Mindi
JF-Expert Member
- Apr 5, 2008
- 3,523
- 4,991
Huwa nashangaa sana watu wanaoiona ACACIA kuwa ni tofauti na BARRICK GOLD. ni Barrick walioanzisha kampuni tanzu ya ACACIA ikiwa ni namna ya kushughulika na nchi zetu za kimagumashi, na viongozi magumashi. Nyerere mwenye akili aliwaambia kabisa mapema kwamba subirini kwanza, tujipange kama nchi. uroho wa Mkapa ukatuingiza kichwa kichwa. PAPARA ZA MAGUFULI NAZO ZIKATUTOA MATAKO MATAKO.Naikumbuka hiyo kesi, ilifunguliwa na Acacia. Tusisahau tangia mwanzo Acacia walionekana kupinga moja kwa moja madai ya serikali huku parent company, Barrick ikiweka mbele suala la majadiliano na serikali!!
So, few months ago baada ya Barrick kuonesha wazi kwamba wanataka "kulimaliza" hili suala kwa majadiliano kutokana na makubaliano ya awali waliyokuwa wameafikiana na serikali, hapo hapakuwa na namna zaidi ya Acacia kufuta kesi kesi ili hatimae Barrick warudi mezani!
Kwa mfano, habari ya Reuters kuhusu Acacia kuachana na kesi ni hii hapa:-
Unaona hapo hiyo habari imeripotiwa July 17, 2019.
Makubaliano ya Awali kati ya Serikali na Barrick Gold ni haya hapa:-
View attachment 1239915
Unaona hapo makubaliano yanaonekana ni July 19, 2019... yaani siku 2 tu baada ya Acacia kutangaza kuachana na kesi!!!
Kwahiyo ndo tunarudi pale pale... kwenye makubaliano ya awali tayari Barrick alishafahamu watatakiwa kulipa ile USD 300 Million TU, tena kwa masharti kwamba, hatimae makinikia yataruhusiwa kusafirishwa!!
Hiyo kwao ilikuwa ni advantage ndio maana Acacia wakafuta kesi! Na hapa hapa JF nilishawahi kuongea kwamba Acacia watajifanya kuendelea ku-press hard ili kuitisha serikali na hatimae wakubaliane na suala la "Kishuka Uchumba" tu, na ndicho kilichotokea!!
Sasa kama Kabudi anahisi anastahili pongezi kwa Acacia "kufuta" kesi kutokana na ushawishi wake, then we've long way to go! Kama ni kutokana na ushawishi wake, kwanini Acacia wafute kesi baada ya kuona makubaliano yameshafikiwa na badala ya kulipa yale matrilioni, hivi sasa watalipa tu mabilioni na makinikia yanaruhusiwa kusafirishwa!!
Barrick anaonesha kidole kwa ACACIA kwamba ndiyo mtoto mkorofi, wakati yeye ni msikivu na mtiifu!!! Barrick ni wazoefu sana wa kupora mali kama hizi kwa miaka nenda miaka rudi.
Hata hii habari ya kampuni ya pamoja na hisa 16%, subiri kwanza uone je tutapata kitu? nina mashaka sana tutaambulia propaganda tu.