ARCHBISHOP
JF-Expert Member
- Jan 15, 2012
- 271
- 484
Wanajukwaa,
Kwanza nichukue nafasi hii kuwakumbusha ndugu, jamaa na marafiki kwamba, ni vyema tukajua ni wapi tuchore mstari wa mwisho unapojadili mambo yasiyo kuhusu, especially yanayogusa hisia za wengine.
Pili niwe wazi mimi ni mmoja wa waathirika wa jambo ninaloenda kuliandika, maana nipo kwenye ndoa kwa miaka miwili na sijajaliwa mtoto.
Kuna katabia miongoni mwetu wa Tanzania pale vijana wanapoamua kuoana basi watu ujipa majukumu yaku "monitor" matumbo ya wenzao, utasikia wanaanza kukuuliza bado tu? Hamjapata mtoto? Fanyeni bwana muda unaenda, lakini jambo wasilolijua nikwamba nijinsi gani wanavyoumiza nafsi zetu, hawajui mangapi tunapitia, mimba kutoshika, mimba kutoka na mengine mengi.
Unaulizwa mpaka kama unailenga ipasavyo? Jitihada zote hizi mngeziweka katika kutuchangia labda tufike kwa wataalamu wa uzazi ikiwezekana tukafanya direct plantation ingependeza kuliko kutuamkia kutwa kucha kusikitika pamoja na sisi.
Wengine wamepata mmoja mambo yakagoma au wameamua kupumnzika, basi utasikia lini mnapata mwingine? Mmekuwa ovulation monitor? Tukimpata mbona hata nepi hamleti? Ada mtalipa? Acheni hii tabia maana haitufariji bali inatuumiza. Kama mpo wenye hari kama hii tushirikishane uzoefu na tuungane kuilaani.