Acheni kuwauliza wanandoa lini wanapata watoto

ARCHBISHOP

JF-Expert Member
Jan 15, 2012
271
484
Wanajukwaa,

Kwanza nichukue nafasi hii kuwakumbusha ndugu, jamaa na marafiki kwamba, ni vyema tukajua ni wapi tuchore mstari wa mwisho unapojadili mambo yasiyo kuhusu, especially yanayogusa hisia za wengine.

Pili niwe wazi mimi ni mmoja wa waathirika wa jambo ninaloenda kuliandika, maana nipo kwenye ndoa kwa miaka miwili na sijajaliwa mtoto.

Kuna katabia miongoni mwetu wa Tanzania pale vijana wanapoamua kuoana basi watu ujipa majukumu yaku "monitor" matumbo ya wenzao, utasikia wanaanza kukuuliza bado tu? Hamjapata mtoto? Fanyeni bwana muda unaenda, lakini jambo wasilolijua nikwamba nijinsi gani wanavyoumiza nafsi zetu, hawajui mangapi tunapitia, mimba kutoshika, mimba kutoka na mengine mengi.

Unaulizwa mpaka kama unailenga ipasavyo? Jitihada zote hizi mngeziweka katika kutuchangia labda tufike kwa wataalamu wa uzazi ikiwezekana tukafanya direct plantation ingependeza kuliko kutuamkia kutwa kucha kusikitika pamoja na sisi.

Wengine wamepata mmoja mambo yakagoma au wameamua kupumnzika, basi utasikia lini mnapata mwingine? Mmekuwa ovulation monitor? Tukimpata mbona hata nepi hamleti? Ada mtalipa? Acheni hii tabia maana haitufariji bali inatuumiza. Kama mpo wenye hari kama hii tushirikishane uzoefu na tuungane kuilaani.
 
Hizo story mnaanzia wap hadi kufikia kuulizana mambo hayo? Si kwamba ww ndo unatoa nafasi ya kuulizwa maswali hayo? Pamoja na yote si vema kuuliza Umri wa Mtu, Mambo yanayohusu Familia za Watu na Una Watoto wangapi???
 
Pole sana mkuu watu wanakera kweli. Usiwape nafasi ya kukuuliza maswala hayo.
 
Kweli mkuu hata mim ktk ndowa yangu nimepitia changa moto hiyo nadhani ilipita miezi kadhaa kama(9) hivi toka nilipo funga ndowa na mke Wang akiwa hajashika ujauzito kiukwel halihiyo ilinikosesha raha kipindichote hicho cha miezi 9 kutokana na maneno aliyo kuwa anasemwa mwanamke Wang tena anesemwa maneno hayo ni mamangu mdogo akiwa anamsema mke wang kwa majirani na majirani hawo wanakuja kufkishia huwo umbea mke Wang kiukweli niliumia xana Maneno hayo kusemwa na mamaangu mdogo, maneno yenyewe alokuwa akisemwa mke Wang ni haya yafuatayo Eti huyo mke wafulani ambae ni mke wangu alishaga towa mimba ndio maana kachelewa kushika mimba, kiukweli maneno haya yaliniuzunisha sana kusemwa namtu kama mamaangu mdogo kwa nini asinge nifuata kabla sijamuo huyo mwanamke nakunifahamisha Mimi ili ibakie ni juuyangu kuchaguwa kuowa au kutoowa,? kweli rafiki wakaribu ndie anae kuharibia kazi na kukuvunjia Nazi. ila kwa sasa namshukuru M/mungu mke wang ni mjamzito Na ujauzito wake unamiezi 8 sasa...
 
Pole sana, hii tabia ya kijinga sana,nakushauri kama kitu hupendi hasa kuhusiana na familia/ ndoa yako sema, usimpe mtu mwanya kukupangia mambo.
Na pia wale wenye kuuliza unaoa lini? Kwa nini hujaoa wanakera pia. Vitu vingine sio mashindano.
 
Pole boss..





Hii hutokea zaidi kwa kuwaendekeza watu na kuwaachia wawe ni michango juu ya maisha yako binafsi...







Haijalishi ni nani....ndoa ni kati ya mume & mke na sio ukoo,jamaa & marafiki!
 
Kuna katabia miongoni mwetu wa Tanzania pale vijana wanapoamua kuoana basi watu ujipa majukumu yaku "monitor" matumbo ya wenzao, utasikia wanaanza kukuuliza bado tu? Hamjapata mtoto? Fanyeni bwana muda unaenda, lakini jambo wasilolijua nikwamba nijinsi gani wanavyoumiza nafsi zetu, hawajui mangapi tunapitia, mimba kutoshika, mimba kutoka na mengine mengi.

Mkuu;
Kwanza niseme; Sijawahi kupata shida katika kuzaa hadi nikawakataa mwenyewe kuwa sitaki tena. Ila, huwa napambana na mtu yeyote anayewasumbua wana ndoa kwa habari za kuzaa. Yaani wengine ni kero hadi wanawafanya wanandoa wanachepuka. Kisa, mmechelewa kupata mtoto. Hii ni dhambi mbele za Mungu. Haikubaliki.
Nilipoenda kuoa sikuenda kutafuta watoto bali mwenzi wa maisha. Anipende yeye nami nimpende yeye. Ningelitaka mtoto ningemzalisha kwanza ndipo nimuoe. Lakini neno la Mungu linatunyima kumjua kabla ya ndoa. Viongozi wengi wa dini haswa za Wapentekoste hawaifungi ndoa mwanamke akiwa na ujauzito unaoonekana. Sasa hapo si ni pata potea??
Yawezekana pia tumepanga uzazi kutokana na malengo mazuri tuliyo nayo. Labda, tumalize ujemzi kwanza na kama mwenzangu akiwa mbali nami, naweza nikatenda dhambi ya uzinzi. Sasa tukapatana tuoane, tuzuie mimba miaka 3 halafu ndo tuanze uzazi. Yawezekana mwenzangu anataka kusoma zaidi, hatuwezi kuchukua majukumu yote hayo kwa pamoja ila tuende kwa mpango. Swali; Wewe mama mkwe/mawifi/jirani mna shida gani na nyumba yangu??
Jambo hili ni la kukemea na kuwadharau hadi mwisho. Mnaopitia majaribu haya, wekeni pamba masikioni na kuvaa miwani ya mbao msiwasikilize hao wambeya.
 
Back
Top Bottom