, 2017
  Joined: Nov 2, 2008
  Messages: 11,212
  Likes Received: 6,362
  Trophy Points: 280
  Nguruvi3,
  Mwenye wahka ni wewe ujae kwa ukali na kutaka kunifunga mdomo.
  Fumbo mfumbie mjinga...

  Pitia hiyo post yako na zitazame hizo kejeli za ''kaptura,'' ''ng'onda,'' nk.

  Najua inakuchoma historia ya wazee wangu lakini tufanyeje na hivyo
  ndivyo ilivyokuwa?

  [​IMG]

  Picha hii Mzee Mshume na Mwalimu Nyerere 1964 Mzee Mshume
  alipokwenda pamoja na wazee wengine kumfariji Mwalimu Nyerere
  baada ya maasi ya Tanganyika Rifles tarehe 20 Januari 1964.

  Ingia hapo chini:
  THOMAS SOUDT PLANTAN RAIS WA MWISHO WA TAA ALIYEKABIDHI CHAMA KWA VIJANA WADAI UHURU WA TANGANYIKA
   
 16. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #75
  May 18, 2017
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,280
  Likes Received: 7,465
  Trophy Points: 280
  Bin Said taratibu.
  Nilisema mwanzo wahka hautatuweka kikao. Turudishe nyoyo nyuma, tuongee kwa stara

  Nimeuliza , si kweli Mshume alitoa Sh 200 kumpa Nyerere wakati anaelekea sokoni pale mtaa wa Faya?

  Sokoni kuna mengi, huenda alikwenda kupata kibaba cha unga, mboga na kadha wa kadha

  Mimi historia ya wzee wetu inanisisimua sana hasa utu wao.
  Nikisoma habar zao kwakweli nafarajika

  Ninatatizika kidogo wakati utu wao unapokuwa pembeni zaidi ya kitu chao.

  Mzee Dosa mchango wake ni mkubwa. Kwamba, alifisilika kwasababu ya! inasumbua
  Mzee Kiyate ndio huyo wa Rufiji na Baiskeli. Kwamba, alimpa mwenza senti za kitoweo,it's toubling
  Halafu picha za wazee wetu si zile za harakati bali wakiwa na kaptura, it's unfortunate

  A a! tusirejee huko, vyama vijitafutie michango ili siku za mbele tuongelee utu
  Hatuhitaji tena kusoma na kuangalia picha za nyakati hizi flani akiwa na makobazi
   
 17. Mohamed Said

  Mohamed Said Verified User

  #76
  May 18, 2017
  Joined: Nov 2, 2008
  Messages: 11,212
  Likes Received: 6,362
  Trophy Points: 280
  Nguruvi3,
  Siwezi kujipigia zumari mimi mwenyewe...lakini sina tabia ya shari.
  Pitia maandiko yangu hilo utatambua.

  Wewe si wa kunifunza mimi adabu.

  Aliyekuwa anapanda baiskeli kueneza TANU Rufiji si Mshume Kiyate
  ni Said Chamwenyewe.

  Hakika mtasumbuka kwa mengi.

  1968 alipokufa Abdul Sykes walisumbuka pale Mhariri wa Tanganyika
  Standard, Brendon Grimshaw alipoandika taazia na kusema nchi ina
  deni kwa Abdul Sykes kwa kuunda TANU.

  Pale Lumumba Street walisumbuka kama unavyosumbuka wewe hivi sasa.

  Na walipotoa medali ya Mwenge wa Uhuru kumtunuku Abdul na mdogo
  wake Ally katika kuadhimisha miaka 50 ya uhuru walisumbuka hawakujua
  waseme kitu gani kuhusu mchango wa hawa ndugu wawili.

  Naam.
  Mtasumbuka.
   
 18. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #77
  May 19, 2017
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,280
  Likes Received: 7,465
  Trophy Points: 280
  Ahlan Mohamed. Mbona unazidi kufuka muungwana? Hakuna mahali nilipoandika kukufunza adabu na wala sitajaribu. Kwetu tumefunzwa kuongea katika hadhra.

  Nitakuvunjia heshima kwa kuanzia wapi wewe mzee wa Mjini! Nikija Dar nyakati hizo nilikuwa na kaptura , Nyerere peke yake aliweza, seuse ngulumbili mimi. Turudi katika mjadala wala usiwe na wahaka heshima ya mtu haivunjwi

  Mzee Said, swali langu ni moja ambalo huenda limetibua nyongo lakini sikulipata kwingine ni katika maandiko yako
  Hivi si kweli Mzee Kiyate alimpa Nyerere sh 200 za Mboga wakati akienda sokoni?

  Hili la mboga lisikutie simanzi, mboga yaweza kuwa msemo ikimaanisha pishi za mchele, kipande cha Ng'onda au fungu la matembele. Sh 200 nyakati hizo nyingi, je, si kweli kwa mujibu wa maandiko yako Kiyate alimpa Mwalimu?

  Pili, Mohamed si uliwahi kutueleza hata fundi cherahani wa nguo za Mwalimu? Au tuvute uzi
  Picha ya Mwalimu akiwa na kaptura si ilitoka katika nyaraka zako zilizopo katika kavazi la Mwalimu?

  Tatu, Mohamed hujawahi kusema Dosa alifilisika kwasababu ya shughuli za Chama?

  Nne, Mohamed, hujawahi kuandika mahali ukasema Kiyate aligawa kadi Rufiji?

  Mbona ukiulizwa wawa mbogo, maneno useme mwanazuoni, tukifanya reference inakuwa muhali, tukiuliza inakuwa tafrani.

  Tujadiliane taratibu tukirudisha nyoyo zetu na kuzungumza kwa mila na desturi zetu sisi wa Pwani na Magila
   
 19. Petro E. Mselewa

  Petro E. Mselewa Verified User

  #78
  May 19, 2017
  Joined: Dec 27, 2012
  Messages: 7,588
  Likes Received: 10,467
  Trophy Points: 280
  Nimekuwaje Mkuu?
   
 20. Mohamed Said

  Mohamed Said Verified User

  #79
  May 19, 2017
  Joined: Nov 2, 2008
  Messages: 11,212
  Likes Received: 6,362
  Trophy Points: 280
  Nguruvi3,
  Sijui kipi kimekufanya uje na staili hii ya kujifanya mpole kwangu na kujitahidi
  kuaminisha wasomaji kuwa mimi nimegadhibika.

  Sidhani kama kwa mtindo huu utafika mbali na mimi.

  Mimi siwezi kuandika kuhusu ''kaptula,'' na maandishi yangu yangekuwa katika
  mtindo huo nisingekuwa hapa nilipo katika kuandika historia ya Tanganyika.

  Ningedharaulika miaka mingi.
  Labda nikufahamishe kitu.

  Market Master Abdul Sykes sare yake ya kazi pale Kariakoo ilikuwa kaptula
  na shati jeupe.

  Baba yangu akifanya kazi siku hizo ikiitwa ''Exchange,'' Idara ya Simu Posta ya
  kikoloni nikimuona akivaa kaptula na ''stockings.''

  Wazee wengi hapa Dar es Salaam katika 1950 sisi wadogo tukiwaona na kivazi
  hicho na kwa hakika kilikuwa kivazi cha wasomi.

  Hivi vijembe vyako vya, ''kaptula,'' mtupie mtu mwingine mimi sihusiki navyo.

  Ikiwa umekuta uandishi wa ''kaptula,'' katika yale niliyoandika basi lete hapa
  tusome tumalize ubishi huu.

  Uhusiano wa Mshume Kiyate na Mwalimu Nyerere nimeueleza kwa kirefu
  katika kitabu cha Abdul Sykes yeyote atakae anaweza akasoma.

  Wala simlazimishi mtu kuamini, si hayo ya Kiyate Mshume hata kuwa Abdul
  kadi yake ya TANU ni no. 3 na mdogo wake Ally ni na. 2 na Nyerere na. 1 si
  lazima iaminike.

  Huna haja ya kuamini.
  Dossa nimesema amefilisika katika siasa.

  Katika Kavazi la Mwalimu Nyerere hakuna nyaraka zangu hizo kama umeziona
  ni nyaraka ambazo mimi nimepata katika Nyaraka za Sykes hakuna chochote
  katika hizo nyaraka zinazohusu ''kaptula.''

  Sijapata kusema kuwa Kiyate Mshumi aligawa kadi za TANU Rufiji.

  Rufiji Abdul Sykes alimkabidhi Said Chamwenyewe hii iilikuwa Julai 1954
  wakati wa kuisajili TANU na ndiyo walitoa wanachama wa mwanzo wa TANU
  na uamuzi huu ulifanywa nyumbani kwa Ally Sykes Mtaa wa Kipata na hapo
  aikuwapo walikuwa Abdul, Ally na Nyerere na Bi. Zainab mkewe Ally Sykes.

  Abdul Sykes mwenyewe yeye aliuza kadi za TANU pale kazini kwake Kariakoo
  Market.

  Kisa hiki nimekieleza katika kitabu cha Abdul Sykes atakae anaweza kusoma.
  Nahitimisha kwa kufahamisha kuwa sina ''muhali,'' wala ''tafrani,'' lugha yangu
  ndiyo hii ikiwa hii unaona ni shari kwako basi hakika una lako jambo.
   
 21. YEHODAYA

  YEHODAYA JF-Expert Member

  #80
  May 19, 2017
  Joined: Aug 9, 2015
  Messages: 11,112
  Likes Received: 10,447
  Trophy Points: 280
  Kwani chadema wamewahi jenga kipi kwa pesa zake? Chadema pesa wanazotumia ni za walipa kodi ambazo ni za ruzuku lakini wameandika kuwa ni mali za chadema utafikiri walitumia pesa zao.mna ufahamu mdogo mno tena sana hizo pesa za ruzuku ni za watanzania wote mnapata wapi guts za kusema hizo mali za chadema?
   
Loading...