Acheni watu waseme, nani angempinga yule shujaa wa Afrika?

The golden

JF-Expert Member
Sep 11, 2018
1,381
2,553
Kameibuka katabia kakusema, "aaa mbona hukusema kipindi yupo?"

Tuweni wakweli basi, nani kati yetu angethubutu kumkosoa?

Nani angempinga mpakwa mafuta wa bwana? Yule alikuwa mteule bwana.

Alikuwa na masikio ya kusikia hata kama ungeongea kwa sauti ya kunong'ona. Jamaa alikuwa anatisha. Kulitaja jina lake ilibidi kwanza ujitie kichaa. Hata sasa bado tunamuogopa. Ngoja niishie hapa asije akanisikia.
 
Inaonekana leo umezunguka mji mzima bila kurudi hata na nazi nyumban, ndo maana hasira na stress zako umeamua uje umalizie hapa jamii forum, pole san kijana
 
Kwa kweli tuwaache waseme tu😀😂 watu wanamlaumu ndugai, unafikiri yeye hajipend? Huyu Rais si ndo alikuwa Makamu wake tena yupo kwenye high command af sa hv anajifanya kuwanyooshea vidole wenzake? Wote walikuwa under hot supu.

Kama kuna maamuz ya hovyo na wao waliona kabisa sema wakatulia kulinda ugali ni mda wa kufanya marekebisho wala wasiogope bhana. Nani angekubali ujenzi wa SGR bila kurekebisha mfumo Kwanza wa Bandari? Nani angekubali ujenzi wa uwanja wa ndege wa kimataifa chato huku unauacha wa Mwanza?!
 
JPM na wapambe wake kweli kila Zama na kitabu chake ,ila mungu Huyu,acha aitwe ALFA NA OMEGA, UFUNDI WAKE KAMWE WATISHA SANA , ila mbele zake yeye binafsi , alafu eti polepole anasimama bungeni kwamba wananchi waliokua wanalia walikua na Jambo lao na awamu ya tano.

Ukweli wa mungu ni kwamba waliolia Sana ni wale waliokua na connection za upigaji,utesaji, kunyanyasa WATU mpaka wengine kukimbia nchi yao , wengine walikua wa kutengeneza, mfano.

Mkulima analiaje
Mtumishi analiaje
Mfanyabiashara vipi

Aliebomolewa nyumba Bila fidia,Ndugu jamaa wa waliofukuzishwa na vyeti feki, waliopotelewa na Ndugu zao,wanachama walioporwa ushindi wao waziwazi wa ccm kura za maoni, na vyama pinzani,ugum wa maisha kila kona nani wa Julia mpaka kugalala kwenye magroup hayo, watanzania sio wajinga
 
Back
Top Bottom