Acheni kutumia picha za watu weusi kuripoti mlipuko wa monkeypox!

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,006
1,026
VCG31N1240797679.jpg


Hivi karibuni, ugonjwa wa monkeypox umeendelea kuenea katika nchi za magharibi. Tangu tarehe 13, nchi 23 zikiwemo Marekani na Uingereza zimeripoti maambukizi zaidi ya 250 yaliyothibitishwa na zaidi ya maambukizi 100 yanayoshukiwa kwa WHO. Hata hivyo, Reuters, BBC, ABC News na vyombo vingine vya habari vya magharibi vimetumia sura nyingi za Waafrika weusi katika ripoti zao kila vinapozungumzia ugonjwa huo.

Shirika la Afya Duniani WHO hivi karibuni lilisema virusi vya monkeypox ambavyo havina matibabu kwa sasa hupatikana zaidi Afrika Magharibi na Afrika Kati. Ingawa zamani kulikuwa na maambukizi yaliyoenda Marekani kutoka Afrika, wasiwasi wa sasa ni kwamba monkeypox inaenea kutoka kuwa ugonjwa wa kikanda hadi maeneo mengine. Kauli hii ina ukakasi kiasi na imezuia maswali. Je, ni nchi ngapi katika maeneo ya Afrika Magharibi na Kati zilizowahi kukumbwa na maambukizi ya monkeypox? Je, ugonjwa huo ambao uliibuka barani Afrika na kutajwa kama "ugonjwa wa kikanda", unaweza kuzua wasiwasi tu unapoenea hadi Marekani? Inaonekana kuwa ni sahihi kwa ugonjwa huo kutokea barani Afrika, na kinga dhidi ya ugonjwa huo imetolewa kwa muda mrefu kwa watu wa mahali pengine.

Lakini kinachoudhi zaidi ni "ukuu wa wazungu" unaoonyeshwa na vyombo vya habari vya magharibi. Mei 20, ABC ilitumia "seli za virusi chini ya darubini" kama picha katika ripoti yake juu ya kuenea kwa ugonjwa wa monkeypox katika nchi za Ulaya na Marekani, lakini makala hiyo ilisema, "Ugonjwa huu unaonekana kuenea kwa mara ya kwanza miongoni mwa watu ambao hawajafika Afrika."

Lakini katika angalau makala tatu zilizofuata, ABC ilitumia picha za watu weusi wenye vipele mikononi na tezi zilizovimba kuripoti hali ya maambukizi ya ugonjwa huo katika jiji la New York na maeneo mengine ya Marekani. Picha hizo zinaelezwa kuwa "zilizopigwa na CDC ya Marekani wakati wa mlipuko wa monkeypox nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo mwaka 1997 ".

Na vilevile makala ya BBC Mei 22 ilitumia picha ya mtu mweusi akiwa na vidonda wazi mwilini kuripoti ugonjwa huo unaoenea Magharibi.

Ripoti hizi zimepingwa na sekta zote barani Afrika. Shirikisho la Waandishi wa Habari wa Kigeni barani Afrika (FPPA) lenye makao yake makuu nchini Kenya, limetoa taarifa likisema matumizi ya picha za Waafrika yanazidisha picha hasi na "kubebesha lawama jamii ya Waafrika kwa janga hili". Mtumiaji wa Twitter Siphumelele Zondi naye alisema: “ukiangalia tu picha hizo utafikiri ugonjwa wa monkeypox unalipuka barani Afrika, kwa sababu vyombo vya habari vya magharibi vinachagua picha za waafrika weusi zinapoeleza habari kuhusu ugonjwa huo. Lakini ukisoma habari zenyewe unaona kuwa ugonjwa huo unaenea Ulaya na Marekani, na hakuna uhusiano wowote na Afrika."

Kwa muda mrefu, jamii ya Waafrika imekuwa ikipinga habari potoshi kuhusu Afrika katika vyombo vya habari vya magharibi, ambazo huwa zinaielezea Afrika kama sehemu ambayo kila siku inapambana na magonjwa na maafa. Mwaka 2019, gazeti la The New York Times lililaaniwa sana kwa kutumia picha za maiti kuripoti shambulio la kigaidi huko Nairobi, Kenya.

Kuna maswali matatu ya kimsingi yaliyoulizwa na Shirikisho la FPPA katika taarifa yake, "Je, si ni jambo la kimantiki zaidi kwa vyombo vya habari vya magharibi kutumia picha za hospitali za nchi zao? Je, kutumia picha kama hizi kunaweza kuzisaidia nchi za magharibi kujikwamua kwenye mlipuko wa ugonjwa wa monkeypox? Je, vyombo hivi vya habari “vinalinda usafi wa wazungu’ kupitia ‘uhalifu wa watu weusi’?”
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom