Acheni kulima miwa ya mafuta, limeni chakula!

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,475
39,991
KUPANGA NI KUCHAGUA, KUTOCHAGUA NI KUJIUMBUA!

Na. M. M. Mwanakijiji

kwa mara nyingine tena naomba niwe mleta habari mbaya kwa Watanzania. Hili wazo la kukimbilia kulima miwa ili mpate mafuta litaifikisha nchi pabaya. Kuna maeneo mengi ambayo watu walikuwa wanalima chakula sasa wanakimbilia kulima miti ya mafuta na miwa.

Yota haya yanatokea kwa sababu ya imani ya utajiri wa haraka haraka kwani kama hatuwezi kuchimba mafuta kwanini basi tusiyazalishe kwenye mimea? Ingawa mafuta yatokanayo na mimea (biofuel) ndio mojawapo ya bidhaa adimu zaidi duniani sasa hivi, hali halisi ni kuwa kwa nchi kama ya kwetu, utajiri wa kweli hauko kwenye miwa na miti ya mbono.

Ndugu zangu, tutakuwa tumeingia mtego mbaya kabisa kama tunaamini japo on principle kuwa miwa na mimbono ndiyo itakayowatoa wakulima wetu kwenye kilimo cha kimasikini na cha kuhemea. Hivi hawa wataweza kushindana na wakulima wa nchi za magharibi ambao wameacha kulima nafaka kwa ajili ya chakula na badala yake wanaanza kulima nafaka kwa ajili ya mafuta?

Mazao ya wakulima wetu waliotoka jasho kwa wingi yatakuwa kweli na bei sawa kwenye soko la dunia ukilinganisha na mazao ya mafuta toka nchi za magharibi ambako gharama ya uzalishaji wake itakuwa chini sana kwa heka moja ukilinganisha na kwetu. Je tutakapopewa bei ya chini huko mbeleni tutalalamika kweli wakati hawa hawa viongozi wanaotutia mioyo kulima mimbono watakapokuja na kusema "ndivyo hali ilivyo kwenye soko la dunia"?

Kinachonishangaza zaidi ni jinsi gani wanasiasa wetu na wataalamu wetu wameacha kuchangamia jambo ambalo kwa hakika tuna faida ya kiushandani na kutuingiza katika kitu ambacho ni wazi kitatugeuka. Leo hii tunasikia jinsi wawekezaji kutoka Brazili na nchi nyingine wote wakikimbilia Bonde la Rufiji ili waanze kulima miwa ya mafuta kwa kutupa tumaini kuwa tutaweza kushindana na mafuta yatakayozalishwa huko kwao Brazili ambako kilimo cha miwa ni cha kisasa kweli.

Lakini zaidi kinachonisumbua nikiwa mchambuzi wa masuala haya ya kiuchumi na kijamii ni wasiwasi wangu kuwa tutakapokuwa tunachangamkia tenda ya miwa na mimbono tutaanza kuacha kulima mazao ya chakula. Hebu fikirini kwa dakika moja endapo makampuni ya magharibi yakianza kuingia Nyanda za Juu kusini na maeneo yale ya bonde la Usangu, Mbalizi, n.k yakageuzwa badala ya kulima mahindi ya chakula na kuanza kulima mahindi ya mafuta?

Sizungumzii kitu cha ndoto; Wakati kimbunga kimepiga nchi ya Mynamar (Burma) hivi karibuni mojawapo ya matatizo makubwa ya chakula yametokana na uamuzi wa utawala wa kijeshi wa visiwa hivyo kuanzisha kampeni ya kutumia Ekari 200 za mraba kupanda miti hiyo ya mimbono (jatropha) ili kuzalisha mafuta ya dizeli ambayo kwa hakika ni mafuta mazuri na ya kiwango cha juu tu. Hata hivyo ili kufanikiwa hivyo ilibidi wabadilishe baadhi ya maeneo yaliyokuwa yanatumika kulima chakula na kuyafanya yalime mimbono na hilo limekuwa gharama kubwa kwa Myanmar.

Kimbunga cha Nargis kilipopiga kimeharibu maeneo mengi ya viunga vya mpunga na nafaka nyingine na hivyo kusababisha upungufu mkubwa wa chakula. Tusije tukaingia katika mtego huo.

Wenzetu China na India ambao wamekuwa wakipanda zao hili la mimbono wamekuwa wakipanda kwenye maeneo ambayo nafaka hazistawi kwani mimbono ni miti inayostahimili ukame. Binafsi ningeona kampeni hii ya mimbono ingekuwa kwenye mikoa ya kati kama Dodoma na Shinyanga na Tabora na hata baadhi ya mikoa ambayo rotuba yake ni ya mashaka. Lakini tusipoangalia tunapoanza kugawa maeneo yenye rutuba kama bonde la Rufiji kwa kulima miwa badala ya nafaka kwa hakika tunajitengenezea njaa yetu wenyewe.

Binafsi naamini kuwa kama Watanzania wanataka kweli kunufaika na kilichomo chao na kupata utajiri kutoka hicho, basi hakuna njia nyingine isipokuwa kilimo cha chakula. Leo hii wakati dunia ina hangaika na upungufu mkubwa wa chakula Tanzania nchi iliyozungukwa na maziwa makubwa matatu, mito mingi ya misimu yote tunashindwa kuingia katika kampeni ya haraka ya kulima nafaka ili mwakani tuanze kuilisha Afrika!

Watawala wetu wamebweteka mawazo yao kwenye madini, na utalii na sasa kwenye haya mafuta lakini wameshindwa kuja na vitendo vya kweli vya kukibadilisha kilimo cha chakula nchini na kukifanya kuwa ni kilimo cha faida. Watawala wetu bado hawajaona umuhimu wa kweli wa kuhamasisha mbinu, na taratibu za kisasa za kilimo na matokeo yake wameendelea kuimba wimbo ule ule wa enzi na enzi wa "mapinduzi ya kilimo".

Saa na wakati kamaa huu ndio wakati muafaka kabisa kwa taifa letu kuongoza katika mapinduzi ya kilimo cha chakula. Cha kwanza ambacho tungeweza kufanya ni kutoa unafuu wa kodi na motisha kwa wawekezaji wa kilimo cha mazao ya chakula kuja nchini. Kubwa kabisa ni kufuta kodi yoyote (ambayo bado ipo) ya zana za kilimo, kurahisisha upatikanaji wa ardhi yenye rutuba, na zaidi ya yote kuhakikisha kuwa tuna sera itakayowafanya wananchi wa maeneo mbalimbali kuwa sehemu ya uwezekaji mkubwa wa chakula aidha kwa kuingia ubia (pale wanapoouza maeneo ya mashamba yao) na pia kama wafanyakazi (badala ya kujilimia wenyewe tu).

Pia bado naamini tungerudia mambo yale tuliyokuwa tunayafanya zamani kwa ufanisi mkubwa ambapo shule za Sekondari na Vyuo vilikuwa vinashiriki kikamilifu katika kilimo cha chakula na kujitegemea. Leo hii nashtushwa na habari kuwa Waziri Mkuu ameenda Dodoma kushiriki katika harambee ya kuchangia chakula katika shule. Hili sijui limetoka wapi kama siyo uvivu wa utendaji na uzembe wa kisiasa.

Nilikosoma mimi na bila ya shaka wale wenzangu waliosoma Bweni watakumbuka kwenda shamba kulima mahindi , alizeti, ufuta na vile vibustani vya mboga mboga. Ninakumbuka nilipokuwa shule vyakula pekee ambavyo tulikuwa tunaagzia nje ni nyama, sukari, chumvi na mchele. Maharage tulikuwa tunalima sisi wenyewe, mahindi tulikuwa tunalima na alizeti tulikuwa tunalima wenyewe na kukamua mafuta yake sisi wenyewe. Zaidi ya yote bustani zetu zilikuwa zina mboga za kila aina kama mchicha, kabichi, vitunguu na nyanya (nakumbuka zile nyanya zilivyokuwa zinapotea mara zikianza kuonesha dalili ya kuwiva).

Leo hii tumefika mahali tunafanya harambe ya kuchangia chakula!! Haya bwana nyie limeni mafuta tu, hiyo siku ikifika tutaona kama watoto na watoto wa watoto wetu na wenyewe watakaa chini kulishwa matufa ya mimbono na badala ya kutafuta miwa wajikuta wanafyonza mafuta kutoka kwenye miwa!!

Haihitaji uanasayansi kuona kuwa tunakoelekea siko, tubadili njia na tuje na sera ambayo iko balanced ili tusije tukajikuta tunatilia mkazo mafuta halafu tukishapata hizo hela za mafuta, hatuna chakula cha kununua! Kupanga kwa kweli ni kuchagua, na kuchagua ni kupangua, na ukipangua utakuwa unachagua!
 
Hili swala ni la muhimu sana lwa bahati mbaya Muungwana ameweka washauri wake walevi kutwa wanashind pale ghymkhana club.

Inahitajika sera ya nguvu kuhusu hilo jambo hasa ukiangalia kuwa kilimo ndio uti wa mgongo wa uchumi wetu na wakati ni huu kwa ardhi yetu ilivyo,ambayo sehemu kubwa bado ni virgin...tunaweza kulisha nchi zote za Afrika ya kati na kusini.....Je ni nani anyewweza kulet muongozo?
 
nchi wazalishaji wakuu wa biofuels wanasema kuwa biofuels hazichangii katika kupanda kwa bei ya chakula, kinyume na maoni ya nchi nyengine.
ila hii isiwe kisingizio cha kusema kuwa haito athiri upatikanaji wa chakula.

nchi kama tanzania, nafikiri tunahitaji kuinua kilimo kwa mazao ya kuliwa kwanza kabla ya kufikiria kuuza miwa ya mafuta kwa sababu pesa hiyo itakayopatikana yote itaenda katika kununua chakula upya.

serikali inapaswa kuwasaidia watu wanaotaka kulima mazao ya chakula, kwa kuwapa mikopo ya riba cha chini, na kuwasaidia kupata elimu juu ya ukulima wanaotaka kuufanya
 
nchi wazalishaji wakuu wa biofuels wanasema kuwa biofuels hazichangii katika kupanda kwa bei ya chakula, kinyume na maoni ya nchi nyengine.
ila hii isiwe kisingizio cha kusema kuwa haito athiri upatikanaji wa chakula.

nchi kama tanzania, nafikiri tunahitaji kuinua kilimo kwa mazao ya kuliwa kwanza kabla ya kufikiria kuuza miwa ya mafuta kwa sababu pesa hiyo itakayopatikana yote itaenda katika kununua chakula upya.

serikali inapaswa kuwasaidia watu wanaotaka kulima mazao ya chakula, kwa kuwapa mikopo ya riba cha chini, na kuwasaidia kupata elimu juu ya ukulima wanaotaka kuufanya

Gaijin.. kwa mtu yeyote aliyesoma basic Economics anatambua principle ya scarcity. Na zaidi ya yote kanuni kubwa za soko za mahitaji na ugavi (demand and supply) zinaapply kwenye suala la chakula pia. Kama mataifa mengi ambayo yalikuwa yanazalisha chakula, yakaacha kuzalisha mazao hayo ya chakula na kuanza kuzalisha mazao ya mafuta basi wanafanya mazao ya chakula kuwa scarce.

Sasa katika ulimwengu ambapo ukiacha kufanya mwingine atafanya tunatarajia kuwa kuna watu ambao watachukua shughuli za kilimo cha chakula na hivyo kuoffset madhara ya kupungua kwa chakula. Sasa mataifa ambayo yana comparative advantage katika kilimo cha chakula na yenyewe yanapoanza kulima mazao ya mafuta basi utaona kuwa tunaanza kutengeneza demand kubwa ya mazao ya chakula. Sasa kwa vile ugavi wa mazao hayo ni mdogo basi kile kidogo kilichopo kinatatufutwa na watu wengi na hivyo kusababisha bei kwenda juu.

Sasa kwenye tatizo la bei kwenda juu utaona kuwa wale wenye uwezo mkubwa wa kifedha ndio watakuwa wa kwanza kupata the little commodities za chakula. Na hili si kwa watu binafsi tu bali kwa mattaifa pia. Ndio maana mada yangu ile nyingine ya njaa ilikuwa inaangalia hili. Huko tunakokwenda nchi kama Tanzania, Kenya, Uganda n.k hazitaweza kushindana na mataifa ya magharibi kugombania chakula kidogo kilichopo.

Wakati wao (nchi za magharibi) wakati wowote wanaweza kufungua Alaska na kuingia kuchimba mafuta na kupata mafuta wanavyotaka sisi hatuna uwezo wa kuamua kulima nafaka mara moja na kwa kiasi kikubwa kwani bado kilimo chetu ni cha kujihami (subsistence farming).

Ndio maana binafsi naamini kuchangamia mimbono na miwa ya mafuta badala ya kuchangamkia uwekezaji mkubwa wa kilimo cha kisasa na cha nafaka (na hapa cha kisasa siyo kama isemavyo ilani ya CCM) bali ni kilimo cha mbinu, mashine, na uvunaji wa kisasa pamoja na uhifadhi wa mazao wa kisasa. Ni kwa sababu hiyo utaona hata kwenye kilimo wakubwa bado watatafunga magoli na matokeo yake miezi michache ijayo mtasikia Taifa letu likiomba msaada wa chakula!!
 
tatizo la viongozi wetu hawaoni mbali.
wao hawana kabisa akili ya kutizama baada ya miaka 10 mbele hali itakuwaje.
utajiri wa mali asili ya madini na mfuta upo tele tanzania, kama tunataka kutajirika haraka na tufanye hayo kwa ufanisi ila tusiingilie kilimo.
tanzania mpaka leo hii hatuli matunda hadi wakati wa msimu wake! tunashindwa kuwafundisha wakulima jinsi ya kukausha na kufunga matunda yao!.
na sio kama ni kitu kigumu. nimeona dried fruits (mananasi na ndizi) yalokuwa packed kuttoka uganda...the quality is excellent.
wao wanaweza, kwanini tushindwe sisi?
jibu la wazi ni kuwa viongozi hawana interest. wao wapo more interested na biashara za kutoa faida kwa haraka, kama migodi.....lakini wakumbuke, nchi yetu inawakulima wengi zaidi kuliko watu wengine wote
 
Gaijini.. umesema kitu kimoja muhimu sana; Watanzania tunaishi in the "now" hatutaki kuona mbali sana. Hivi miaka ishirini iliyopita wakati wa mabadiliko ya kiuchumi hakuna mtu aliyejua kuwa Dar inahitaji barabara mpya, kubwa na uongozi mzuri wa magari? Kwanini hatukujiandaa? Sasa leo hii tumekimbilia miwa na mimbono, mwakani ikitokea njaa hivi tuna udhuru kwamba ni "kazi ya Mungu"?

Kwanini wazungu wanajitahidi sana kuona mbali, wamejaliwa nini wenzetu kwenye neurons za bongo zao ambacho sisi tumenyimwa na muumba?
 
Hiyo njaa ni inevitable, na haitotokea mwakani, tayari watu wameshaanza kuhangaika
 
Mpita Njia wapi huko kwenye njaa? Kwa sababu nina wasiwasi walioshiba hawamjui mwenye njaa.. au hadi watu waanze kula tena mizizi au matunda ya sumu?
 
Haya ndiyo tunayoyazungumzia:...

Makampuni ya kigeni yanunua ardhi kubwa ya wanavijiji Pwani

2008-06-05 10:53:02
Na Joseph Shayo wa JET


Kuibuka kwa makampuni mengi yanayotafuta ardhi kwa ajili ya kilimo chama mazao yatakayozalisha nishati uoto, ni tishio kubwa kwa mazingira na lishe ya binadamu. Joseph Shayo wa JET, anaelezea zaidi.



Kwa sasa baadhi ya makampuni makubwa ya kimataifa yanazunguka katika vijiji vya wilaya tatu za mkoa wa Pwani yakitafuta na kuwashawishi wakazi wake, ili walime jatropha na miwa kwa lengo la kuzalisha nishati uoto (biofuels).

Kwa kutumia mbinu mbalimbali makampuni hayo yameweza kuwashawishi viongozi na wakazi wa baadhi ya vijiji kuwapatia ardhi ya kulima mazao hayo.

Mathalani katika wilaya ya Rufiji kampuni ya Kigeni kutoka Sweden ijulikanayo SEKAB Bio-Energy Tanzania, inatafuta kwa udi na uvumba hekta 400,000 kwa lengo la kuotesha miwa ili kuzalisha nishati uoto aina ya Ethanol.

Katika Delta ya mto Rufiji eneo maarufu kwa samaki aina ya kamba lenye miti aina ya mikoko, mwekezaji wa Kampuni ya SEKAB aliitisha mikutano ya vijiji 10 katika tarafa ya Mkongo kuanzia mwaka 2006 ikishawishi viwapatie ardhi kwa ajili ya madhumuni hayo.

Wakati maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani yakifanyika, SEKAB imefanikiwa kupata hekta 9,000 kwa ajili ya kuotesha miwa Lengo hasa ni kupata hekta 50,000 kwa ajili ya mradi huo.

Timu ya waandishi wa mazingira (JET) ikifuatana na waandishi wa toka nchi za nje na maofisa watafiti kutoka Oxfarm International, limebaini kwamba katika kijiji cha Kipo mwekezaji huyo ameahidiwa kupewa hekta 9,000 kwa kilimo cha miwa na juhudi zake zinaendelea ili apate eneo kubwa zaidi.

Katika kijiji cha Kipo, SEKAB inatarajia kuvuta maji kutoka mto Rufiji na kuyaingiza katika bwawa la Zimbwi ambalo kwa sasa ni maarufu kwa uvuvi wa samaki wa maji baridi ambalo linatoa ajira kwa watu wengi na chanzo kikubwa cha mapato kwa wavuvi.

Mwenyekiti wa kijiji cha Kipo, Bw. Kasimu Kindimba alisema wavuvi husafirisha samaki na wengine huwauza katika masoko mbalimbali ya jijini Dar es salaam.

Alisema waliamua kuwapatia SEKAB hekta 9,000 kati ya 20,000 walizoomba kwa imani kwamba wakazi wa kijiji hicho watapata ajira kutoka kwa kampuni hiyo, pamoja na huduma za afya na miundombinu zikiwepo barabara.

Hata hivyo, baadhi ya wanakijiji, hasa wavuvi wanaovua katika bwawa la Zimbwi, wana wasiwasi na maisha yao ya baadaye.

``Mimi siafiki uamuzi wa kutoa ardhi na kumpa mwekezaji, kwa sababu mradi huo utaleta uharibifu mkubwa, hasa kwa ziwa letu kwa sababu ya kuingiza maji ya mto Rufiji.

Huenda samaki wakaathirika na sisi tukakosa kitoweo`` alisema, Bw. Kindimba na kuongeza kama watafyeka msitu huo ni dhahiri kuwa maji ya ziwa yatapungua na huenda wakachukua na kulimiliki kabisa ziwa Zimbwi.

Bwawa la Zimbwi limesababisha kuwepo kwa kambi kubwa ya uvuvi, ambapo wakati wa msimu wanakuwepo watu zaidi ya 300 wanaotegemea biashara ya uvuvi wa samaki.

Mvuvi mmoja katika kambi hiyo huweza kupata jumla ya Sh 50,000 kwa siku moja samaki wanapokuwa wengi.

Wilaya ya Rufiji katika miaka michache iliyopita, ilivamiwa na kampuni moja ya uvuvi wa kamba ya African Fishing Company ambayo ilitaka kuanzisha mashamba ya kufugia samaki aina ya kamba, lakini kutokana na shinikizo la JET na wadau wengine wa mazingira mwekezaji huyo Bw. Nolan alishindwa kuanzisha mradi huo wenye athari kwa mazingira.
Delta ya Rufiji ni maarufu kwa mikoko ambayo ndio mazalia makuu ya samaki aina ya kamba na samaki wengine.

Hivyo, ufyekaji wa miti hiyo na matumizi ya madawa na mbolea katika mashamba ya miwa yataleta athari kubwa kwa mazingira.

Mkuu wa wilaya ya Rufiji, Bw. Ali Rufuga, alisema SEKAB inahitaji eneo la hekta 50,000 ili kampuni hiyo iweze kujenga kiwanda cha kuzalisha nishati ya ethanol ambayo ni nishati uoto.

``Tumepokea maagizo kutoka mamlaka za juu tutekeleze.Hatuna la kufanya. Binafsi siamini sana ahadi za wawekezaji kwa sababu mara nyingi hawazitimizi lakini mimi sina la kufanya`` alisema mkuu wa wilaya hiyo.

Alishauri serikali ipate maoni kutoka kwa wadau katika ngazi za chini kabla ya kutoa maagizo toka juu, kwa sababu wadau wa ngazi ya chini ndio wahusika muhimu wanaojua matatizo na faida za miradi.

Bw. Rufunga, akifafanua zaidi alisema,`` Mimi nina vijana wangu wengine ambao hawana ajira, baadhi yao ni wavuta bhangi. Sasa huyo mwekezaji akitoa ajira na huduma muhimu za afya na elimu na miundo mbimu, mbona wilaya yangu itapata faraja`` alisema.


Hata hivyo, Mtafiti kutoka Oxfarm International, Bi.Lucy Ibrinicombe, anasema Oxfarm imeingiwa na wasiwasi mkubwa kutokana na makampuni ya kimataifa kuanza kutafuta ardhi ya kilimo cha nishati ya uoto, wakati hivi sasa dunia inakabiliwa na ukosefu mkubwa wa chakula.

``Mara nyingi mwekezaji anaangalia tu mahitaji binafsi ya ardhi bila kujali mgawanyo wa ardhi na hasa eneo la kilimo na ufugaji `` anasema.

Akizungumzia mradi wa kuzalisha miwa kwa ajili ya kutengeneza nishati uoto, Bi Josephene Brennam Mabaye ambaye ni Mkurugenzi wa Maendeleo Afrika wa kampuni ya SEKAB, anasema uzalishaji nishati uoto hauna madhara kwa mazingira, ila ni nafasi kubwa kwa Tanzania kukua kiuchumi na kutoa mfano wa Brazil ambayo inazalisha nishati uoto kutokana na miwa.

Alisema mahitaji ya ardhi ya kuotesha miwa na mazao mengine yanayotoa nishati mbadala, yatasaidia nchi nyingi duniani kuacha kutegemea nishati itokanayo na mafuta yanayochimbwa ardhini.

Bi Nrennan, anasema licha ya kupanda kwa bei ya mafuta ya nishati ya petroli mafuta hayo kwa sasa yako katika hatari ya kumalizika duniani na kusema utafiti umeonyesha dunia yaweza kutokuwa na nishati hiyo katika miaka 50 ijayo.

Je, tutapata wapi nishati mbadala, aliuliza Bi. Brennan.

Anasisitiza kuwepo kwa mpango mkakati wa kuhakikisha kuwa nishati ya uoto inazalishwa bila kuathiri mazingira na uzalishaji wa chakula.

Anasema ili kampuni yake iweze kujenga kiwanda cha kuzalisha ethanol ni lazima kuwe na shamba la hekta 50,000 za miwa .

Anasema SEKAB imepata eneo la ukubwa wa hekta 20,000 katika wilaya ya Bagamoyo na kwa kuanzia hekta 15,000 zitalimwa miwa na hivi sasa wameanza kuotesha miche ya miwa.

Anasema SEKAB itawasaidia wanavijiji kwa kununua miwa watakayolima na pia watawapa ushauri kwa kuwatumia wataalamu wa mradi huo ili walime kilimo bora.

Kamishna wa Nishati na Madini, Bw. Bakari Mrindoko, anakiri kuwa serikali haina sera kuhusu kilimo cha nishati uoto, lakini akaeleza kuwa tayari serikali imeunda Tume ya Nishati na hivi sasa wajumbe hao wako Brazili wakijifunza ili kuwe na sera safi.

Lakini kasi ya utafutaji wa ardhi kwa ajili ya kilimo cha kuzalisha nishati uoto inatia shaka kwa wawekezaji kutofuata masharti ya Uwekezaji na sheria ya Usajili wa Ardhi ya Mwaka 2007.

Mtaalamu wa kitengo cha uhamishwaji wa nguvu, Dk Khoti Kamanga, anasema msukumo wa kusaka ardhi ya uwekezaji wa nishati uoto unatoka nje na hasa nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya (EU) ambao unataka kuendeleza matumizi ya nishati uoto kama pia njia mojawapo ya kupunguza hewa ya ukaa.

Anaeleza kuwa Tanzania haijafanya utafiti wa kutosha ili kuruhusu uzalishaji wa nishati uoto.
``Hakuna sheria, sera wala kanuni zinazosimamia wawekezaji wa nishati uoto wanaomiminika hapa nchini kutafuta ardhi.

Kisheria anasema kampuni hayo yana paswa kufanya Utafiti wa Athari za Mazingira( Environmental Impact Assessment - EIA) ya miradi yao, kabla ya kuanza kuingia mkataba ya kumiliki ardhi na wanakijiji.

Baada ya kupata EIA ripoti hiyo kwa Baraza la Taifa la Usimamizi na Hifadhi ya Mazingira (NEMC) ndipo aanze kufanya vikao na wanavijiji ili kujua mwekezaji atahitaji ardhi kubwa kiasi gani kwa kuzingatia mahitaji ya wanakijiji na mfumo wa ugawaji wa ardhi.

Alisema NEMC, watatoa fursa ya kusikiliza maoni ya jamii kuhusu mradi wa mwekezaji ambaye anapaswa kuweka matangazo kwenye magazeti kuhusu nia yake na pia mabango katika eneo atakalohitaji kwa mradi wake.

Dk Khoti alisema hayo yote hayajafanyika ila kuna taarifa kuwa wawekezaji hao wameshaanza kuotesha miche ya miwa na tayari wanamiliki mashamba ambapo sasa wanatafuta hati za umiliki wa ardhi.

Anatahadharisha iwapo Tanzania itaingia `` kichwa kichwa`` kwa kuwakaribisha wawekezaji wa nishati uoto bila kuangalia madhara yake katika mazingira na upatikanaji wa chakula, wananchi wake watajikuta hawana ardhi na watabakia kuwa manamba katika mashamba ya wawekezaji.

Pia kuna uwezekano mkubwa wa uharibifu wa mazingira hasa katika bonde la mto Rufiji. Katika wilaya ya Kisarawe, Mwekezaji mwingine, Sun Biofuels (T) Ltd baada ya ushaswishi kwa wanavijiji, amepata ya hekta 18,000 kwa ajili ya kuotesha jatropha katika vijiji kumi na moja ambavyo vimeingia mkataba na kampuni hiyo katika eneo linalopakana na msitu wa Hifadhi wa Ruvu.

Mkurugenzi Mkuu wa Sun Biofuels anasema, baada ya kuotesha jetrpha wanatarajia kuwapatia ajira wakazi wa vijiji hivyo na kutoa huduma za afya na pia kujenga miundo mbinu.

Hata hivyo, eneo hilo ambao lina vichaka na misitu minene litalazimika kufyekwa na baadaye kuotesha jetropa.

Kutokakana na kutofanywa kwa Utafiti kuhusu athari za miradi hiyo katika wilaya za Bagamoyo, Kisarawe na Rufiji hakuna ajuaye mazingira ya maeneo hayo yatakuwaje baada ya mradi hiyo kuanza.

Lakini ukweli ni kwamba miradi ya mashamba hayo, miti ya asili na uoto wa asili na wanyama wataathirika.

Wakati maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani yakifanyika ni muhimu kuchukua hatua za haraka kudhibiti mfumo wa utwaaji wa ardhi katika vijiji ikiwa pamoja na kuangalia umuhimu wa chakula kwa taifa badala ya kukimbilia faida za kiuchumi tu.
 
Sasa katika ulimwengu ambapo ukiacha kufanya mwingine atafanya tunatarajia kuwa kuna watu ambao watachukua shughuli za kilimo cha chakula na hivyo kuoffset madhara ya kupungua kwa chakula.

Ukweli tupu Mzee Mwanakijiji, in the long run madhara ya upungufu wa mazao ya chakula yatakuwa offset.

Sasa mataifa ambayo yana comparative advantage katika kilimo cha chakula na yenyewe yanapoanza kulima mazao ya mafuta basi utaona kuwa tunaanza kutengeneza demand kubwa ya mazao ya chakula.

Again in the long run, demand ya mazao ya chakula ikiwa juu, itachochea uzalishaji wa mazao ya chakula.

Sasa kwa vile ugavi wa mazao hayo ni mdogo basi kile kidogo kilichopo kinatatufutwa na watu wengi na hivyo kusababisha bei kwenda juu.

In the long run, kama bei za mazao ya chakula zitakuwa juu zaidi ya zile za mazao ya mafuta, tutarudi pale pale, hayo mataifa yaliyokuwa na comparative advantage kwenye mazao ya chakula yatarudi kuzalisha mazao ya chakula, kumbuka yatakuwa kwenye comparative disadvantage yatakapokuwa yanazalisha mazao ya mafuta, na hili yaendelee na mazao ya mafuta basi bei za mazao hayo lazima iwe nono mno ku-offset disadvantage waliyonayo dhidi ya mazao ya mafuta.

Anyway, kanuni za uchumi haziko nyoofu (linear) na zinapokuwa applied kwenye hii issue wachumi watakuambia kwamba in the long-run tutarudi pale pale, mana kila kitu kitaji-offset na kuji-onset over and over.
 
tatizo la viongozi wetu wana mambo ya zamani sana ushauri wa kitaalamu siku zote iwa hawazingatii kabisa.Watakacho fikiri wao ndo hicho hicho kitakuwa na watabaki kung'ang'ania likitokea balaa la njaa wanaaanza kutupiana lawama.
 
Ukweli tupu Mzee Mwanakijiji, in the long run madhara ya upungufu wa mazao ya chakula yatakuwa offset.

Ndiyo lakini yatakuwa offset na wakulima wa wapi Africa au Nchi za Magharibi?



Again in the long run, demand ya mazao ya chakula ikiwa juu, itachochea uzalishaji wa mazao ya chakula.

Ndio nani atakuwa katika advantage ya kuzalisha mazao ya chakula endapo bei yake itakuwa juu? sisi waafrika au wamagharibi?

In the long run, kama bei za mazao ya chakula zitakuwa juu zaidi ya zile za mazao ya mafuta, tutarudi pale pale, hayo mataifa yaliyokuwa na comparative advantage kwenye mazao ya chakula yatarudi kuzalisha mazao ya chakula,

Kumbuka hizi bidhaa mbili (chakula na mafuta) siyo mbadala kwamba unaweza kuchagua kula badala ya mafuta au kinyume chake; Hivyo, kwa kadiri ya kwamba kutaendelea kuwa na mahitaji ya mafuta (kitu ambacho sioni sababu kwanini kisiwe) basi kama ugavi hautatosha au utakuwa pungufu basi bei itaendelea kuwa juu; na kama mahitaji ya chakula yataendelea kuwa juu (kwa sababu watu wataendelea kula) sioni sababu kwanini bei ishuke wakati ugavi bado ni mdogo.

Matokeo yake basi utaone kuwa bei ya mafuta na bei ya chakula havitahusiana moja kwa moja na hivyo kusababisha vyote viwili kuwa adimu (scarce). NI kwa sababu hiyo basi ile dhana ya uchumi ya "division of labor by specialization" inapokuja. Na ndio maana binafsi naamini we have to specialize in something that we have a bigger comparative advantage (food production) kuliko kujiingiza katika kitu ambacho tukilinganisha hatuna faida kubwa nacho (biofuel production).

kumbuka yatakuwa kwenye comparative disadvantage yatakapokuwa yanazalisha mazao ya mafuta, na hili yaendelee na mazao ya mafuta basi bei za mazao hayo lazima iwe nono mno ku-offset disadvantage waliyonayo dhidi ya mazao ya mafuta.

Sasa kwenye nchi ambazo zina diversity katika uchumi wao ni rahisi sana kufanya yote mawili kwa uzuri tu, lakini kwa nchi kama za kwetu ambazo uchumi wetu kimsingi bado ni wa aina moja itakuwa kazi sana kushindana katika soko la dunia. Lakini tukitaka kweli kushindana, I still believe ni massive infusion of capital katika Agriculture investment. Nothing less than that. And the capital I'm talking about not just pouring money bali mambo mengine mengi ambayo kwa kweli yanaweza kubadilisha kilimo chetu na kukifanya kiwe cha kisasa kweli.

Anyway, kanuni za uchumi haziko nyoofu (linear) na zinapokuwa applied kwenye hii issue wachumi watakuambia kwamba in the long-run tutarudi pale pale, mana kila kitu kitaji-offset na kuji-onset over and over.[/QUOTE]
 
Mimi navyojua miwa haistawi kila mahali hivyo sioni kama kuna ubaya gani Watu wanaokaa sehemu ambazo miwa inastawi walime lakini maeneo mengine walime chakula. Tatizo kubwa si kulima miwa bali technology ya kutengeneza hayo mafuta ni ya juu na ina gharama sana. Tanzania inatakiwa kufanya mpango wa uwezekano wa kutumia Natural Gas ambazo tunazo za kutosha. Kuna technologia ya Magari ya Gas au Mchanganyiko na mafuta.Hata chakula Tanzania tatizo kubwa ni Technologia ya kilimo haiwafikii wakulima na barabara si imara. Productivity ya mashamba siyo nzuri
 
Mzee Mwanakijiji, pamoja ya kwamba hukuelewa hoja mzima ya posting yangu, maswali yako mazuri na point zako pia ni sawia.

Kwa ufupi hoja yangu ni kwamba, kanuni au nadharia za uchumi kama ulivyozielezea kwenye post yako ambayo nili inukuu, haziko nyofu wala simple kama ulivyokuwa umezipanga. Madhara ya kupanda na kushuka kwa bei katika nadharia ya uchumi lazima yaangaliwe both in short-run and in long-run, na nadharia hii ina apply sio tu katika suala la mazao ya chakula vs ya mafuta, bali katika bidhaa zote. Sasa uki apply nadharia ya uchumi kwa suala hili na kutazama short-run na long-run, nadharia ya uchumi huru wa ushindani itakuambia kwamba in the long-run tutarudi pale pale. Hii ndio hoja yangu.

Baada ya kuirudia hoja yangu, labda nikujibu tu kwa nadharia maswali yako magumu ambayo kwa kweli yanahitaji volumes za vitabu kuyajibu kikamilifu, so bare with me.

Ndiyo lakini yatakuwa offset na wakulima wa wapi Africa au Nchi za Magharibi?

Kama tunaongelea suala la njaa, na tunaikubali nadharia kwamba madhara ya njaa yatakuwa offset, sidhani kama ina matter wakulima gani wana offset madhara hayo.

Ndio nani atakuwa katika advantage ya kuzalisha mazao ya chakula endapo bei yake itakuwa juu? sisi waafrika au wamagharibi?

Kwa nadharia ya kiuchumi, it really doesn't matter who has comparative advantage, as long as there is free trade. Vile vile comparative advantage wala sio kitu kinachoshushwa kutoka kwa mungu; it is human-made. Afrika ikiamua inaweza kuwa na comparative advantage katika mazao ya chakula, kadhalika India ikiamua inaweza kuwa na advantage.

Kumbuka hizi bidhaa mbili (chakula na mafuta) siyo mbadala kwamba unaweza kuchagua kula badala ya mafuta au kinyume chake; Hivyo, kwa kadiri ya kwamba kutaendelea kuwa na mahitaji ya mafuta (kitu ambacho sioni sababu kwanini kisiwe) basi kama ugavi hautatosha au utakuwa pungufu basi bei itaendelea kuwa juu; na kama mahitaji ya chakula yataendelea kuwa juu (kwa sababu watu wataendelea kula) sioni sababu kwanini bei ishuke wakati ugavi bado ni mdogo.

Mzee Mwanakijiji kwa kiasi upo sahihi ila umechanganya mambo mawili. Kwanza umechanganya substitution ya uzalishaji na substitution ya ulaji. Substitution ya uzalishaji inayofanywa na mzalishaji inachochewa profit za kitu anachozalisha, mfano mkulima anayelima mahindi yuko tayari kulima bangi kwa sababu tu bangi inampa faida, sasa huwezi kusema kwanini kaacha kulima mahindi ati tu kwa sababu bangi hailiwi na watu hawataacha kula mahindi, na kudai kwamba hizi bidhaa mbili haziwezi kuwa substituted, kwa mzalishaji kila zao au bidhaa ni mbadala.

Pili, umechanganya madhara au dhana ya bei kuwa juu. Kupanda kwa bei za chakula tunakozungumzia hapa ni kule kunakotokana na uhaba wa chakula (an upward shift of supply curve), sio kunakotokana na, kwa mfano kupanda kwa bei za pembejeo (movement along supply curve). Kupanda kunakotokana na uhaba kunasababisha new entries (wakulima wapya for this case)katika uzalishaji kwasababu kunaleta profit kwa wazalizashaji, kwa sababu mahitaji ya chakula kama ulivyosema yatabaki kama mwanzo. Hivyo basi kama mahitaji ni responsive to price changes, utategemea in the long-run bei ya chakula ibaki kama mwanzo au ishuke.
 
.... umechanganya madhara au dhana ya bei kuwa juu. Kupanda kwa bei za chakula tunakozungumzia hapa ni kule kunakotokana na uhaba wa chakula (an upward shift of supply curve), sio kunakotokana na, kwa mfano kupanda kwa bei za pembejeo (movement along supply curve). Kupanda kunakotokana na uhaba kunasababisha new entries (wakulima wapya for this case)katika uzalishaji kwasababu kunaleta profit kwa wazalizashaji, kwa sababu mahitaji ya chakula kama ulivyosema yatabaki kama mwanzo. Hivyo basi kama mahitaji ni responsive to price changes, utategemea in the long-run bei ya chakula ibaki kama mwanzo au ishuke.

Mkuu mimi nnamini kuna factors nyingi tu zinzazofanya chakula kupanda bei.....moja kubwa kabisa ni kupanda bei ya mafuta hii nadhani ndilo msingi...kwa sababu mafuta yanapopanda bei inakuwa catalyst ya kila kitu ,pembejeo,mbegu,..n.k... pili kubwa zaidi ni ile demand ambayo inatokana na population kuwa kubwa.
 
Mkuu mimi nnamini kuna factors nyingi tu zinzazofanya chakula kupanda bei.....moja kubwa kabisa ni kupanda bei ya mafuta hii nadhani ndilo msingi...kwa sababu mafuta yanapopanda bei inakuwa catalyst ya kila kitu ,pembejeo,mbegu,..n.k... pili kubwa zaidi ni ile demand ambayo inatokana na population kuwa kubwa.

Nakubaliana nawe kwa 100%
 
Mgonjwa nimekupata sana na hasa msisitizo wako wa "in the long run" na ndani yake kuna ukweli mkubwa mno. Ninachosema ni hivi:

Nchi za magharibi kwa kiwango kikubwa sana zimeachana na uchumi unaotegemea kilimo. Wenzetu sasa hivi wanategemea zaidi teknolojia, viwanda na biashara ya mambo ya fedha n.k Kilimo kilimo; wao wametengeneza uchumi mbali sana na kilimo. Leo hii kwa Marekani ni karibu asilimia moja tu ndio imeajiriwa katika Kilimo moja kwa moja. Hata hivyo hiyo asilimia moja inazalisha kwa ufanisi mkubwa sana kiasi kwamba kiasi cha mazao yanayozalishwa kwa kila hekta ni kikubwa mno ukilinganisha na nchi kama ya kwetu ambapo karibu asilimia 80 imeajiriwa katika kilimo.

Sasa pointi yangu mimi ni kuwa kwa vile mataifa ya magharibi yanazidi kwenda mbali na kilimo then someone has to come in and take advantage of that. Na ninaamini kuwa Afrika inaweza kabisa kuulisha ulimwengu mzima na watu wakatajirika kwa kilimo. Sasa linapokuja suala la mafuta ya mimbono na nishati ya miwa tumeanza kuingia kwenye mtego wa kuhudumia teknolojia na viwanda vya wakubwa kwa kuzalisha wanachokihitaji wao na hatutotumia nafasi yetu katika kuzalisha chakula.

Mjasiriamali mzuri ni yule ambaye anaona nafasi na anaamua kuitumia; Kutokana na upungufu wa chakula sasa hivi duniani Tanzania ingeweza kabisa kuwa mjasiriamali na kuchakarika kupanua kilimo cha chakula. Kwa vile ugavi wa chakula umepungua na mahitaji bado yameongezeka na hivyo kufanya bei ya chakula iwe juu kuliko kawaida basi Tanzania ingeamua kuingia katika biashara hiyo ili kwa muda mfupu watu waweze kutumia chakula kama jinsi ya kujijengea utajiri.

Ninachoona mimi sasa hivi ni kuwa watawala wetu hawana mpango wala nia ya kuwahamasisha wakulima wa Tanzania kuwa wazalishaji wanaotegemewa kwa chakula duniani.

Sasa matokeo yake (ni kile unachosema haijalishi nani anakuja kuoffset) ni kuwa Hali itakapozidi kuwa mbaya na Afrika kuonekana kutoweza kumudu uzalishaji wa chakula basi Mataifa ya magharibi yatarudi na kuanza kuwekeza katika kilimo cha kisasa zaidi na kuzalisha vingi zaidi na hivyo kuua soko tulilokuwa tunalitegemea. Mazao yao yatakuwa bora, yatahifadhiwa vizuri na na itakuwa rahisi kuyasafirisha. Sisi bado tutakuwa tunahangaika na "Lumbesa" na vikwazo vingine 1001 kiasi kwamba hadi gunia la nafaka lifike sokono ile value added inafanya gunia hilo liwe ghali kwenda na wakati mwingine zaidi ya gunia la kigeni.

Sasa Marekani na Ulaya Magharibi wakianza tena kuzalisha mazao ya chakula na hasa hizi GMO kweli sisi tutakuwa na nafasi yoyote ya kushindana nao katika biashara?
 
Mgonjwa nimekupata sana na hasa msisitizo wako wa "in the long run" na ndani yake kuna ukweli mkubwa mno. Ninachosema ni hivi:

Nchi za magharibi kwa kiwango kikubwa sana zimeachana na uchumi unaotegemea kilimo. Wenzetu sasa hivi wanategemea zaidi teknolojia, viwanda na biashara ya mambo ya fedha n.k Kilimo kilimo; wao wametengeneza uchumi mbali sana na kilimo. Leo hii kwa Marekani ni karibu asilimia moja tu ndio imeajiriwa katika Kilimo moja kwa moja. Hata hivyo hiyo asilimia moja inazalisha kwa ufanisi mkubwa sana kiasi kwamba kiasi cha mazao yanayozalishwa kwa kila hekta ni kikubwa mno ukilinganisha na nchi kama ya kwetu ambapo karibu asilimia 80 imeajiriwa katika kilimo.

Sasa pointi yangu mimi ni kuwa kwa vile mataifa ya magharibi yanazidi kwenda mbali na kilimo then someone has to come in and take advantage of that. Na ninaamini kuwa Afrika inaweza kabisa kuulisha ulimwengu mzima na watu wakatajirika kwa kilimo. Sasa linapokuja suala la mafuta ya mimbono na nishati ya miwa tumeanza kuingia kwenye mtego wa kuhudumia teknolojia na viwanda vya wakubwa kwa kuzalisha wanachokihitaji wao na hatutotumia nafasi yetu katika kuzalisha chakula.

Mjasiriamali mzuri ni yule ambaye anaona nafasi na anaamua kuitumia; Kutokana na upungufu wa chakula sasa hivi duniani Tanzania ingeweza kabisa kuwa mjasiriamali na kuchakarika kupanua kilimo cha chakula. Kwa vile ugavi wa chakula umepungua na mahitaji bado yameongezeka na hivyo kufanya bei ya chakula iwe juu kuliko kawaida basi Tanzania ingeamua kuingia katika biashara hiyo ili kwa muda mfupu watu waweze kutumia chakula kama jinsi ya kujijengea utajiri.

Ninachoona mimi sasa hivi ni kuwa watawala wetu hawana mpango wala nia ya kuwahamasisha wakulima wa Tanzania kuwa wazalishaji wanaotegemewa kwa chakula duniani.

Sasa matokeo yake (ni kile unachosema haijalishi nani anakuja kuoffset) ni kuwa Hali itakapozidi kuwa mbaya na Afrika kuonekana kutoweza kumudu uzalishaji wa chakula basi Mataifa ya magharibi yatarudi na kuanza kuwekeza katika kilimo cha kisasa zaidi na kuzalisha vingi zaidi na hivyo kuua soko tulilokuwa tunalitegemea. Mazao yao yatakuwa bora, yatahifadhiwa vizuri na na itakuwa rahisi kuyasafirisha. Sisi bado tutakuwa tunahangaika na "Lumbesa" na vikwazo vingine 1001 kiasi kwamba hadi gunia la nafaka lifike sokono ile value added inafanya gunia hilo liwe ghali kwenda na wakati mwingine zaidi ya gunia la kigeni.

Sasa Marekani na Ulaya Magharibi wakianza tena kuzalisha mazao ya chakula na hasa hizi GMO kweli sisi tutakuwa na nafasi yoyote ya kushindana nao katika biashara?

Nimekuelewa mkuu, yote uliyoyaongea ni sahihi.
 
Hongera san Mzee MJJ naona hoja yako muhimu imemfikia hata Mkuu Kofi Annan

African nations should be wary of growing biofuels on prime farm land or risk uprisings triggered by food shortages, former UN Secretary-General Kofi Annan said on Wednesday. African governments trying to produce biofuels, whether from sugarcane or other products, have to be careful to protect their essential farm lands, he told Thomson Reuters on the sidelines of the FAO summit to combat the food crisis. [Thomson Reuters/Factiva]

"Africa needs strong leaders who will connect with the global community and follow up on the many promises made to help pull the continent out of poverty, officials said at the World Economic Forum (WEF) on Wednesday.

The 18th WEF on Africa began in South Africa's second biggest city and would discuss how the continent could sustain recent strong economic growth and tackle challenges including soaring food and fuel prices...Senior delegates said as Africa's development continually topped the world agenda, leaders on the continent should follow up on pledges to help the continent out of its poverty trap. …" [Thomson Reuters/Factiva]


Na mimi namkanya tena, JK ole wako kutokee balaa ya njaa nchini...UFISADI+NJAA=?...
 
Back
Top Bottom