Acheni mbwa wavae tisheti za CCM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Acheni mbwa wavae tisheti za CCM

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by RMA, Oct 27, 2010.

 1. R

  RMA JF-Expert Member

  #1
  Oct 27, 2010
  Joined: Oct 10, 2010
  Messages: 409
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Polisi huko Songea wanamtafuta mtoto wa darasa la Sita kwa kumvisha mbwa tisheti ya CCM. Hata watoto wamechoshwa na CCM. Huyo mtoto asisumbuliwe. Ameonyesha uzalendo wake. Watanzania wote waige mfano. Popote pale mbwa walipo wakamatwe, wapewe zawadi za CCM dakika hizi za lala salama.
   
 2. Oxlade-Chamberlain

  Oxlade-Chamberlain JF-Expert Member

  #2
  Oct 27, 2010
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 7,928
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  Huu ni uonevu wa hali ya juu.wao wamepita kugawa kofia na fulana kwa wananchi bila kujali nani anawaunga mkono au nani hawaungi mkono.sasa wale wasiowaunga mkono ndio wameamua kumvalisha mbwa wao t-shirt hio ya ccm kwani kwao haina thamani.


  Itakuwaje hilo liwe kosa? Kila mtu anaamua mwenyewe haitumie vipi zawadi yake au hongo aliopokea na sio kuwapangia wananchi.Ccm waligawa fulana hio na hapo hawaimiliki ni huyo mtu aliyepewa ndio mmiliki na ana haki ya kuifanya chochote anachotaka.
   
 3. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #3
  Oct 27, 2010
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  hawa ccm wanachekesha kweli yaani wanawakana wenzao hadharani.baba wataifa angekuwa hai angemtetea huyo mtoto.
   
 4. R

  RMA JF-Expert Member

  #4
  Oct 27, 2010
  Joined: Oct 10, 2010
  Messages: 409
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  [​IMG]
   
 5. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #5
  Oct 27, 2010
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Hilo halikubaliki kabisa kabisa ,kwani sio ustaarabu wa kufanya siasa naona waliofanya hivyo watakuwa wamejidharau wenyewe na wamekosa uvumilivu wa kisiasa au wameshindwa na akili zao zinaonyesha wazi wazi ni finyu ,mimi wakati wa kampeni huwa nauona kama wakati wa mavuno kuna watu wanajenga ,kuna watu wanatajirika wakati huu na kuna watu wanapata hela wakati huu na wengi wa hao hawajali wanapokea hela au kitu,au tuseme zawadi kutoka chama gani, jamani siri ya mpiga kura anaijua mtu mwenyewe ,wakati wa kampeni huwa tunasema ukipewa hela pokea na kula,ukipewa ngua chukua na ivae ,hivi jamani hapa JF zitembezwe milioni mojamoja kwa cheque ,iwe inatoka CCM ,au Chadema au CUF au kwengine kokote kule mtazikataa ,mimi nitachukua na kura yangu nitaipeleka ninapoitaka na kama kofia na fulana nitazivaa vile vile ,muhimu msimamo wangu haubadiliki, Sasa tuchukue picha ya mgombea wako amevalishwa huyo jibwa ,wewe utahisi vipi ? Hilo kwa kweli halikubali na kamuulize huyo kiongozi wako uone jibu atakalo kupa na akikwambia inafaa basi hafai kuwa kiongozi hata wa timu ya gololi.
   
 6. K

  KIURE Member

  #6
  Oct 27, 2010
  Joined: May 8, 2009
  Messages: 16
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hivi hao CCM kama wangetengeneza unifomu za shule na kugawa mbwa angevalishwa? Hawajui hata namna ya kampeni. Wao wanataka watu wavae picha la chizi au mtu wanayedhani amewasababishia matatizo kifuani? Kama ingekuwa fulana yenye picha ya Slaa au Maalim Seif akapewa mshabiki wa CCM ingepokelewa? Kwanza ingezua ugomvi wa mapanga! Sasa hao jamaa ni wastaarabu sana, wamepokea wakaamua kuitumia wanavyopenda wao kwa kuwa ni mali yao ya halali. Ubaya uko wapi? Wanasheria wasaidieni hao kwani wanaonewa tu. Tundu Lisu upo?
   
Loading...