Acheni kupotosha alichokuwa amesema Tundu Lissu kuhusu Acacia na MIGA

Chige

JF-Expert Member
Dec 20, 2008
9,929
2,000
Wafuasi wa Lumumba ama kwa ile kukosa uelewa, au kwa makusudi tu, since Day 1 wamekuwa wakipotosha ambacho Tundu Lissu aliongea kuhusu MIGA! Au wakati mwingine inawezekana ni kutokana na tabia yetu Watanzania ya kutotafuta ukweli!

Binafsi nimekuwa nikilijadili suala la makinikia since Day 1, na kwavile nilikuwa nafuatilia sana nakumbuka vyema nini Tundu Lissu aliongea, na ninamnukuu hapa chini:-
Sisi Tanzania ni wanachama wa kitu kinaitwa the MIGA Convention. MIGA ni the Multilateral Investment Guarantee Agency ya Benki ya Dunia. Ukiwa mwanachama, Wawekezaji wakileta mali zao kwako, ukiwa-expropriate, ukichukua mali zao kama alivyochukua namna hii, utapelekwa kwenye mahakama za kimataifa... unaenda kushughulikiwa huko. Unaenda kushughulikiwa... huko!
....................................................
Kwahiyo tafadhali sana... na sisi tumezungumza, haya mambo tumeyapigia kelele for years... for years. Hatujaanza jana. Kama unataka kufanya hayo unayoyafanya, elewa hali halisi ilivyo. Tatizo liko wapi! Kama tatizo ni kwamba tunapata mapato madogo... na ni kweli wanatupiga kweli kweli. Wanatupiga kweli kweli. Kama unataka kufanya mambo... kweli kweli, kajiondoe kwanza MIGA ili hawa wawekezaji wasikushitaki kwenye hizo mahakama za huko.
Hiyo ndiyo hoja ya Lissu... kwamba, kama kweli Serikali ya Magufuli ilikusudia kupambana na Acacia, basi walitakiwa kwanza wajitoe kwenye mkataba wa MIGA!

Ushauri sawa na huo wa TL ulikuja tena kutolewa na Dr. Rugemeleza Nshala mbele ya Wabunge walipokuwa wanatafuta maoni ya wadai wakati wa utungwaji wa sheria mpya ya madini.


Gazeti la the Citizen linatujuza:-
By doing so, said the co-founder and executive director of the Lawyers' Environmental Action Team (LEAT), Dr. Rugemeleza Nshala, the country country would be able to defend its sovereignty from instutions like the Multilateral Investment Guarantee Agency (MIGA) Convention, and the International Centre of Settlement of Investment Disputes (ICSID).

"To make sense out of what we want to achieve with these laws on natural resources, we need to start the withdrawal exercise sooner than later,” he said told Members of Parliament who were collecting stakeholders’ views on three natural resource bills here yesterday.
Pia the Citizen wanatukumbusha kwamba, Dr. Nshala ni Mtanzania wa pili kutoa ushauri kama huo huku wa kwanza akiwa ni TL:-
Dr Nshala becomes the second Tanzanian to push for the country’s withdrawal from Miga and ICSID since President John Magufuli embarked on the struggle to ensure that Tanzania gets a fair share of revenues from its minerals and other natural resources.

In May, Mr Tundu Lissu, president of the Tanganyika Law Society (TLS), was quoted as making a similar proposal immediately after President Magufuli received the findings of an investigation into possible undeclared exports by mining companies to evade tax.
Kwa maajabu ya wale waliofuatilia suala la umakini, watu wakapotosha na kudai TL amesema tukipambana na Acacia, watatupeleka MIGA, na huu ndo umekuwa wimbo wa wana-CCM na wafuasi wa serikali!

Busara ya TL kushauri kujitoa MIGA unaweza kuiona kupitia tovuti ya MIGA, hivi ndivyo wanasema:-
As a member of the World Bank Group, MIGA provides an umbrella of deterrence against government actions that could disrupt insured investments and helps resolve potential disputes to the satisfaction of all parties—both of which enhance investor confidence in the safety of investments and encourage the flow of foreign direct investment.
Hapo wanaongea wazi ni namna gani pamoja na mambo mengine, wana jukumu la kulinda uwekezaji dhidi ya maamuzi ya serikali!

Sasa basi, hoja ya TL ilikuwa ni kwamba, tukishavurugana na Acacia ,watakachofanya wao ni kile ambacho kinafanywa na kampuni zingine... yaani kukimbilia Mahakamani, au MIGA!

Lakini kama kweli umeamua kupambana na hawa jamaa, unachotakiwa ni kuchomoa betri kwa kujitoa MIGA ili wasiwe na kwa kukimbilia zaidi ya kwenda kwenye mahakama zetu wenyewe... yaani mahakama zile zile zinazoamua ma-DED wanastahili kusimamia uchaguzi ambao mmoja wa washiriki ni mwajiriwa wake mwenyewe!!!

Kwa maana nyingine, ukishajitoa MIGA maana yake ni kwamba unakuwa huzitambui mahakama zao! Ni kama United States asivyoitambua International Criminal Court, matokeo yake pamoja na uhalifu wote wa kivita wanaoufanya duniani kote, huwezi kumpeleka Mmarekani ICC .

Maajabu makubwa zaidi ya taifa hili, badala ya kuiangalia hoja ya TL Critically, watu wale wale wanaojiona ndio wazalendo zaidi, wakaona mtu kama TL anastahli kuuawa mara moja... na wafuasi wa CCM na serikali yake wamekuwa wakiirudia kauli hii mara kwa mara!!!!

Je, kumpuuza TL kumetugharimu kama taifa?!

Serikali na watetezi wataendelea kujitekenya wenyewe na kucheka wenyewe lakini ukweli ni kwamba imetugharimu kama taifa!

Sote tumeshuhudia danadana za Acacia... watetezi wa serikali wasichofahamu ni kwamba, danadana zote zile ni kwa sababu walifahamu maji yakiwazidi shingo, wangekimbilia mahakamani ambako katu tusingetoka.

Na kwa Mtanzania yeyote anayekejeli kauli hiyo ya TL, kwa hakika anatakiwa kujitafakari mara mbili... anatakiwa kujitafakari kwa sababu sisi ni victim wa hizi mahakama, hususani kupitia IPTL!

Sote sisi tunakumbuka kushikiliwa kwa Bombardier kwa wiki kadhaa kule Canada kutokana na maamuzi yaliyotolewa na mahakama za aina hii!!

Hivyo basi, ili kujilinda tusipelekwe kwenye mahakama kama hizi ambazo kuchomoka ni nadra sana, ndipo TL akasema ukitaka kupambana na hawa watu, basi jitoe MIGA lakini sio kwamba tukipamba na Acacia, wanatupeleka mahakamani!!!

Je, kwanini Acacia Hawajatupeleka MIGA?

Kwa kifupi ni kwamba, Acacia hawakuwa na sababu ya kutupeleka MIGA kwa sababu serikali imepita njia ambayo ni nafuu maradufu kwa Acacia!

Kuweka kumbukumbu sawa, wakati Profesa Orosso akiwakilisha Ripoti ya Pili, alitoa takwimu ya pesa ambayo serikali ilipoteza kama mapato! Prof. Orosso na timu yake waliweka makadirioo ya kiwango cha chini kabisa ambacho serikali ilipoteza, na kiwango cha juu kabisa!

Tuachane na kiwango cha juu kabisa, Profesa Orosso anatujuza, na ripoti kamili inapatikana tovuti ya Ikulu:-
Jumla ya mapato ya Serikali ambayo Serikali ilipoteza ni TZS trillion 68.59 ambazo ni sawa na bajeti ya miaka miwili ya Serikali kwa kigezo cha makadirio ya mwaka 2017/2018.
Hicho ndicho kiwango cha chini kabisa... na ukichanganya na adhabu (ya kuchelewesha kulipa kodi), jumla ndo ile figure maarufu ya TRilioni 450!!

Sasa hebu tujiulize... Uchunguzi uliofanywa na akina Prof Mruma na mwenzake Prof Orosso (pamoja na timu ya watu wa TRA), ilionesha Acacia wamekwepa kulipa Sh. 68 kwa miaka 17. Leo hii serikali imekubali kulipwa Sh. 700 Billion... sasa hata kama wewe ndo ungekuwa Acacia, ungeenda MIGA kufanya nini?!

Na kama ilivyo kwa mahakama zingine, kesi za MIGA zinachukua miaka na miaka!! Sasa kwanini ukae miaka yote hayo huku biashara ikiendelea kuathirika kwa kushindwa kusafirisha makinikia?!

Sasa wakati Wafuasi wa CCM na serikali yake wakiendelea kumkejeli TL kwamba mbona hao Acacia hawajaenda MIGA, jibu ndo hilo hapo! Hawajaenda kwa sababu sisi ndio tumeliwa! Tumekubali kuchukua Sh. 700 Billion out of 68 Trillion!!!!

NOTE: Moderator punguzeni kasi ya kuunganisha threads bila sababu za msingi eti kisa tu kuna baadhi ya keywords zinafanana!!! Kuandika haya mambo it takes time... so, it sucks mtu unapoteza saa moja na ushee kuandika thread, unakuja next time, huoni kwa sababu imeunganishwa na thread nyingine!
 

Nanye Go

JF-Expert Member
Oct 29, 2018
5,753
2,000
Kuna video nikiona juzi Kabudi alisema ACACIA walifuta arbitration case London, hiyo ilikuwa ni sehemu ya makubaliano yao serikali na Baric nadhani, niliiona kwenye blog ya Michuzi, alikuwa akiongelea mafanikio yake/ yao kwenye negotiations, unaweza kuitafuta huko hiyo video.
 

Nanye Go

JF-Expert Member
Oct 29, 2018
5,753
2,000
Mkeka ukichanika umechanika...hela ya mhindi hua hairudi.
Mnajaribu kuokoa jahazi ila ukweli Tundu Lissu alikua na chuki iliyopitiliza kiasi kwamba alitamani nchi inyimwe misaada.
Binafsi mimi huwa sielewi hii misaada tunapewa lini na nani na pesa inaenda wapi?!
Kila siku nasikia deni la taifa linaongezeka, haya madeni ni sehemu ya hiyo misaada?! Au misaada na mikopo tunayokopa ni tofauti?!
Wewe mwenzetu misaada huwa unaipatia wapi?! Binafsi hadi leo hii na umri huu mkubwa sijawahi ona msaada tunaopewa kama taifa popote, naomba msaada kueleweshwa eneo hili la misaada.
 

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,459
2,000
Binafsi mimi huwa sielewi hii misaada tunapewa lini na nani na pesa inaenda wapi?!
Kila siku nasikia deni la taifa linaongezeka, haya madeni ni sehemu ya hiyo misaada?! Au misaada na mikopo tunayokopa ni tofauti?!
Wewe mwenzetu misaada huwa unaipatia wapi?! Binafsi hadi leo hii na umri huu mkubwa sijawahi ona msaada tunaopewa kama taifa popote, naomba msaada kueleweshwa eneo hili la misaada.
Hawezi kukujibu
 

Gellangi

JF-Expert Member
Apr 11, 2016
978
1,000
Mkeka ukichanika umechanika...hela ya mhindi hua hairudi.
Mnajaribu kuokoa jahazi ila ukweli Tundu Lissu alikua na chuki iliyopitiliza kiasi kwamba alitamani nchi inyimwe misaada.
Mbona mnalilia misaada?Are we not a donor country?
Likikorogeka na kuambiwa ukweli mnasingizia kunyimwa misaada,Mara wafadhili,mabeberu,wadau wa maendeleo,wawekezaji nk,tuwaelewe msimamo wenu ni upi?
Ukweli usemwe bila mipaka wala vikwazo.Jambo lisemwalo lawezaje kuwa kikwazo cha maendeleo na hasa kama ni uongo?
 

Chige

JF-Expert Member
Dec 20, 2008
9,929
2,000
Kuna video nikiona juzi Kabudi alisema ACACIA walifuta arbitration case London, hiyo ilikuwa ni sehemu ya makubaliano yao serikali na Baric nadhani, niliiona kwenye blog ya Michuzi, alikuwa akiongelea mafanikio yake/ yao kwenye negotiations, unaweza kuitafuta huko hiyo video.
Naikumbuka hiyo kesi, ilifunguliwa na Acacia. Tusisahau tangia mwanzo Acacia walionekana kupinga moja kwa moja madai ya serikali huku parent company, Barrick ikiweka mbele suala la majadiliano na serikali!!

So, few months ago baada ya Barrick kuonesha wazi kwamba wanataka "kulimaliza" hili suala kwa majadiliano kutokana na makubaliano ya awali waliyokuwa wameafikiana na serikali, hapo hapakuwa na namna zaidi ya Acacia kufuta kesi kesi ili hatimae Barrick warudi mezani!

Kwa mfano, habari ya Reuters kuhusu Acacia kuachana na kesi ni hii hapa:-
Reuters.png

Unaona hapo hiyo habari imeripotiwa July 17, 2019.

Makubaliano ya Awali kati ya Serikali na Barrick Gold ni haya hapa:-
Barricck.png


Unaona hapo makubaliano yanaonekana ni July 19, 2019... yaani siku 2 tu baada ya Acacia kutangaza kuachana na kesi!!!

Kwahiyo ndo tunarudi pale pale... kwenye makubaliano ya awali tayari Barrick alishafahamu watatakiwa kulipa ile USD 300 Million TU, tena kwa masharti kwamba, hatimae makinikia yataruhusiwa kusafirishwa!!

Hiyo kwao ilikuwa ni advantage ndio maana Acacia wakafuta kesi! Na hapa hapa JF nilishawahi kuongea kwamba Acacia watajifanya kuendelea ku-press hard ili kuitisha serikali na hatimae wakubaliane na suala la "Kishuka Uchumba" tu, na ndicho kilichotokea!!

Sasa kama Kabudi anahisi anastahili pongezi kwa Acacia "kufuta" kesi kutokana na ushawishi wake, then we've long way to go! Kama ni kutokana na ushawishi wake, kwanini Acacia wafute kesi baada ya kuona makubaliano yameshafikiwa na badala ya kulipa yale matrilioni, hivi sasa watalipa tu mabilioni na makinikia yanaruhusiwa kusafirishwa!!
 

Yamakagashi

JF-Expert Member
Sep 19, 2016
8,682
2,000
Kwani unayafikiria haya hawa viumbe hawayajui?

Nikupe mfano mmoja wakati Lisu anapigwa risasi, Nyalandu alisema sababu ya yeye kuondoka ccm ni hilo la kuzuiwa kwenda kumuona Lisu, sio kumchangaia damu nk,
Hawa viwavi wakashangilia sana ni msaliti, alistahili kuuwawa na Boss mkubwa wakati amepatikana mbunge mwingine akasema wazi sasa Singida Mashariki watapata maendeleo

Majuzi yakamkuta ya kumkuta mwenyewe watu wale walioumizwa na ya Lisu wakaanza kufurahia kama wao walivyo fanya kwa maana ya kipimo unachopima ndicho utakachopimiwa

Leo wanakuja na unafki tumefikaje hapa wakati muanzilishi wa huu ujinga wa kutenganisha Watanzania ni huyo Boss wao

Bana eeh kila mtu ale alipopeleka mboga
 

Automata

JF-Expert Member
Mar 3, 2015
2,232
2,000
Mkeka ukichanika umechanika...hela ya mhindi hua hairudi.
Mnajaribu kuokoa jahazi ila ukweli Tundu Lissu alikua na chuki iliyopitiliza kiasi kwamba alitamani nchi inyimwe misaada.
Hakika Tindu Lisu alikua anachuki iliyopitiliza kiasi cha kutamani nchi inyimwe misaada, mikopo, itengwe na kuwekewa vikwazo

So anapoitwa msaliti kunaukweli
 

Ileje

JF-Expert Member
Dec 20, 2011
5,665
2,000
Binafsi mimi huwa sielewi hii misaada tunapewa lini na nani na pesa inaenda wapi?!
Kila siku nasikia deni la taifa linaongezeka, haya madeni ni sehemu ya hiyo misaada?! Au misaada na mikopo tunayokopa ni tofauti?!
Wewe mwenzetu misaada huwa unaipatia wapi?! Binafsi hadi leo hii na umri huu mkubwa sijawahi ona msaada tunaopewa kama taifa popote, naomba msaada kueleweshwa eneo hili la misaada.
Bila misaada na mikopo kutoka kwa mabeberu nchi hii haitawaliki. Tunapata misaada na mikopo katika kufanikisha bajeti ya serikali kuu. Bila hiyo hata mishahara serikali ingeshindwa kulipa. Pia tunapata misaada na mikopo kufanikisha utekelezaji wa miradi ya maendeleo kama ujenzi wa miundombinu ya barabara, reli, maji, umeme, meli nk. Hata baadhi ya semina na makongamano ya serikali yanafadhiliwa na fedha za mabeberu.

Hivyo puuzia kabisa majigambo ya kiongozi wetu eti nchi hii inaweza kuwa donor country badala yake ni matonya country!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom