Acharazwa viboko 12 kwa kubaka mwanafunzi. Asema ibirisi wa mapenzi ndiye aliyemshawishi kufanya yote hayo

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,499
9,279
MAHAKAMA ya Mkoa wa Lindi, imemuhukumu mkazi wa Kata ya Nyengedi, Kassimu Bidhali Chilumba (18), kuchapwa viboko 12 makalioni, baada ya kupatikana na kosa la kumbaka mwanafunzi.

Mtuhumiwa hiyo alimbaka mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Nyengedi (jina limehifadhiwa).

Hukumu hiyo ilitolewa mwishoni mwa wiki na Hakimu wa Mahakama hiyo, Magala Muyonga, baada ya kuridhishwa na ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka, ambapo mshtakiwa alikiri kutenda kosa.

Kabla ya kutolewa kwa hukumu hiyo, mshtakiwa aliulizwa kama ana sababu zitakazoishawishi mahakama isimpe adhabu kali, kwa madai ni mkosaji wa mara ya kwanza, ibirisi wa mapenzi ndiye aliyemshawishi kufanya yote hayo, hivyo anajutia, huku akiahidi kutorudia kosa.

Baada ya utetezi huo, Hakimu Muyonga alimuuliza mwanasheria wa serikali kama ana kumbukumbu ya makosa ya zamani ya mshtakiwa na kujibu hana, ingawa aliiomba Mahakama kumpatia mshtakiwa adhabu kali ili iwe fundisho kwake na wengine wenye na tabia hiyo.

Hakimu Muyonga akitoa hukumu katika Shauri hilo namba 512020, kupitia vifungu vya sheria 130 (i) (2) (e) na 131 (2) (a) Sheria ya Elimu mwaka 2019, alisema amesikiliza maombi za pande zote mbili na kumuhukumu mshtakiwa Chilumba kuchapwa viboko 12 makalioni.

Awali ilidaiwa na Mwanasheria wa Serikali, Godfrey Mramba, kuwa mshtakiwa alimbaka mwanafunzi huyo wa kidato cha tatu Juni 5, mwaka huu, majira ya alasiri.

Mramba alidai mtuhumiwa alikamatwa eneo ambalo kinajengwa choo kipya, kilichokuwa kinajengwa nyumbani kwa mzazi wa mtuhumiwa, wakati mwanafunzi huyo akiwa anapita eneo la nyumba hiyo.
 
khaaaa, kwahio kaishia viboko tuuu?
Huyu ana mungu wake..
Angekuta upepo umekaa vibaya

Kubaka = 30,
Mwanafunzi = 30,
Under 18 = 30,
mara paaap na Mimba =30,
Mara tena iwe kinyume na maumbile = 30,
Ubao unasoma 150.

Hakimu naye akiongeza marupu rupu yake ya kazi, unasikia Anagonga lile rugu lao paaap, Miaka 200 a.k.a karne 2,

Mpaka hapo Kwisha habari yake, Mungu aliapa hamna binadamu atapitisha miaka 120(Mwanzo 6.3), kinachofuatia ni kuanika tuu maturubai in advance.

Huyu kama ni upepo, basi ana upepo na jamhuri, wewe una upepo wa selo, iga uone.
 
khaaaa, kwahio kaishia viboko tuuu?
Huyu ana mungu wake..

Angekuta upepo umekaa vibaya
Kubaka = 30,
Mwanafunzi = 30,
Under 18 = 30, na malupu lupu ya hakimu inasoma 100yrs, a.k.a karne, mara paaap na Mimba =30, Mara tena Iwe kinyume na maumbile = 30..
Karne na nusu.

Huyu Kama ana akili atabadilika
marupurupu,..... Karne....
 
Huyo pepo wa mapenzi mbona anaubaguzi!! Hatuoni na sisi wenye uchu wa mapenzi aje sasa ili nasi wengine tupate ka experience ka kubaka😂😅
Halafu adhabu yanapewa makalio utafikiri ndo yalibaka..😅
 
Adhabu ya kubaka mimi nilijua ni miaka 30 jela. Lini imebadilika na kuwa viboko 12? Ama hakimu naye anatoka huko huko Lindi na kwa hiyo ameona ni kitu cha kawaida kwa kadiri ya utamaduni wao?
Mkuu itakuwa mbakwaji alikuwa hapigi kelele
 
Wanasheria wetu humu ,njooni mtoe ufafanuzi sisi malaymen haituingii akilini kutoka miaka 30 mpaka mikwaju 12 inakuaje kuaje hapa ?Kwa huyu bazazi.
 
Tz unaweza ukabambikiwa kesi ya ubakaji na ukaozea jela..ila leo mbakaji kala viboko tu
 
Back
Top Bottom