Acheni ushabiki wa Usimba na Yanga, Jerry Muro yupo sahihi uchawi upo na watu wanalogwa

popo1986

JF-Expert Member
Jul 30, 2014
1,120
371
Kwa kawaida upinzan katika mpira hususani simba na Yanga ni mkubwa sana .....lakini jambo ambalo Jerry Muro alimtuhumu mjumbe wa simba sports club kuingia kinyemela katika jengo la Yanga ni uhalifu mkuu....alichokifanya jerry muro ni kujihami kitu ambacho kwa yyte mwenye akili timamu anaelewa uhasama uliopo kati ya simba na yanga ataelea na pia Jerry muro anatambua kua ni hakika UCHAWI UPO.........<<<<UCHAWI UPO NA WATU WANALOGWA KWELI>>>>>>
Kama hutataka kuniamini ni kwa kuwa unaushabiki mno....lakini hebu tuongee fact <<<<UCHAWI KATIKA MPIRA UPO.>>>> Kwa wale mashabiki wa Yanga nyie mtanielewa vizuri kwa sababu mtakumbuka kilicho wapata msimu wa jana katika ligi kuu ya vodacom-Tanzania kule mkwakwani Tanga ile mechi ya mwisho mliocheza na mgambo...mechi ambayo iliwapa Azamu ushindi.......

JERRY MURO KAMA MSEMAJI WA YANGA YUPO SAWA KWA KUMSHUKU HUYO MJUMBE WA SIMBA KUWA ALIKUJA KULOGA........KAMA SIVYO WW UNAESOMA HII COMMENT JIULIZE ALIFUATA NINI JANGWANI?
 
Msomi mzima tena kijana anaamini ushirikina kweli? Ndio maana mapambano dhidi ya mauaji ya alibino na wazee wetu(vikongwe) hayafanikiwi kwa sababu ya wapumbavu kama hawa. Jana nliumia sana kumuona msomi ambae ni kijana na public figure akitamka maneneo ya kishirikina.
 
Mtu ambaye katika karne hii bado anaamini katika uwepo wa nguvu hewa za uchawi ni bado hajajikomboa kutoka kwenye minyonyoro ya ujinga!
 
Msomi mzima tena kijana anaamini ushirikina kweli? Ndio maana mapambano dhidi ya mauaji ya alibino na wazee wetu(vikongwe) hayafanikiwi kwa sababu ya wapumbavu kama hawa. Jana nliumia sana kumuona msomi ambae ni kijana na public figure akitamka maneneo ya kishirikina.


Mimi ni mshabiki mkubwa wa Yanga. Lakini sikubaliani kabisa na Jerry Muro tena amenishangaza saana saana. Baba wa watu kajieleza kutumia oppourtunity ya waandish wa habari kuwepo pale kupeleka press release yake na amejieleza vizuri. Mbona Mzee Akilimali alimuelewa kabisa na alikaa nae kwenye benchi kirafiki zaidi. Jerry anataka kutupeleka wapi? Wakati serekali inataka kupambana na imani hizi za kishirikina yeye kama muandishi wa habari mzoefu anaturudisha nyuma. Nilimfurahia sana huyu kijana nilivyotambua ni Msemaji wa Yanga alakini sasa nina mashaka nae. Hivi kuna mtu ana uchungu kuliko Mzee Akilimali? Mbona hakuenda huko alikoenda Jerry Muro. No this is not acceptable Jerry, najua utakuwa unasoma mitandao hapa umepotoka!
 
Mleta mada ww na Jerry ndio wachawi yule jamaa hajaenda kwaajili ya Simba pale Jangwan ameenda kupeleka habari kwa wanahabar waliokua wanamsikiliza Jerry kwakua ametoka ukumbi wa habar maelezo ameambiwa wapo hapo jangwan na Mzee akilimali alivyoombwa na huyo jamaa mzee akamjibu mm sihusiki muone Jerry ila Murro anaanza kufoka hovyo ni ujinga tu mtu anakuja kukuroga mchana kweupe mbele ya macho yote na camera zote zile.Jerry Muro hana tofauti na Nape kwa uropokwaji
 
mkuu nielewe nimesema Jerry muro amejihami kwa njia hiyo..
 
simba mliwafanyia yanga mambo mabaya sana basi tu yanga ni timu ya wananchi ingekuwa kama nyota nyekundu haingekuepo.
 
huyu jerry muro angekamatwa maana naweza akawa nahusika na mambo ya mauaji ya albino. kwa jinsi anavyoongea ana weza amini kuwa Yanga ili ishinde inapaswa kupata mkono au mguu wa albino na akaamua kutafuta watu wa kutafuta viungo hivyo.
 
Jamani wana Yanga imekuaje tena Muro mnakubali kuambatana na Simba ZIMBABWE wakati tunajua hawa wanatafuta kutushusha kwenye ligi na kusajili wachezaji wetu? Hamuoni wanatafuta jinsi ya kuwakaribu na timu yetu ili wapenye kwa wachezaji? Kuweni makini na hili.
 
Tuweni makini sana hasa kipindi hiki.juzi tu wameingia klabuni leo wanataka kuambatana na timu wao timu yao inacheza ligi mapenzi hayo yametoka wapi muda huu?
 
Mleta mada ww na Jerry ndio wachawi yule jamaa hajaenda kwaajili ya Simba pale Jangwan ameenda kupeleka habari kwa wanahabar waliokua wanamsikiliza Jerry kwakua ametoka ukumbi wa habar maelezo ameambiwa wapo hapo jangwan na Mzee akilimali alivyoombwa na huyo jamaa mzee akamjibu mm sihusiki muone Jerry ila Murro anaanza kufoka hovyo ni ujinga tu mtu anakuja kukuroga mchana kweupe mbele ya macho yote na camera zote zile.Jerry Muro hana tofauti na Nape kwa uropokwaji

tangu siku ile nikimkuta jerry anaongea nahama channel mpuuzi sana alitakiwa amsikilize halafu mengine yangefuata nilichokisoma kutoka kwake ni kwamba
1. Si mwana michezo
2. Malezi yasiyoridhisha
3. Hana adabu maana yule bwana ni mkubwa sana kwa kwake
4.Anajifanya anauchungu sana na yanga kuliko walioianzisha

pale yangu hawana mtu wamechagua jina
 
Muro anamzuia huyo jamaa wakati anaambatana na timu iliyojaa wachezaji kibao ambao ni wapenzi wa Simba, tukianzia Barthez!
 
Kwa kuwa wanaitwa WATANI Jerry yuko sahihi, au ninyi mnaopiga kelele hamuelewi
maana ya UTANI? Hawa ni watani wa jadi na anachokifanya Jerry ni utani tu.
 
Back
Top Bottom